Biden kutuma msaada wa mwisho kwa Ukraine kabla ya kuondoka madarakani

akili kisoda

Member
Joined
Oct 31, 2024
Posts
17
Reaction score
38
Raisi wa nchi ya Marekani Joe Biden amepanga kutoa mabilioni ya dollar kwajili ya masuala ya kijeshi huko nchini Ukraine kabla hajaachia ngazi rasmi mwezi January. Hii inakuja huku kukiwa na mkanganyiko kutokana na matamshi ya Donald Trump ambaye mara kadhaa kwenye kampeni zake alikuwa akikosoa vikali jinsi serikali ya Joe Biden ilikuwa mstari wa mbele kuchochea vita pale ulaya mashariki.

Na mara kadhaa alisema ataimaliza vita iliyopo ulaya mashariki ndani ya masaa 24 tu akiwa ni raisi wa nchi ya Marekani.

Ushindi wa Trump dhidi ya Kamala Harris umeibua wasiwasi mkubwa kwa serikali ya Kiev kuwa huenda isipate tena msaada wa kijeshi kama ambavyo ilikuwa inasadiwa na serikali ya Joe Biden. Hivyo Biden amejiandaa kutuma kifurishi cha mwisho cha msaada nchini Ukraine kabla hajaachia ngazi.

Baada ya kuchaguliwa kwa Donald Trump kama raisi wa nchi ya Marekani, raisi wa Ukraine Volodymir Zelenksy alikuwa ni moja ya viongozi wa kwanza kumpongeza Trump kwa ushindi huku akiamini kuwa anategemea ushirikiano wa Marekani na nchi yake utazidi kuendelea kama awali

Wakati wa kampeni, Trump aliwahi kukaririwa akisema kuwa raisi wa Urusi Vladimir Putin asingefanya uvamizi wowote nchini Ukraine 2022 endapo yeye angekuwa kwenye ikulu ya White House kwa kipindi kile, hata baada ya kuchaguliwa atahakikisha anamaliza vita ndani ya masaa 24 tu.

Trump alipendekeza kuwa Ukraine inapaswa kuachia maeneo yake kwa Urusi ili kufikia makubaliano baina ya pande zote mbili japo ni kitu ambacho Ukraine ilikitupilia mbali huku serikali ya Joe Biden nayo ikiwa haiko tayari kufanya hivyo.

USA imepanga kutoa msaada wa dollar bilioni 9 kwa Ukraine ikiwa ni msaada wa mwisho kabla ya Joe Biden kuondoka madarakani.

Via Al Jazeera

FB_IMG_1731077759650.jpg
 
View attachment 3147227
Marekani wa nataka kutawala dunia tu na kusambaza ushoga tu
 
Biden kajichanganya kalusu Ukraine ishambulie Russia kwa silaa za masafa marefu urusi kajbu pigo mojo kimya wamefyata
 
Back
Top Bottom