Bidhaa feki na duni zinatumaliza Watanzania

Mtafiti77

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2011
Posts
1,877
Reaction score
2,314
Ndugu wana JF, suala la bidhaa feki na duni limekuwa ni changamoto kubwa. Nina mfano mzuri kupitia mavazi. Binafsi, nimekuwa nikiishi kwa kuvaa mitumba kwa muda mrefu kwakuwa nimekuwa na mtazamo hasi dhidi ya nguo "special" au tuseme za dukani. Lakini, siku za hivi karibuni mitumba imekuwa adimu mno hasa kwa baadhi ya mikoa, hali iliyonifanya kugeukia dukani. Baada ya kuvaavaa suruali zile za elfu 25 na 30, nikajikuta nguo zinapauka baada ya kufuliwa mara mbili au tatu.

Hali hii sikuridhika nayo, kwakuwa ninajua kusoma na kuandika, nikawa ninapitia tovuti za wazalishaji na wauzaji wakubwa wa mavazi duniani, mfano, Banana Republic, H&M, Zara n.k.Huku nikagundua kuwa mavazi ni ghali kwa kulinganisha na huku kwetu. Pia, niliamini kuwa bidhaa halisi ni ghali. Nikiwa na elimu hii, nikaaanza kuwinda maduka makubwa kabisa jijini Dar es Salaam. Nikisema makubwa ninadhani ninaeleweka, yale maduka unakowakuta kina fulani wenye kuchanganya Kiswahii na Kiingereza. Huwezi amini, nilinunua suruali 4 aina ya kadet kila moja kwa 150,000, lakini, nguo hizi hazikumaliza hata miezi sita, zilipauka balaa. Aidha, nilinunua kashati ka linen, cha mikono mirefu na kenyewe baada muda mchache kanafumuka mikononi. Na nguo hizi zimewekwa hadi lebo ya mtengenezaji, tena wauzaji ni mawakala.

Sasa ninajiuliza, nikimbilie wapi? Kumbe waweza kuwa na hela hapa Tz na bado usipate kitu cha ukweli? Siwezi kujigamba kwamba 150,000 ni hela kubwa kiviile maana huko mbele, kutegemea na ubora na jina,unaweza usipate nguo fulani kwa hela hiyo.

Mnaofahamu bidhaa za mavazi, ninaomba mnipe shule wapi hapa Tz ninaweza kupata nguo mpya zenye uhalisia. Maana sasa hata haya maduka makubwa ninayaogopa.Mitumba siku hizi mpaka uweke oda kwa muuzaji anaefuata mzigo Nairobi.

Siku njema
 
Kuna vifaa vya electronics mkuu ni majanga hatari yaan kama. Ni umeme unaunguza nyumba mchana kweupe! Sijui TBS na FCC wamabadilishiwa majukumu?
 
Huko ndiyo usiseme maana athari zake ni kubwa sana. Kinachokera ni kwamba unaweza kuwa na hela zako na bado usipate bidhaa bora hasa kama si mjuzi.
 
Mi nadhani ni sisi wenyewe tunapenda ivi vitu maana wsle wauzaji wanaoleta vitu original hatuvinunui kwa madai ya kwamba bei zao ni kubwa ni ivyo tunapenda vya bei ndogo ivyo na wauzaji wanakuwa hawana namns nyingine zaidi ya kuleta vifaa vile vya bei nafuu tuvyoitaji
 
Hili lipo kwa kweli. Watanzania wengi tumekuwa na mazoea hayo ya kupenda vya bei ndogo bila kuchanganua ubora na kiasi. Matokeo yake hata mwenye nazo bado ananunua vitu vya kiwango duni sababu ya mazoea. Lakini, ukisoma post yangu hapo juu, kuna maduka yanajifanya kuzima kiu ya wale wanaohitaji vya ukweli lakini bado ni walaghai.
 
Kiukweli hili swala linaumiza kichwa sana, mkuu naona kama vile ulikuwa pamoja nami katika kuwaza. Maana juzi nlikaa nikaangalia Kadett zangu zilivyopauka nikakosa jibu, mpaka nikajiuliza au mimi ndio sikufwata manual of instruction. Lakini kila nikitafakari naona hapana, ni kweli hizi industries zimevamiwa, vitu fake ni vingi madukani kuliko kawaida. Kiukweli Mchina ameharibu soko vibaya mno.
 
Bidhaa halisia mara nyingi ni ghalama sana na wengi wetu wenye kuhitaji izo bidhaa tunashindwa kuafford costs na ndio maana wauzaji nao wameamua kutuletea bidhaa zisizo na ubora kulingana na vipato vyetu
 
Kabisa mkuu. Mimi niliamini sana hapo awali kuwa kupenda vya chee ndiyo kunatumaliza, nikaji-upgrade, kutoka suruali za 20, 30,.. hadi za shilingi 95 hadi 150. Lakini sioni mabadiliko. Kuna wakati nikikaa vema ninaagiza nje toka kwa rafiki zangu wanaosoma huko.Sasa hii ni changamoto.
 
Bidhaa halisia mara nyingi ni ghalama sana na wengi wetu wenye kuhitaji izo bidhaa tunashindwa kuafford costs na ndio maana wauzaji nao wameamua kutuletea bidhaa zisizo na ubora kulingana na vipato vyetu

Ndugu, mimi na baadhi ya wachangiaji wengi tu hapa wanakiri hili, lakini jikusanye weee na vihela vyako, kanunue hizo wanazosema za bei uone. Wengi ni walaghai tu. Labda uniambie hata nchi za mbele hakuna suruali yenye afadhali kwa shilingi 100,000, 150,000 hadi 200,000 hapo nitakubali. Haya maduka yetu yanauza nguo za bei hizi lakini bado zina ubora mdogo sana.
 
Ni kweli ndugu bidhaa nyingi tunazoletewa kutoka nje au ata apa apa kwetu ni chini ya viwango ila kulingana na vipato vyetu vya kila siku hatuna budi kununua ivyo ivyo ili kukidhi mahitaji yetu.. Jaribu kuvuta taswira kwa yale maduka yenye bidhaa halisia mara nyingi wanunuaji ni wachache mnooo ila maduka yenye low quality products kila siku bidhaa zinaisha
 
Sawa. Sasa hoja yangu ni kwamba hata hizo wanazodai ni halisi, ukienda huko unapigwa pia.
 
Hili lipo kwa kweli. Watanzania wengi tumekuwa na mazoea hayo ya kupenda vya bei ndogo bila kuchanganua ubora na kiasi. Matokeo yake hata mwenye nazo bado ananunua vitu vya kiwango duni sababu ya mazoea. Lakini, ukisoma post yangu hapo juu, kuna maduka yanajifanya kuzima kiu ya wale wanaohitaji vya ukweli lakini bado ni walaghai.
Mkuu naomba nirekebishe kitu hapo kwenye bidhaa hasa za electronics zipo bidhaa ambazo kama sio mjuzi huwezi kuzitambha kama sio mtaalamu hasa! Kuna maduka yanauza bidhaa kwa bei sawa na jle ya bidhaa orihinal na kwa macho tuu unaweza usielewe!! Hapo ndo serekali iliyoajiri wataalam huko TBS na FCC wangesimamia hili jambo!
 
Sawa. Sasa hoja yangu ni kwamba hata hizo wanazodai ni halisi, ukienda huko unapigwa pia.
Kweli mkuu kuna maduka wanauza bidhaa feki ila kwa mwonekano hata ukizichunguza unakuta ni feki! Wataalam hasa wanazijua ila kwa mtu wa kawaidani ngumu!
 
Ndugu, mimi na baadhi ya wachangiaji wengi tu hapa wanakiri hili, lakini jikusanye weee na vihela vyako, kanunue hizo wanazosema za bei uone. Wengi ni walaghai tu. Labda uniambie hata nchi za mbele hakuna suruali yenye afadhali kwa shilingi 100,000, 150,000 hadi 200,000 hapo nitakubali. Haya maduka yetu yanauza nguo za bei hizi lakini bado zina ubora mdogo sana.
Kweli tatizo sio hela kuna bidhaa feki ila. Kwa mwonekano nioriginal na hapoukienda kisa inauzwa bei kubwa unaliwa tena!
 
Kabisa! Ndiyo maana mimi nilihitaji kujua kama kuna mtu anaweza kunishauri duka la kwenda. Ninaona ujanja umeniisha sasa.
 
Back
Top Bottom