Mtafiti77
JF-Expert Member
- Oct 31, 2011
- 1,877
- 2,314
Ndugu wana JF, suala la bidhaa feki na duni limekuwa ni changamoto kubwa. Nina mfano mzuri kupitia mavazi. Binafsi, nimekuwa nikiishi kwa kuvaa mitumba kwa muda mrefu kwakuwa nimekuwa na mtazamo hasi dhidi ya nguo "special" au tuseme za dukani. Lakini, siku za hivi karibuni mitumba imekuwa adimu mno hasa kwa baadhi ya mikoa, hali iliyonifanya kugeukia dukani. Baada ya kuvaavaa suruali zile za elfu 25 na 30, nikajikuta nguo zinapauka baada ya kufuliwa mara mbili au tatu.
Hali hii sikuridhika nayo, kwakuwa ninajua kusoma na kuandika, nikawa ninapitia tovuti za wazalishaji na wauzaji wakubwa wa mavazi duniani, mfano, Banana Republic, H&M, Zara n.k.Huku nikagundua kuwa mavazi ni ghali kwa kulinganisha na huku kwetu. Pia, niliamini kuwa bidhaa halisi ni ghali. Nikiwa na elimu hii, nikaaanza kuwinda maduka makubwa kabisa jijini Dar es Salaam. Nikisema makubwa ninadhani ninaeleweka, yale maduka unakowakuta kina fulani wenye kuchanganya Kiswahii na Kiingereza. Huwezi amini, nilinunua suruali 4 aina ya kadet kila moja kwa 150,000, lakini, nguo hizi hazikumaliza hata miezi sita, zilipauka balaa. Aidha, nilinunua kashati ka linen, cha mikono mirefu na kenyewe baada muda mchache kanafumuka mikononi. Na nguo hizi zimewekwa hadi lebo ya mtengenezaji, tena wauzaji ni mawakala.
Sasa ninajiuliza, nikimbilie wapi? Kumbe waweza kuwa na hela hapa Tz na bado usipate kitu cha ukweli? Siwezi kujigamba kwamba 150,000 ni hela kubwa kiviile maana huko mbele, kutegemea na ubora na jina,unaweza usipate nguo fulani kwa hela hiyo.
Mnaofahamu bidhaa za mavazi, ninaomba mnipe shule wapi hapa Tz ninaweza kupata nguo mpya zenye uhalisia. Maana sasa hata haya maduka makubwa ninayaogopa.Mitumba siku hizi mpaka uweke oda kwa muuzaji anaefuata mzigo Nairobi.
Siku njema