Bidhaa kutoka South Africa zinalipiwa ushuru?

Dingswayo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
4,019
Reaction score
2,925
Naomba kuuliza kwa anayefahamu kuwa nikiingiza bidhaa iliyotengenezwa South Africa nchini Tanzania nitalazimika kulipia ushuru? auliza hivyo nikizingatia kuwa South Africa ni nchi ndani ya SADCC ambapo Tanzania nayo imo. Natanguliza shukrani.
 
Mkuu nadhani hujanielewa. nimemaanisha hata bidhaa made in Zanzibar inalipiwa kodi sembuse made in SA! kifupi jibu ni inalipiwa kodi.
Zanzibar siyo nchi na haipo kwenye umoja SADC-Hujajibu swali!
 
Zanzibar siyo nchi na haipo kwenye umoja SADC-Hujajibu swali!

Kwa kuwa sio nchi bali ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kwa kuwa bidhaa made in Znz ni sawa na bidhaa made in Arusha, Dodoma, Mwanza n.k na kwa kuwa bidhaa made in Znz zinalipiwa ushuru mara ziingiapo Tanzania, basi bidhaa made in Polokwane, RSA zitalipiwa ushuru.
 
Last edited by a moderator:
Msichanganye madesa wakuu kodi (VAT)na ushuru (Exercise Duty) ni vitu viwili tofauti kwa uelewa wangu ni vitu toka East African Community tu ndo havilipiwi ushuru ila toka nje ya east Africa inalipiwa ushuru 25% exercise duty,Sina uhakika na SADC wanaojua waje kutujuza
 
Hebu mwagika hapa: Nimenunua gari kenya nikilileta Tanzania ina maana sitailipia excise duty?
 
My experience: nilikuwa na gari Nairobi, nimeendesha miezi 6, wakati narudi Dar, ilibidi niuze maana lilikuwa halijafikisha mwaka tokea nilimiliki Nairobi. Nilipouliza TRA customs niliambiwa kenya sio car manufactures , so inabidi nilipe tax zote kama nilivyolipa nairobi, wakati naliingiza from japan, then nikaclaim back from kenya. Nikaona kuliko kuidai govt, bora niuze nianze upya!
 
Hebu mwagika hapa: Nimenunua gari kenya nikilileta Tanzania ina maana sitailipia excise duty?

Kenya hawatengenezi Magari ni bidhaa zinazotengenezwa {Manufactured} ndani ya EAC tu sio zilizotengenezwa nje ya EAC.Kwa mfano ukinunua gari Corolla Carina Kenya inaangaliwa hili gari limetengenezwa wapi obvious ni Japani so utapigwa exercise duty ila ukiimport Omo,Blueband toka Kenya kwa vile vimetengenezewa Kenya hautalipa Exercise Duty.I hope umenisoma
 
Tanzania ni mwanachama wa SADC nchi hizo huwa na mikataba ya kibiashara kuhusiana na kuuuzia bidhaa ambazo zimetengenezwa toka nchi wanachama mhusika anataka kujua kama mikataba hiyo inahusiana na uingizaji wa bidhaa miongoni mwa nchi za SADC kama kuna unafuu wowote
Sina jibu kamili labda ucheck na watu wa TRA
 
Mkuu nimefuatilia hazilipiwi ushuru unalipa kodi nyingine tu kama VAT
 
Kuna kitu huwa sielewi,yani hii mikataba mfano SADC naona kama imeweka kuwanufaisha wenzetu tu?sisi tunawauzia nini wao?au ndo hatuna cha kuwauzia!mh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…