Bidhaa kutoka Zanzibar kutolipishwa kodi, Serikali kuunganisha mifumo ya kodi Bara na Zanzibar

Ukinunua vitu Zanzibar na kuja navyo Tanzania Bara vitu husika vilikuwa vinalipiwa kodi ikiwa ni mara ya pili baada ya kulipiwa kodi Zanzibar kabla.

Jambo hilo linaenda kuwa historia baada ya kamishna wa kodi wa mamlaka ya mapato Zanzibar(ZRA), Yussuf Juma Mwenda kusema wanamalizia hatua za mwisho kuunganisha mifumo ya kodi ya Tanzania Bara na Zanzibar ili mtu alipe kodi mara moja pekee.

"Hili jambo likiisha, malalamiko yatasuluhishwa. Ukiwa na risiti halali kutoka ZRA au TRA hautalipishwa kodi mara mbili". Alisema.

The Citizen
Hili naunga mkono
 
Ngoja tuone ila kama kodi za Zanzibar zitabaki vile vile basi Zanzibar ndio watakuwa wamecheza kama pele, mizigo mingi tabidi tushushie kwao, kukwepa gharama kubwa za huku kwetu bara, hivyo bandari yao itakuwa busy zaidi.
Wazanzibari huwajui vizuri. Wavivu sana
 
Kodi ikikatwa Zanzibar inaishia huko huko, haisaidi uchumi WA bara tofauti na Kodi iliyokatwa dar inaweza kutumika karagwe , hii ndio tofauti Kuu.
Wazanzibar wana haki zaidi na huu muungano fake, hatuwataki uvunjwe haraka
 
Hivi ukitoka na bidhaa Dar na kwenda nazo Mologoro au Mwanza au Mbeya au Ntwala au Tanga unalipishwa ? na kote huko kuna bandari aka border.

Zanzibar ilikuwa isiwepo hata check point zaidi ya kuonyesha kitambulisho halisi na ilivyo kila mtu anatakiwa akitembea awe na kitambulisho cha Utaifa
Tupeni ukweli au ndio Zanzibar ni Nchi kamili na mamlaka yake bado kutangazwa rasmi au ndio wanaishi kizagazaga tu ?
Zanzibar ni nchi kamili
 
Ukinunua vitu Zanzibar na kuja navyo Tanzania Bara vitu husika vilikuwa vinalipiwa kodi ikiwa ni mara ya pili baada ya kulipiwa kodi Zanzibar kabla.

Jambo hilo linaenda kuwa historia baada ya kamishna wa kodi wa mamlaka ya mapato Zanzibar(ZRA), Yussuf Juma Mwenda kusema wanamalizia hatua za mwisho kuunganisha mifumo ya kodi ya Tanzania Bara na Zanzibar ili mtu alipe kodi mara moja pekee.

"Hili jambo likiisha, malalamiko yatasuluhishwa. Ukiwa na risiti halali kutoka ZRA au TRA hautalipishwa kodi mara mbili". Alisema.

The Citizen
Na kuanzia hapo ndio bidhaa za Zenji zitakapopaa bei zake. Kwa sasa wenzetu bidhaa zao ni nafuu sn ukilinganisha na zile za bara hasa vifaa vya electronics kam Tv, Computers n.k. Wazee wa kazi wakishatia maguu, sidhan kama hali itabakia kama sasa
 
Kodi ikikatwa Zanzibar inaishia huko huko, haisaidi uchumi WA bara tofauti na Kodi iliyokatwa dar inaweza kutumika karagwe , hii ndio tofauti Kuu.
Na wakifanya hivyo, mnufaika atakuwa Znz coz wao wanaunafuu mkubwa wa kodi bandarini. Halafu bandari ya mapato yote ni yao hakuna DP World kule. Sasa mizigo mingi itashukia zenji. Huku para sasa patakuwa ni geti tu la watu kutolea mzigo wao. Chao chao, chetu chao
 
Ukinunua vitu Zanzibar na kuja navyo Tanzania Bara vitu husika vilikuwa vinalipiwa kodi ikiwa ni mara ya pili baada ya kulipiwa kodi Zanzibar kabla.

Jambo hilo linaenda kuwa historia baada ya kamishna wa kodi wa mamlaka ya mapato Zanzibar(ZRA), Yussuf Juma Mwenda kusema wanamalizia hatua za mwisho kuunganisha mifumo ya kodi ya Tanzania Bara na Zanzibar ili mtu alipe kodi mara moja pekee.

"Hili jambo likiisha, malalamiko yatasuluhishwa. Ukiwa na risiti halali kutoka ZRA au TRA hautalipishwa kodi mara mbili". Alisema.

The Citizen
Haya mambo tayari au ndiyo ukiritimba mwingi?
 
Back
Top Bottom