Bidhaa za China ni feki

Gor

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
2,791
Reaction score
850
Tanzania inaangamia kwa bidhaa hovyo kabisa kutoka uchina,pochi,viatu,mashuka zote hovyo kabisa sb sio ngozi ni plastics sijui kwanini watz wanaendelea kuwa na uhusiano huu na watu hovyo kabisa kama hawa.

Serikali lazima iwalinde walaji kwa kuzuia upumbavu huu wa bidhaa hovyo katika soko.

Unashangaa kwanini tunaagiza bidhaa za hovyo kiasi hiki, simu ndio usiseme upuuzi tu, Kheri ununue kitu ghali but imara cha kushangaza wanaleta wenyewe sasa.

Tumekwisha.
 
Omba mungu sana ccm waondoke bila hivyo tutauziwa mpaka tupinde migongo
 

Mkuu sio kila bidhaa kutoka China ni feki....
 
Bidhaa za China siyo feki tena china kutengeneza feki ni kosa la jinai ila waleta bidhaa china ndio feki....
 
Hata maoni yako ni fake. Nikujuze tu china hawana bidhaa fake kama usemavyo wewe. Zipo genuine products. Na usiwalaumu wanaoingiza bali walaumu watumiaji i.e customers. Mfanyabiashara akinunua bidhaa genuine akileta hapa TZ ,wateja HAWANUNUI kwa vile bei inakuwa juu. Ila akileta copy ya same product kwa bei ya chini mnanunua na kujinasibu kuwa na nyinyi mna bidhaa za brand kama apple, samsung nk. Sasa wateja wakiacha kununua fake products ,je unadhani kuna mfanyabiashara atakae ingiza fake? Mfanyabiashara yeye anafanya biashara ili auze na sio vinginevyo
 

Yes, china imejaa bidhaa feki tena kila mahali.

Lakini bidhaa nzuri zipo nyingi tuu, tatizo ni wafanyabiashara wa kibongo hawajali consumers wao.
 
bidhaa za china siyo feki tena china kutengeneza feki ni kosa la jinai ila waleta bidhaa china ndio feki....
hakuna bidhaa zao feki na hata kazi zao feki,ona hata bara bara au majengo yao feki tu....
 
Tatizo liko kwa wateja na wauzaji. Mteja anapenda vya bei ndogo Bila kuangalia Muda gani kifaa kinakaa.
Muuzaji nae huangalia faida zaidi.
Uchumi wa Tanzania ni mdogo sana kwa Watu kununu brands,
Watu wanachofanya ni kununua chochote kile ili mradi bei owe chini.
 
Bidhaa za china ni fake kama ccm WANa yopata ushindi kwenye chguzi fAke!!
 
Mkuu si kweli bidhaa za China ni fake na wanaoleta bidhaa huko si wachina ila ni wafanyabishara wa kibongo kwa kutaka faida kubwa. Ukienda china unahitaji kitu anakutaji bei unasema nipunguzie na kama mnavyojua wabongo kwa kulia lia. Sasa mchana anakuambia njoo kesho anakutengenezea mfano wa ile uliyotaka kwa bei uliyonayo. Hapo unamlaumu mchina kivipi na kwa nini usimlaumu huyu anayeleta bidhaa?
 
hakuna bidhaa zao feki na hata kazi zao feki,ona hata bara bara au majengo yao feki tu....
Waleta bidhaa feki kwa sababu wananunua the most cheapest ambazo hutumika kama toi ulaya......kazi zao siyo feki kwa sababu wasimamizi wanataka ten percent ndipo kazi inaharibika........Ndugu china ndiyo inayouza bidhaa bora zaidi katika masoko ya Ulaya na Marekani kiasi cha kulalamikiwa kwa kuuwa viwanda vya huko... una taarifa kwamba viwanda vingi vya marekani kama vya simu na laptop zinatengenezea bidhaa zao china kwa sababu ya cheap labour with required quality..... Kwa mifano hii amini kauli yangu china hawana feki ila sisi ndio feki.
 

Nakubaliana na wewe, lakini China vipo fake, kwa maana havina standard, vitu vinavyo letwa bara la ulaya vimewekwa standard zao, na ikisemekana au ikigundulika kuwa ni fake hupigwa fain kubwa sana, kiasi ambacho bora kuuza hio standard, kuna standard za aina 3
Ya kwanza ndio inayo letwa ulaya na America, kwa vile nchi hizi wanauwezo wafanyabiashara pamoja na wananchi,
Standard ya pili inakwenda nchi za arabuni na Asian.
Ya tatu hii inakwenda au inakuja Africa kwa vile sisi ni poor hivyo ndio uwezo wetu. Lakini hapo hapo, sasa hivi wananchi wameamka wanataka quality hata kama ni expensive tatizo lipo kwa wafanya biashara wanataka ku make money haraka sana.
Tatizo Jengine serikali yetu ni rushwa, ndio inayo pelekea kushindwa kuweka standard, hao TBS nakuambia hawafai kabisa, mimi nilisha fanya kazi clearing and forwarding agency, najua vizuri hivi vitengo.
 
wengine wengike hawafikirii kuwa kununua kitu cha bei poa mara nne labda kwa miezi kadhaa ni bora kununua cha gari kitakachokaa miezi mingi zaidi na kujikuta hata bei inakuwa chini ya mtu kukinunua mara nyingi kisichodumu.
 
Ndo maana siku hizi kitu kikiandikwa made in china najiuliza mara mbili zaidi
 
Mpaka "MB" za "Internet" ni feki. Ukiziweka tu kabla hata hujaponyeza tuma zishakwisha, inarudi ripoti kifurishi kimekwisha.
 
sio kweli mi natumia tecno h5 made in china ni original na nzuri sana kwa iyo wabongo tuache kukariri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…