Bidhaa za China ni feki

sio kweli mi natumia tecno h5 made in china ni original na nzuri sana kwa iyo wabongo tuache kukariri

feki, feki tu. Je ushajaribu nokia au samsung original? km wewe simu zako ni OKING ukaamia tecno lazma uone bora, lkn km utatoka iphone to tecno tofauti ipo mzee
 
Maisha ya kukariri mara nyingi huwa ni magumu kuliko ya kuelewa.
 
sio kweli mi natumia tecno h5 made in china ni original na nzuri sana kwa iyo wabongo tuache kukariri

Mkuu nikupe taarifa tuu china hakuna simu inaitwa tecno nilishangaa sana kuulizia wakanambia techno hazikidhi vigezo vya kutumiwa china so that simu ni special Kwa Africa
 

Nakushauri tembelea China utakuja na mtizamo tofauti kabisa ila kwa ufupi tu ni kwamba hizo bidhaa bandia zilizojaa kwenye maduka na maghala yetu hapa nchini kule China hazipo kwenye mzunguko wao wa kawaida wa bidhaa zao bali hutengenezwa vichochoroni kwa matakwa ya Watanzania
 

Ukweli mtupu.
 
Ivi kwann wanatengenezea dada zetu dawa za kuongeza makaĺio na mahipsi wakati wenyewe wako flati scrini behaind ze sini?..🙉
 
Mkuu nikupe taarifa tuu china hakuna simu inaitwa tecno nilishangaa sana kuulizia wakanambia techno hazikidhi vigezo vya kutumiwa china so that simu ni special Kwa Africa

Duh Kaka hapo umedanganya ingawa sijafika China ila techno ni kiwanda kikubwa tu, na ndio maana hata ile Phantom z walikuwa wanaadvertise kwenye channel kubwa tu super sport so kuniambia huko hakuna techno sababu ni yavichochoroni unamdanganya nani sijui na kwafaidi ya nani sielewi ila nachojua kuwa TECNO inapoanzA ilikuwa sababu ya Africa kutupa affordable phone ila baada ya kupata Friday sasa wameingia mpaka ulaya ingawa soko lao huko bado halijawa safi
 

Waio hivyo si Wachina walio hovyo ni hao wanaoenda kununuwa bidhaa hizo Uchina na hivyo ni kwenu hapa hakuna "standards" za kiitaifa na kama zipo basi ni hovyo waliopewa dhamana ya kusimamia hizo "standards".

China kuna vitu vina standard (ubora) wa hali ya juu sana, na wanauza duniani.

Nnakumbuka huko nje, madukani wauza maduka wakati wakuudia bidhaa wanakusifia "This is Chinese made", kwa sababu, Wachina wanauza standard ya hali ya juu huko dunia ya kwanza kuliko mahitaji ili wateke soko la huko, lakini nayo kwa bei yake.

Walaumu Watanzania wenzako wanaokuletea na wale wanaokubali bidhaa zenye ubora hafifu ziingie nchini.

Cheap can be very expensive.
 
Wiki mbili zilizopita nilikuwa Shenzen Industrial City kule Uchina. Na nilikuwa na baadhi ya wabongo wanaochukua bidhaa kuleta Tz. Kwa muktadha wa uzi huu niliyoyaona huko ni haya.

China kuna bidhaa za viwango tofauti kulingana na masokoko tofauti. Mfano kuna bidhaa/simu "cheap" kwa ajili ya wenye kipato kidogo lakin kiwango unakuta imekubalika duniani. Ukitaka kuamini, chukua hiyo simu tunayoita feki, toa betri kwa ndani chunguza kama ina nembo "CE 168" hata kama namba ni tofauti na 168 basi tambua hiyo simu imekubalika ktk viwango vya kimataifa japo umeinunua elfu 20 kariakoo.
CE ni European board of approvals na China wanayo Laboratory Beijing pamoja na Shenzen, kama bidhaa haina nembo ya CE ina maana haiuzwi Ulaya na America. So kwa kifupi ni kwamba, sisi tunaamini bidhaa za America na Ulaya ndo bora, lakini bado America na Ulaya wananunua China.

Sikatai kuna bidhaa baadhi sio zote hutengenezwa uchochoroni, hizo ndo feki na si kila bidhaa iliyotoka China ni Feki. Nilinunua Microscope toka kampuni ya Omax marekani, nilipoichunguza nikakuta ni "made in china" na bei ilikua nzuri na inapiga kazi bila tatizo leo mwaka wa tatu. Nilipouliza kwa nn kampuni ipo marekani halafu bidhaa iandikwe made in china? wakaniambia wamewekeza kule kwa sababu ya cheap labour, china watu ni wengi balaa na malipo ya wfanya kazi ni cheap ndio maana makampuni mengi hata Blackberry ya Ontario Canada utakuta wanakiwanda Shenzen lkn bado ni blackberry original.

Kuna watu wengi duniani wanashukuru mapinduzi ya china na sio tanzania pekee. Hata hivyo tunatofauti ya kipato, kama wewe unamiliki Samsung galaxy note ni kwa sababu uwezo wako unaruhusu (hata galaxy note zipo ambazo ni made in china na ni original kabsaaaaaa). Anayemiliki tecno 611 naye uwezo wake upo pale. Ebu jiulize pasingekuwa na mapinduzi ya china ni wangapi leo tz wangemiliki simu? jibu unalo.

Kwa ujumla china wanabidhaa kwa viwango vyote, na wafanya biashara wetu wanachangua kulingana na viwango vya wateja wao ambao ni mimi na wewe. hatuna sababu ya kulaumu serikali ila labda kila mtu ajilaumu kwa kiwango cha uchumi wake. serikali ikizuia kabisa cheap products tutayarudia maisha ya ujamaa na kujitegemea (kama huyajui mwulize mzazi wako akusimulie).

kuna tovuti imezungumzia "kwa nini made in china kila sehemu" ukiweza soma hapa Jifunze namna ya kufanya biashara au kununua kwa njia ya intaneti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…