Wiki mbili zilizopita nilikuwa Shenzen Industrial City kule Uchina. Na nilikuwa na baadhi ya wabongo wanaochukua bidhaa kuleta Tz. Kwa muktadha wa uzi huu niliyoyaona huko ni haya.
China kuna bidhaa za viwango tofauti kulingana na masokoko tofauti. Mfano kuna bidhaa/simu "cheap" kwa ajili ya wenye kipato kidogo lakin kiwango unakuta imekubalika duniani. Ukitaka kuamini, chukua hiyo simu tunayoita feki, toa betri kwa ndani chunguza kama ina nembo "CE 168" hata kama namba ni tofauti na 168 basi tambua hiyo simu imekubalika ktk viwango vya kimataifa japo umeinunua elfu 20 kariakoo.
CE ni European board of approvals na China wanayo Laboratory Beijing pamoja na Shenzen, kama bidhaa haina nembo ya CE ina maana haiuzwi Ulaya na America. So kwa kifupi ni kwamba, sisi tunaamini bidhaa za America na Ulaya ndo bora, lakini bado America na Ulaya wananunua China.
Sikatai kuna bidhaa baadhi sio zote hutengenezwa uchochoroni, hizo ndo feki na si kila bidhaa iliyotoka China ni Feki. Nilinunua Microscope toka kampuni ya Omax marekani, nilipoichunguza nikakuta ni "made in china" na bei ilikua nzuri na inapiga kazi bila tatizo leo mwaka wa tatu. Nilipouliza kwa nn kampuni ipo marekani halafu bidhaa iandikwe made in china? wakaniambia wamewekeza kule kwa sababu ya cheap labour, china watu ni wengi balaa na malipo ya wfanya kazi ni cheap ndio maana makampuni mengi hata Blackberry ya Ontario Canada utakuta wanakiwanda Shenzen lkn bado ni blackberry original.
Kuna watu wengi duniani wanashukuru mapinduzi ya china na sio tanzania pekee. Hata hivyo tunatofauti ya kipato, kama wewe unamiliki Samsung galaxy note ni kwa sababu uwezo wako unaruhusu (hata galaxy note zipo ambazo ni made in china na ni original kabsaaaaaa). Anayemiliki tecno 611 naye uwezo wake upo pale. Ebu jiulize pasingekuwa na mapinduzi ya china ni wangapi leo tz wangemiliki simu? jibu unalo.
Kwa ujumla china wanabidhaa kwa viwango vyote, na wafanya biashara wetu wanachangua kulingana na viwango vya wateja wao ambao ni mimi na wewe. hatuna sababu ya kulaumu serikali ila labda kila mtu ajilaumu kwa kiwango cha uchumi wake. serikali ikizuia kabisa cheap products tutayarudia maisha ya ujamaa na kujitegemea (kama huyajui mwulize mzazi wako akusimulie).
kuna tovuti imezungumzia "kwa nini made in china kila sehemu" ukiweza soma hapa
Jifunze namna ya kufanya biashara au kununua kwa njia ya intaneti