Bidhaa za China sio feki

HAKUNA DALILI YA KUKARIBISHWA WATU KUPIGWA HAPA ??
 
Hata hilo mimi napingana nalo fikiria kama simu ya tecno inayouzwa laki moja unaweza kuitumia hadi miaka miwili bila kuharibika hii kazi ungempa mbongo sijui ingekuwaje yani simu ya laki idumu kwa miaka miwili ingekuwa kazi sana wachina wanajitahidi sana
 
Tunafeli sana kwa kila kitu
 
Mleta mada naomba ujue kuna tofauti ya bidhaa duni ( low quality / substandard ) na bidhaa iliyoghushiwa ( counterfeit / fake ) ukiweza kutofautisha hizo dhana kamwe hutawatetea wachina! Naomba nikupe facts mbili kwa kuanzia :

1. Zaidi ya asilimia 90 ya bidhaa zilizoghushiwa ( counterfeit / fake ) duniani zinatokea China , hapa namaanisha unaenda dukani kununua simu ya Samsung, iPhone au Television yenye Jina ( brand ) inayofahamika kama Sony, Samsung au Hitachi unaishia kuuziwa bidhaa iliyoghushiwa kwa bei ya bidhaa halisi

2. Kiasi kikubwa cha bidhaa hafifu ( substandard / low quality ) kinatokea China, hapa namaanisha unaenda kununua bidhaa yenye branding ya Chinese manufacturer iwe ni simu, Radio, Seti ya Television au hata vipuri vya gari , hapa mnunuzi anapata bidhaa isiyo na thamani ya pesa zake ( value for money )

3. Kuna mfumuko mkubwa wa bidhaa duni na zilizoghushiwa kwenye soko la dunia baada ya China kupata uwezo wa industrial mass production , hii sio coincidence!
 
Wabongo washamba sana

Wachina wanatengeneza simu zao let say huawei,unaanzaje kuziita fake wakati ni product yao from the scratch??

Fake product ni imitation of the original product..
Pia hizo propaganda hua zinaenezwa na marekani ambayo ndio mshindani wake mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi duniani..as you know marekani ni selfish they want to control each and everything in the world..

Na zaidi mnunuzi anapoenda kununua mzigo anachagua anunue bidhaa halisi ambayo bei yake ni kubwa au anunue bidhaa bandia, ambayo bei yake ni ndogo, na matokeo serikali inakoseshwa mapato kwa sababu waingizaji wa bidhaa bandia hawalipi kodi, kwa vile zinaingizwa nchini kwa kutumia njia zisizo rasmi.

Cha msingi hapa ni serikali kuongeza udhibiti katika njia zisizo rasmi na kushirikiana na kampuni zinazozalisha bidhaa, kuwaelimisha raia ili waweze kutambua bidhaa halisi na bidhaa bandia.
 
Kinaeza kua Fake kikawa imara..ila mara nyingi tunapata bidhaa kutokana na thamani ya pesa yetu we ukitaka cm ya Million 1 kwa laki 6 utapata tuu wachina ni watu wazuri wanatujari tusio na uwezo.
 
Tunaodili na ELECTRONICS Tunaweza kukubaliana na mleta mada.

Vifaa vya Kampuni ya "TRONIC" ni Orijino Sana , Ila navyo vinatengenezwa china
 
Habari za leo wadau. Naomba Connection ndugu zangu. Hizi Slippers zinapatikana Chimbo gani na bei ya jumla jumla ni Shilingi ngapi.
Asanteni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…