Bidhaa zinazoendana katika soko

Bidhaa zinazoendana katika soko

LOVINTAH GYM

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Posts
459
Reaction score
653
MONOPOLISTIC COMPETITION

Hili ni aina ya soko ambalo ni muuunganiko wa monopoly na perfect competition.

Lina uhalisia zaidi kuzidi perfect competition.

Sifa za monopolistic competition:

1.Bidhaa zinafanana sema zina unatofauti katika ladha, ubora, package nk

Mfano: Pepsi na coca, zote ni soda ila ladha zake zinatofautiana.

2. Kila muuzaji anajulikana kwa brand yake japo bidhaa anayouza wauzaji wapo wengi.

Mfano: Wauzaji wa maji ya kunywa Kuna Uhai, Hill, Masafi, Dasani,Pure water nk

3.Kipindi cha mwanzo kwasababu wauzaji wanakuwa wachache basi faida zao zinakua ni kubwa (supernormal profit)

Ila kwa kipindi cha mda mrefu wauzaji wanazidi kuongezeka na kusababisha bei kushuka kwahiyo wauzaji wanaanza kupata normal profit.

4.Ukosefu wa taarifa kamili kuhusu bidhaa zinazouzwa.

Mfano: Colgate na whitedent zote zina ubora sana lakini kutokana na branding bei ya colgate ipo juu kuzidi whitedent. Kwaio kwa ukosefu wa taarifa zote muhimu kuhusu hizo bidhaa watu wataamini colgate ni bora zaidi kwasababu bei yake ipo juu.

5. Muuzaji anaweza kuwa na ushawishi kwenye upangaji wa bei.

Mfano:

Wauza sabuni za kuogea.

Kutokana na branding wa bidhaa yako basi unaweza kuuza bei ya juu kuzidi zile bidhaa ambazo zote zinaendana na bidhaa yako.

Karibuni wachangia mada.

#perfectmonopolistic #swahili #economics #uchumi #water #branding #brand #differentialadvantage

monopolistic-competition.png
 
Back
Top Bottom