Bifu kubwa kati ya Diamond na mbunifu mitindo wa Kimataifa toka Marekani

Diamond anakua sana kimuziki na katika ukuaji huu wa kimataifa anatakiwa awe na mwanasheria wake. Anaye? Ni muhimu sana kwa hadhi ya Diamond kuwa na mwanasheria (aliyemwajiri) kumshauri mambo mbalimbali kuhusu haki na wajibu wa diamond kimataifa.Tabia yetu wabongo kupenda kuiga vya nje yaweza kuzua mgogoro mkubwa wa kisheria kama ilivyogusiwa hapo juu. Ni kazi ya mwanasheria kumwelimisha na kumtahadharisha boss wake juu ya kuigaiga ovyo vitu vya watu. Kiasi kikubwa namshangaa Diamond kuvaa kimarekani kama hapo juu kwenye picha.Tanzania tuna wabunifu wengi wa vitambaa maridadi vya batik. Ukiingia kariakoo, unapata design nzuri sana ya batik ambayo kwa uhakika ukimpelekea Sheria Ngowi atakutolea mshono hatari wa shati hata koti. Unadesign ki alama chako unakishonea kwenye shati kinakuwa ndo trademark yako.Diamond nini bana kuhangaika na majeans yaliyochanika na shati kama teniti?Mlima wa mabatik kariakoo unamwachia nani? Ndo maana mie namsifiaga sana Mrisho Mpoto kukataa kuiga uvaaji wa kimarekani. Ila tu hajapata designer mzuri!
Hey guys, lets be tanzanians and let the world know it!
 

Umesoma kila kilichoandikwa?

Diamond umeona ana kosa gani? Umesoma uzi wote kuona mlalamikaji aliishia wapi pia? Uliona aliyeshona au kuiga mitindo alienda kunyakua logo yake na kuiweka? nani asiyevaa vya nje ya nchi? Mitumba yetu inatoka TZ? Kila mtu na uamuzi wake D ameuza mitumba mitaani anajua whatsup mwacheni aishi maisha yake.

Mwanasheria ukitaka kujua au kusema hana ulimtafuta ili akupe jibu na kukutajia ni nani?
 
  • RED- Umeongea kitu cha msingi... nakuunga mkono kwa 100%!

  • BLUE - Haiakisi (doesn't reflect) na kilichotokea! Malalamiko ya jamaa sio kwa sababu Diamond amevaa "Kimarekani" kama unavyodai bali Diamond kumtaja Qboy Msafi kama Designer wa ile model! I hope huko kumtaja mwingine (Qboy) kama ndie designer sio ulichomaanisha kwamba ni kuiga!!! Correct me if I am wrong!

  • BOLD BLACK- Nchi hii kumtuhumu mtu kwamba anavaa Kimarekani ni kumuonea tu kwenye taifa ambalo halina any dressing code!

  • BROWN- Najaribu kuvuta hisia wakati Diamond au mwanamuziki yeyote yule wa aina yake atakapokuwa ndani ya batiki... I think it's brilliant idea and advice especially tunapokuja na suala la BUY TANZANIA and showing appreciation to what we have though am bit disappointed by your avatar!

  • LIGHT PINK- Wakati mwingine nahisi tunalazimika kukubali kwamba kila kitu kina identity yake! Mrisho Mpoto anafanya muziki wa asili na hivyo akifanya local dressing code anakuwa amewakilisha sanaa yake moja kwa moja! Hata Tatu Nane, at least jukwaani walikuwa wanavaa kiasili! Saida Karol, angalau jukwaani nae alikuwa anavaa kiasili! Lakini umwambie Jide leo hii avae kiasili jukwaani ni kutaka kumwondolea confidence yake! Ushauri uliotoa hapo kwenye BROWN unatakiwa kufanywa na Designers wetu na sio mtu kama Diamond... the excuse is there, he's not a designer na ndio maana hata kuvaa tu analazimika kuwa na Stylist coz' yeye kama yeye isn't an expert kwenye hilo eneo! Don't say mbona Mrisho Mpoto amefanya wakati na yeye sio designer... kwa staili ya muziki wa Mpoto hata akivaa magunia ya hovyo hovyo yaliyounganishwa kwa kwamba za katani kisha akapanda jukwaani, ataeleweka tu lakini kitu kama hicho akifanya mtu kama Diamond ataambiwa anatafuta kick!!! Hawa designers wetu ndio wanatakiwa ku-translate taste za wasanii wetu/vijana wa kileo kisha watumie materials zetu wenyewe kama hizo batiki na kutengeneza brands ambazo, kwa upande mmoja hazitafuta identity ya muziki wa kileo unaoambatana na aina fulani ya mavazi na upande mwingine zikiwa zimebeba African identity! Hili la identity halikwepeki and I think, I repeat, I think, hatahao akina Marehemu Muhidini Ngurumo, Mbaraka Mwishehe, Marijani Rajabu, sidhani kama walipata kuvaa kama anavyovaa Mrisho Mpoto au Tatunane! I know your concern is to make our locals fabrics into a modern form lakini hiyo ni kazi ya designers unless kama wasanii wenyewe wanakuwa na hiyo karama!
 
Good mate! Sensible post from a sensible jf member. Thanks for a word on my avatar.Will think it over tonight bro!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…