Yaani jamaa walitaka wamiliki music industry yote wao.. wamcontrol kila msanii.. matamasha makubwa waandae wao tu, dili zote wapewe wao kwanza.. tuzo za kili wameua wao, bahati kwa sasa mambo yamebadilika, radio sio tena platform yenye nguvu kama zamani enzi hizo unakaa eti unasubiria ngoma fulani itambulishwe muda fulani..
Social media imebadili kila kitu kwa sasa.. jamaa hawana nguvu tena kama zamani na haiwezi jirudia..
Walijitahidi kumtengeneza kiba na kutengeneza bifu na mondi ili wapige hela.. ila mondi alipoamua kusonga kivyake wakamkatia waya matokeo yake jamaa anazidi pepea tu na kiba mwenyewe kwa sasa hana time nao kabisa.. inajibidi wajipange upya tu, mambo ya kuwaimbisha wasanii bure kwenye shows hayapo tena.