Bifu la P-Funk na Wasafi Litafikia Kikomo?

Linguistic

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2021
Posts
3,669
Reaction score
8,268
P Funk Majani Ni Bulldozer.

Amechonga Barabara kubwa katika Sanaa ya mziki ambayo Hadi Kufika leo Hapa Inatakiwa Tumpe Maua Yake.

Kitendo Cha Sallam Kumjibu vibaya ni Kumkosea heshima.
................

Baada ya mahojiano aliyoyafanya Producer mkongwe hapa nchini Pmajani na Bongofive ambapo alieleza namna WCB inavyowakandamiza wasanii wake pale wanapotaka kutoka katika lebo hiyo.

Msanii Babalevo alipost kupitia Instagram yake na kutoa maoni na baada ya maneno hayo kuyaona Majani alikuja kwenye comment na kudadavua namna wasanii na maproducer akiwatolea mfano lizerclassic na s2kizzy wanavyonyonywa stahiki zao pale wanapofanya kazi na WCB lakini pia akienda mbali zaidi akiwatolea mfano Rayvanny na Harmonize.

Baada ya comment hiyo alikuja meneja wa Diamondplatnumz sallam_sk na kumtolea povu Majani kwa kueleza pia Majani alivyowanyonya wasanii na kudai kuwa anaishia kuwapiga hao wasanii.
 
Tukianzisha nyuzi tuzingatie kuwa si kila mtu anamjua muhusika wa uzi wako.
Mleta uzi umeandika kama vile wote tunafuatilia kina P Funk kiasi cha kujua kama ana ugomvi na Wasafi.

Kwa faida ya wasiojua kwanza ungeandika huo ugomvi, alichombiwa na huyo Sallam halafu unafunga na swali lako. Hapo hata kina sisi tusiojua tunapata kuelewa pia kinachojiri.
 
P-Funk anamwambia Salam "WCB inanyonya wasanii Rayvany kasepa, Harmonaiz nae kasepa.",

Salam akamjibu Majani,,,"hao waliotoka WCB unawatetea kwasababu wanakulelea binti yako na mke wako wa zamani[emoji23][emoji23]
Salam kapiga kwenye mshono[emoji125][emoji125][emoji125]
 
Ambacho sijapenda ni Salam kuingiza personal attack Kwa Majan
.
hao waliotoka wcb unawatetea kwasababu wanakulelea binti yako na mke wako wa zamani
.
Sio kauli NZuri yeye angejibu Hoja ya Majani with vivid evidence na Sio personal attacking Kwa mleta Hoja

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Upo sahihi kabisa mkuu.
 
Anayo yaongea Majani yana evidence?

Kaongea vitu ila vingine vina mrudia yeye?

Sababu hata hao akina Prof Jay na Nature hawana haki na nyimbo zao, kapewa dollar 50000 baada ya nyimbo ya Nikisaidieje kutumika na movie moja US, Prof alimpa ngapi?Mpaka kufikia level ya Prof kusambaza bakuli kwa ajili ya matibabu.

Vip Nature mmoja ya wasanii walioikamata bongo, ila cha ajabu kwa wasanii waliolipwa mirabaha hayupo, ila tulimwona yeye akienda BASATA kuvuta mzigo (japo najua sio mkubwa).

Chanzo cha beef lao ni baada ya kuomba apewe support ya msanii wake Raptcha, ila WCB wakamchomolea kwani pale kwao kila kitu biashara hamna cha bure.
 
Atleast wew ume ongea kinacho eleweka watu hawajui hivi vitu hua vina anzia mbali ni kweli kipindi Rapcha ametoa ile nyimbo yake jamaa alikua ana enda mpaka kweny page ya platnumz kuomba msanii wake apostiwe kirahisi rahis tu
 
Sina Shida na hayo Ila usipomheshimu mtu Kwa umri wake basi mheshimu hata Kwa kukutangulia Kwake kwenye industry

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Uzuri akili za majani na salaah Ni Kama pipa na mfuniko wake.Zina-match.
 
Lakini hakuna mtu mzinguaji kama Salam, niliwahi kusimamia contract yake na Mzee Mmoja Mwarabu Yuko Moro Mpaka Nilijuta, jamaa hata kama unamdai buku, hakupi ontime
.
Mpaka yule Mzee akaamka asubuhi akaenda kuweka Kufuli mlangoni ambako Kuna Radio na Tv Yao ya Dizzim FM.
.
Wote Wako kwenye Hyo industry ni Wahuni wahuni tu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Sina Shida na hayo Ila usipomheshimu mtu Kwa umri wake basi mheshimu hata Kwa kukutangulia Kwake kwenye industry

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Hivi unajua heshima ni bidirectional?

Jinsi unavyo behave na ndivyo watu watakavyo watakuchukulia.

Huwezi kuizungumzia biashara ya mtu vibaya kisa tuu kukataa kumpa promo msanii wako halafu akuachie.Wasafi ni brand ya kibiashara ukiizungimzia vibaya utajibiwa.

Mfano nyayua mdomo wako sasa hivi halafu uongee vitu visivyo na evidence kwa brand za Tigo,Vodafone nk halafu uone watakufanya nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…