Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Ukilitaja jina Tabora Boys, kwa mtu aliyewahi kusoma Tanzania ya zamani, huwezi kuwa umetaja shule kama shule nyingine, umetaja historia, umetaja nidhamu, umetaja viongozi, umetaja akili za darasani, michezo, gwaride na zile hadithi ambazo kila kizazi cha wanafunzi huwa nacho, huku baadhi zikisimuliwa kwa sauti kubwa, nyingine kwa tabasamu la mtu anayekumbuka ujana wake.
Shule hii ilianzishwa mwaka 1922 ikiwa inajulikana kama Tabora Central School.
Wakati huo, lengo kubwa lilikuwa kutoa elimu kwa watoto wa machifu na familia mashuhuri, ili kuwaandaa kwa nafasi za uongozi katika mfumo wa utawala wa kikoloni.
Baadaye milango ilipanuliwa na shule ikaanza kuchagua wanafunzi wenye vipaji vya masomo kutoka maeneo mbalimbali ya Tanganyika.
Kwa miaka mingi, Tabora Boys ikajijengea sifa ambayo ilifanya iitwe kwa jina lililokuwa na uzito mkubwa: 'Eton of Tanganyika' ikifananishwa na shule maarufu ya wavulana nchini Uingereza, Eton College.
Lakini historia ya Tabora Boys haiwezi kusimuliwa bila kutaja shule pinzani ya Milambo.
Kwa vizazi mbalimbali vya vijana wa Tabora, ushindani kati ya shule hizi mbili ulikuwa mkubwa, hasa kwenye michezo. Kumbukumbu za kimtandao zinaonyesha jinsi mechi zao zilivyokuwa zikichukuliwa kwa uzito mkubwa. Na hapo ndipo mpira ulipoweza kugeuka kuwa vita ya heshima kwa kila upande kutotaka kuwa mnyonge wa matokeo.
Ushindani huo ulikuwa na nyakati za kuvuka mipaka ya michezo, huku kukiwa na simulizi za uvamizi wa shule na mapambano ya wanafunzi.
Baadhi ya kumbukumbu za wahitimu zinaeleza hata matukio yaliyowahi kuhitaji kuingiliwa kati na vyombo vya usalama.