Jaguar
JF-Expert Member
- Mar 6, 2011
- 3,437
- 1,027
Uwoya amchana live mpenzi wa Flora Mvungi i.e H-baba kwamba hafai katika mapenzi kwa sababu hana stamina katika uwanja wa 6 kwa 6. Flora Mvungi naye akaja juu na kudai kwamba maneno ya Uwoya ni maneno ya mkosaji na akadai zaidi kwamba H-baba hana tatizo katika mapenzi na yuko fiti ile mbaya.Wakati malumbano yakiendelea,dada mmoja akapiga simu clouds fm,akakataa kutaja jina lake lakini naye akazidi kuchagiza kwamba H-baba si lolote si chochote katika ulingo wa ma-lovey dovey,ana mbwembwe za kukata viuno jukwaani tu.Haya ndio mapenzi ya ma-star wa ki-bongo.