Bifu na timu zinawajenga wasanii

Bifu na timu zinawajenga wasanii

mataka

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2011
Posts
286
Reaction score
61
Nikirejea historia za haya mabifu mi naona kama zinawasaidia. Hebu tuangalie kidogo: Nasma kidogo na Khadija Kopa jinsi walivyojaza kumbi mashabiki, Banza Stone akiwa TOT na Ally Choki akiwa Twanga unakumbuka walivyonyanyasa muziki wa dansi?

Vipi kuhusu East Coast Team na TMK walivyouza kwa timu zao. Haya tujikumbushe Sikinde chini ya Dede na Msondo ya Moshi na Gurumo unakumbuka walivyobamba? Na hata ukija kwenye timu za mpira Yanga na Simba wanajaza uwanja sababu ni huo upinzani wao.

Kiba na Mondi wanaomba dua usiku na mchana huo upinzani wao uendelee ili njia ya chooni isiote nyasi. Mimi hao nimewakumbuka ongezea na wewe. Kwa kweli timu na bifu zinalipa kwa wahusika ila kwa wapembeni ni maumivu tu!
 
Siku zote Competition kutoka kwny industry zinazofanana hata Music industry zinajenga ubunifu na uboreshaji.

Ila kwa hizi zinazoitwa teams hasa za bongo ni ujinga mtupu kwani wamebase kwenye matusi na kuponda kazi za watu badala ya kutoa changamoto za kumsaidia mhusika.
 
Siku zote Competition kutoka kwny industry zinazofanana hata Music industry zinajenga ubunifu na uboreshaji.

Ila kwa hizi zinazoitwa teams hasa za bongo ni ujinga mtupu kwani wamebase kwenye matusi na kuponda kazi za watu badala ya kutoa changamoto za kumsaidia mhusika.
ndugu kumbuka wao wanachoangalia ni jinsi gani wao watanufaikaila tatizo sisi mashabiki ndo tunahamishia kuwa za kweli
 
Ubaya wake moja akishuka au kupotea ndo mwisho wa mwingine mfano Ray. " The Greatest" Vs Kanumba "The Greater"
 
Si kwa Tanzania beef zetu tz ni kuwachukia wale waliofanikiwa, na wengine wanathubutu kutengeneza nao beef ili warudi kwenye gemu kwa kumchafua mwenzake ambacho si kitu kizuri. Mi napendaga zile beef za mwenzetu za kutengeneza mkwanja kama Kanye West na 50, beef yao ya kubust mauzo ya album zao ndio beef nzuri, sio zile beef zetu za kuponda hata kama mtu anafanya vizuri sana au kumshusha mmoja mwengine apande au kisa eti jamaa anaringa, ana nyodo, anajisikia ila ukija kuchunguza ni wivu tu. Beef zetu hasa za miaka hii za hawa watu wawili zinaua mziki kwani wanaangaliwa wao, wengine hawatazamwi, japokuwa mmoja anamtegemea sana mwenzake na kila siku anaomba mungu amuweka hai ili aendelea kushine kupitia yy.
 
Back
Top Bottom