Watu wanachukulia poa hili Swala. Tatizo lilianzia wakati Zahera namnanga Yondani, Kwa namna ambavyo Zahera alivyo elezea swala lile ni kana kwamba yeye Kocha alikua tayari wamekwisha yamaliza na Ajib kuhusu kumpokonya Unahodha Yondani, ni kana kwamba ajib alichangia kumshawishi kocha au kumpa nguvu ya kumpokonya kitambaa yondani. Angalia hata wakati Ajib anahojiwa juu ya swala hilo ni wazi jamaa alikua na bashasha na furaha flani hivi. Tabia ya Zahera kuwananga wachezaji hadharani ni tabia flani za Wakongo, yaani hao jamaa wanapenda kuonekana wako juu kuliko hata uhalisia. Nikupe mfano mmoja, Huyo Zahera anaye jinasibu kuwapa pesa wachezaji wake, usishangae hana hata nyumba ya kuishi, hilo ni kawaida kwa Wakongo. Zahera anajiona anajua sana. Fikiria jana anawalaumu wachezaji kwamba hawajiongezi, tena analaumu hadharani ili kujikosha na kuonekana yeye hana kosa. sasa alitaka wafanyeje kama sio kufuata maelekezo ya kocha na hata kama wangejiongeza wakafanya tofauti jamaa angelaumu kuwa hawakufuata maelekezo. Kinachofanya wachezaji wa Yanga kuwa wapole ni kwakua hakuna tumaini ya kupata timu mbadala yenye hadhi kubwa kwa wakitazama huo Unyamani kumejaa sasa wanabidi kukomaa na kusubiri labda kocha afukuzwe ili amani irejee. Kama kocha anawasimanga hadharani sasa huko vyumbani si akunakutukanwa?