Big, Bigger, Biggest...


Maker Pen kubwa kuliko zote(2.74m)

Ilitengenezwa na Muhammad Dileef mwaka 2020 ili kuwapa motisha kizazi kijacho wajifunze kuandika kwa kutumia mikono(bila msaada wa teknolojia)
 
I like it, Thanks for the knowledge mate.
 
Strepy Thieu Boat lift(Belgium)- ni lifti ya kubebea boti yenye urefu wa zaidi mita 73 na uwezo kubeba tani 350 na ndo ilikua lifti ndefu kuliko zote duniani kwa muda mrefu mpaka 2016 ilipokuja kupigwa bao na Ship lift ya Three gorges Dam(113m, tani 3000)




Lengo hasa la wabelgiji kuwa na hii lifti ni ili kutimiza ndoto yao ya muda mrefu ya kuweka kuonganisha mito miwili ya Meuse na Scheldt ili iweze kukatiza katikati ya nchi. Tatizo pekee walilokua nalo ni kwamba mito hiyo ina tofauti yq kimo(asl) ya zaid ya mita 96
Ila kwa teknolojia hii mambo murua kabisa waliweza kutengenezwa hii canal inaitwa SART CANAL ambapo magari yanapita chini baadhi ya sehemu na mto unapita juu
 

Kisiwa kilichojengwa kila square inch (Kimetelekezwa sasa)

UPDATE:

Kinaitwa Hanshima Island au majina mengine Gunkajima/Battleship Island. Kipo Japan

Kilitengenezwa kwanza kwa lengo kubwa la kuwa machimbo ya makaa ya mawe chini ya bahari toka mwaka 1887 huko kwahiyo walijengewa watumishi wa mgodi na kikakua sana ikawa alama kubwa ya mapinduzi ya viwanda japani. Ila wakati wa vita ya pilibya dunia serikali ya japani ilianza kukamata mateka wa vita haswa wakorea na kuwapeleka kufanya kazi kwa nguvu/bila malipo

Kwahiyo baada ya vita na ukizingatia msimamo wa japani kujitenganisha na matumizi ya silaha(pacifism) na makosa ya uhalifu wa kivita basi walihamisha watu wote na kukifunga.

Japokua stori nyingine ni kuwa "eti" kuna ghosts za watu waliouwawa, na pia kuna ajali ilitokea mafuta yakamwagika(petroli)

Kwa sasa kimefunguliwa tena kwa ajili ya utalii tu watu wana organise tours kwenda kushangaa ila sio kuishi
 
aisee
 
Haiwezekani tukadai hii Mali yetu iliyopelekwa ujerumani?
Hii ndiyo Taarifa ya mwisho niliyoipata kuhusiana na Masalia ya Dinasour huyo?

WABUNGE Kumi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameanzisha kamati maalum ya kuhakikisha sehemu ya mapato ya utalii yanayotokana na mabaki ya mjusi mkubwa aliyeko katika jumba la makumbusho Mjini Berlin nchini Ujerumani yanarejeshwa hapa nchini. Mjusi huyo anatambulika kwa jina la DINOSAUR ambaye mabaki yake yalivumbuliwa zaidi ya miaka 100 iliyopita katika eneo la Tendaguru mkoani Lindi. Tangu kugunduliwa kwa mabaki hayo na hata kusafirishwa hadi mjini Berlin nchini Ujerumani hakuna kiasi chochote cha mapato kilichowahi kurejeshwa hapa nchini ikiwa ni faida inayotokana na utalii wa mjusi huyo hali iliwalazimu wabunge hao wakiongozwa na mwenyekiti Riziki Lulida kuanzisha kamati hiyo .​

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…