Big Brother Africa 2009: The Revolution

Its good day for us, i was so worried today.... Huh, thanks God
 
yaaani kweli ukisikia maajabu basi ya leo ni maajabu maana watu wote tulikuwa matumbo moto, Eliza atazivuta hizi pesa wazee kama amekwepa hii eviction leo basi, maana niliona Cristal na Quinn walikuwa ndio the strongest contenders, labda sasa shida itakuwa kwa Edward
 
Mbogela u r a true addict of BBA!!!
I WAS IN 2007 wakati wa Richard...never again!
 
Mbogela u r a true addict of BBA!!!
I WAS IN 2007 wakati wa Richard...never again!

nimekosa hiyo ya richard kwasababu nilikuwa sehemu haina net kabisa, lakini ya mwisho niliangalia day 1 mpaka siku ya mwisho
 
nimekosa hiyo ya richard kwasababu nilikuwa sehemu haina net kabisa, lakini ya mwisho niliangalia day 1 mpaka siku ya mwisho
BBA 2007.... ilikuwa ni homa ya jiji...watu wengi walikuwa hawakai mbali na luninga zao....peopleof all ages and walks of life...it was something else.
 
Ebana mi leo nimefurahi sana...

  1. Ushindi wa jana wa Chelsea jana
  2. Kufungwa kwa Man Utd na L'pool leo
  3. Ku-droo kwa Arsenal leo
  4. Kubaki kwa dadangu Elizabeth ndani ya BBA House!
Full shangwe 😛
 
BBA 2007.... ilikuwa ni homa ya jiji...watu wengi walikuwa hawakai mbali na luninga zao....peopleof all ages and walks of life...it was something else.

Ya mwaka jana nadhani kwa Wa TZ wengi ilipoteza mvuto baada ya mwakilishi wetu kutolewa mapema, hata hivyo niliiangalia mpaka mwisho. Lakini leo nimefurahi sana, huyu mtoto anahitaji kubadirika sasa huko ndani aache hizo mood zake zisizotabirika anatuweka watu matumbo joto
 
Pair zimevunjwa sasa kila mtu anajitegemea, haya mbombo inogile
 
Elizabeth kama walivyo washiriki wa kike wengi kwenye Jumba hawataki yawakute yaliyomkuta Tatiana 2007..unakosa mshiko na Boyfriend anakumwaga kwa vile ulipendana na mtu ndani mle.Kanishangaza Krystal alipokuwa anahojiwa..akasema
" I love my boyfriend more than I love myself!" Aliniacha mdomo wazi.
 
Mlioangalia mbona kama Kelvin alikuwa bado anaomba wakati wanasubiri jina kutajwa imekaaje hiyo au nimeona vibaya
 
Watazamaji tunakubaliana na msimamo wake lakini inayotupa shida ni kuwa huwezi kumkataa mtu kistarabu bila kulia machozi na kubadirika mood ukawa kama mgonjwa ukawachunia na House mates wote?
 
Kanishangaza Krystal alipokuwa anahojiwa..akasema
" I love my boyfriend more than I love myself!" Aliniacha mdomo wazi.

Thats her, and i think she knows exactly what she meant... wewe je?
 
Thats her, and i think she knows exactly what she meant... wewe je?
sidhani kama alikuwa sahihi huwezi kuwa extremist kwenye mapenzi kiasi hicho, kumpenda mtu kuliko unavyojipenda??? Lakini to a certain extend nakubalina na Vera kuwa wadada wengi wana bank their trust kwa wanaume na wanawapenda kwa moyo wote.
 
Watazamaji tunakubaliana na msimamo wake lakini inayotupa shida ni kuwa huwezi kumkataa mtu kistarabu bila kulia machozi na kubadirika mood ukawa kama mgonjwa ukawachunia na House mates wote?

She really love her boyfriend na hataki kabisa kuchanganya feelings..

Thats her, and i think she knows exactly what she meant... wewe je?

Honestly..hata kama nampenda vipi siwezi kudeclare that infront of millions of people wakati huna uhakika kama naye anakupenda kwa kiwango hichohicho
 
washiriki wa kike wengi kwenye Jumba hawataki yawakute yaliyomkuta Tatiana 2007..unakosa mshiko na Boyfriend anakumwaga kwa vile ulipendana na mtu ndani mle..
Hivi Richard naye ilikuwaje na Mke/Girl friend wake maana nasikia maara ya kwanza alikubali kuwa lilikuwa game lakini baadaye alikuja kubadiri kibao kampiga mshikaji taraka, vipi ilikuwaje?
 
Elizabeth ameahidi kwamba kuanzia sasa atabadilika, ila sijajua hayo ni mabadiliko gani.

Kevin and Elizabeth sit on the couch contemplating their un-pairing. Kevin advises Elizabeth on her game plan. Elizabeth says that she is glad to have made it this far but she plans on being herself from now on.

Ngoja tuone wiki ijayo mambo yatakuwaje.
 
Elizabeth ameahidi kwamba kuanzia sasa atabadilika, ila sijajua hayo ni mabadiliko gani.

Ngoja tuone wiki ijayo mambo yatakuwaje.
Mkuu karibu ulikuwa umejificha wapi???? Presure watu zilikuwa zinapanda zinashuka, Nadhani Eliza amebakizwa ndani sababu ya Kelvin alionyesha uungwana sana pamoja na kupigwa buti wasi wasi wangu kuwa sasa akisimama kwa miguu yake mwenyewe (Eliza) inaweza ikawa hatari sana kama hatabadiri strategy.
 
She really love her boyfriend na hataki kabisa kuchanganya feelings..

Huyo ni msanii, amesema hivyo kwa kuwa ametoka salama bila touchy touchy. Ninakumbuka alishawahi kusema kwamba ana boyfriend nyumbani lakini likitokea lolote ndani ya Jumba, kwake it was OK (hapa alikuwa anamaanisha akitokea mtu ndani ya Jumba na akamfia, angekuwa tayari kum-bwaga bf wake. Ukweli ni kwamba hakupata mtu wa aliyemvutia, na kuna dalili zote kwamba alikuwa akimtaka Jeremy ila bahati mbaya Jeremy akawa amevutiwa na Emma.

Honestly..hata kama nampenda vipi siwezi kudeclare that infront of millions of people wakati huna uhakika kama naye anakupenda kwa kiwango hichohicho

Lakini VeraCity unasahau kwamba matendo yatakushitaki, unajua kama unampenda bf wako, hata usipotamka mbele ya mamilion ya watu, bado matendo yako yataonyesha. Akina dada/mama huwa wako weak sana kwenye hiyo area, huwa hawawezi kuficha feelings zao na watu wengine wakikuona watajua tu kwamba umekolea kwa bf. Wanaume tunaweza kuficha na wala tusionyeshe kwa watu wengine.
 
Hivi Richard naye ilikuwaje na Mke/Girl friend wake maana nasikia maara ya kwanza alikubali kuwa lilikuwa game lakini baadaye alikuja kubadiri kibao kampiga mshikaji taraka, vipi ilikuwaje?
Richard was newly married alipoingia BBA...
Mapenzi yake na Tatiana yalikuwa hatari maana kila mtu alijua Richard na mkewe ndio basi tena.Alipojishindia mshiko wake..hakumjua cha Tatiana wala nini alirudi kwa mkewe..
Mke naye alikuwa anataka kumwacha Richard...wakapatanishwa na sasa wana mtoto tayari. Tatiana aliachwa na mchumba wake.....na aliamini kuwa Richard atamwacha mkewe ili wawe pamoja.Ikawa pata potea.

Ni hiyo hali ya ndoa ya Richard iliyoweza kumfanya aonewe huruma na watazamaji hadi akawa mshindI.In a way, Tatiana alicheza nafasi kubwa sana katika ushindi wa Richard na kwa kiwango kikubwa aliweza kumsaidia akabaki kwenye jumba bila ya kuwa evicted.Kuna wakati Tatiana hata alimuokoa Richard from nominations na kujiweka yeye mwenyewe...this shows how women love earnestly! Sidhani Richard angeweza kujitolea kivile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…