Nasikia kwenye elimu kuna wimbo mpya umeanzishwa. Ajabu ya wimbo huu ni kuwa waimbao huimba maneno yao, wasikiao husikia ya kwao na wachezao hucheza mdundo wao. wanasiasa na watendaji serikalini wanaamini kuwa wameshafanya yatoshayo kubadili matokeo yale ya zero kuongoza na one kushika mkia. Wazazi na wanafunzi ambao ni wasikilizaji wametoa macho kuona angalau dogo linalotokea kuashiria tofauti lakini wanaishia kuona yale yale ya shule bila vitabu,darasa, madawati wala walimu. Walimu waliopo shuleni wanacheza ngoma yao ya sukuma siku mwisho wa mwezi ufike. Wameshazoea kuishi kwa kutukanwa na Mangi. wanachojua wao ni kile kile cha siku zote hawaruhusiwi kugoma, hawaruhusiwi kufanya biashara shuleni, hawaruhusiwi kufundisha tuition na sehemu nyingi wanabidi kukubali kucharazwa bakora na wakuu wa wilaya na wazazi. Wanajamii wenzangu mazingira ni muhimu sana katika kuelimisha.Hivi mazingira ya Elimu Tanzania yana dalili yoyote ya kuleta matokeo chanya? Hivi haya yanayoitwa matokeo makubwa ni chanya au ni hasi? mawazo yasiyotiwa katika matendo ni mfu.Sisi kama jamii hatujaanza kutenda yale yafanyayo elimu ilete matokeo hata madogo tu. sasa taraja hili jipya ni nini kama si ndoto mpya? NAOMBA KUWASILISHA