Haya ndiyo aina ya maswali tunayopaswa kujiuliza ili kuweza kunoa vichwa, ninaomba tuweke uzalendo pembeni ili tuingie darasani kidogo tujadili hesabu za kiuchumi.
1) Tukubaliane na hizi takwimu ulizozileta na tuanze kuzifanyia kazi, mwaka 2010 GDP ya Kenya $40B, uchumi unakua kwa wastan wa 5.5%, na GDP ya Tanzani ilikua $31B, uchumi unakua kwa wastani wa 7%. katika mwendokasi huo utasemaje gap inaongezeka badala ya kupungua au angalau kubaki lile lile?.
Kama kweli gap linaongezeka, basi yafuatayo ni mambo ambayo yanaweza kuchangia
1)GDP ya Kenya ilikuwa kubwa kuliko hiyo uliyotaja ya $40B, au
2)GDP ya Tanzania ilikuwa Ndogo kuliko hiyo iliyotajwa ya 31B au
3)uchumi wa Kenya umekua kwa kasi zaidi ya ile ya Tanzania
4)GDP ya Kenya ya sasa hivi sio sahihi, ni ndogo kuliko inavyotangazwa
5)GDP ya Tanzania ni kubwa kuliko inavyotangazwa.
Sasa tuje katika kutumia akili tu za kawaida ambazo mtu huitaji kwenda darasani, ukiangalia njia kuu zinazoziingizia mapato hizi nchi mbili, kama vile FDI, utalii, Kilimo, Manufacturing, construction, Financial services na Transportation, bado Tanzania inafanya vizuri zaidi ya Kenya katika maeneo mengi, isipokua manufacturing and financial services tu, zaidi ya maeneo hayo, Tanzania inapata mapato ya ziada kwenye madini na gas ambazo Kenya hakuna. Sasa unaposema gap la Kenya na Tanzania linaongezeka badala ya kupungua, ni kwa uchawi gani unafanyika mpaka gap liongezeke?, ndiyo pale baadhi ya watu wanakuwa na wasiwasi na uhalisia wa ukweli wa GDP ya Kenya.