Big Up AliKiba! Hakuna Cha English Hapa!

Big Up AliKiba! Hakuna Cha English Hapa!

eRRy

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2009
Posts
1,126
Reaction score
206
[ame="http://www.youtube.com/watch?v=SdrTkDNcaWY"]http://www.youtube.com/watch?v=SdrTkDNcaWY[/ame]
 
Mkubwa kiinglish kigumu hahaha...Sio mchezo!! Nimesikia katika maswali aliyoulizwa hapo amesema her tu sio zaidi..
 
Mimi namheshimu mtu yeyote anayeelewa kwamba kwa kulazimisha kuongea kiingereza ambacho hana uwezo mkubwa nacho, anaweza kukosa uwezo wa kujieleza vizuri.

Au hata yule anayejua kiingereza vizuri lakini kusisitiza kutumia lugha yake.

Kuna ulimbukeni unaojikita katika jamii sasa hivi unaoambatanisha kiingereza na usomi. Wakati ni ukweli usiopingika kwamba watu wengi waliopata fursa ya elimu ya kimagharibi nzuri wanajua kiingereza, au niseme wengi wa wanaojua kiingereza vizuri wamepata fursa ya elimu ya kimagharibi, pia ni ukweli kwamba kupata fursa ya elimu ya kimagharibi si kuelimika, na kujua kiingereza si kuelimika, na mtu anaweza kuongea kiingereza cha kilimbwende lakini bado akakosa mantiki na wala asilete tija.

Kwa hiyo kama mtu anajisikia kuongea kiingereza ni bora akijue vizuri, la hasha aongee lugha anayoijua vizuri.

Zaidi ya yote, kuchanganya Kiswahili na Kiingereza ni ishara ya kutojua vizuri lugha zote hizi mbili.
 
Back
Top Bottom