mimi huwa nawahurumia sana mashabiki wa simba wanaoingia kichwa kichwa kuwaiga yanga kwa kumsema vibaya huyu kocha sven: eti hafai kweli? eti wakimlinganisha na patrick osseums wanaona huyu bado sana!! mi naona ni wagumu wa kuelewa na kupima uwezo wa makocha.. patrick alikuwa anapendwa na mashabiki kwa sababu alikuwa mhamasishaji tofauti na huyu. huyu yuko more technical ila anakosa uwezo wa kuhamasisha mashabiki kama alivyokuwa anawafanyia patrick. na ndio maana ukifuatilia simba chini ya sven huwa ubora wake uko katika level moja na mara nyingine huwa unapanda tofauti na patrick ambaye leo mnashinda nyumbani kesho mnaenda kufungwa tano ugenini kitu ambacho sven hakiwezi kutokea. anachezesha mshambuliaji mmoja mbele na kwa uhakika timu inakuwa bora kabisa na inafunga magoli mengi zaidi ukiliganisha na patrick alikuwa anachezesha washambuliaji wawili lakini timu bado ilikuwa inafunga magoli machache. kwa sven kila mchezaji ni mfungaji, mshambuliaji anabaki pale kwa ajili ya kudstab walinzi wa timu pinzani. hebu fuatilia match ya platinum waliofunga magorli ni mabeki na viungo, boko amekuja kuambulia mwishoni kwa bahati tu. tuendelee kumwamini sven mimi bado naona ni kocha bora kabisa kumzidi patrick