Big Up Mzizi Mkavu, Asante Jamii Forums!

Big Up Mzizi Mkavu, Asante Jamii Forums!

Inch 9

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2024
Posts
1,093
Reaction score
1,365
Hamjambo member wote wa JF?

Mimi naitwa inch 9, mwanachama mpya mkongwe wa JF nichukue fursa hii kumshukuru Mungu wangu pamoja na wale waliofanikisha kunileta duniani.

Awali ya yote napenda nimshukuru pia member mkongwe wa JF wa kuitwa Mzizi Mkavu kwa sababu kupitia yeye ndo nilianza kuufahamu mtandao huu wa JamiiForums kwa mara ya kwanza kabisa na sababu ya kukutana na huyu mwamba.

Ilikuwa hivi:
Mwaka 2011 nilikuwa na msichana mmoja ambaye alikuwa ni girlfriend wangu kipindi hicho yeye alikuwa na changamoto ya kuumwa na tumbo chini ya kitovu; sasa mimi kabla sijafanya uamuzi wa kwenda hospitali nikaamua kuzama mtandaoni(hii ni kawaida yangu hata sasa).

Basi bwana kwenye kupekuwa pekuwa nikakuta kuna site imezungumzia kile nilichokuwa natafuta, nikafungua nikasoma baada ya kumaliza shida yangu nikataka kujua ni page gani nimetembelea nikakuta imeandikwa "Dr mzizi mkavu" anakopatikana Jamii Forums.

Toka hapo nikawa hata nikiwa na kwikwi natembelea JF kuuliza hivi kwikwi inasababishwa na nini (NATANIA) nikawa mlevi wa JamiiForums, naingia majukwaa mbalimbali nafanya utalii wa mambo mbalimbali ya JF na majukwaa yangu pendwa ni jukwaa la Mahusiano, Hoja Mchanganyiko na jukwaa la Spoti ila hili siku hizi siingii sana kwa sababu nimejipa miaka mitano nataka kuachana na mambo yote ya michezo kwani naona hayana tija kwangu. Na pia mimi ni shabiki wa MAN UTD na Bongo SIMBA SC, na kuonyesha usiriasi wa jambo langu sijasikiliza kipindi chochote cha michezo toka siku Simba afe chuma tano na Yanga mpaka leo.

Hivyo natoa shukrani zangu pia kwa uongozi wote wa Jamii Forums kwa mambo mengi niliyojifunza kupitia mada mbalimbali za wanachama wake humu jamvini na bila kusahau tukio lililonifanya niwe mwanachama.

Iko hivi, tunapitia kaugomvi fulani na wife hivyo kuna minuno moja mbili tatu tunapitia sasa jana usiku nikaingia JF kuchukua nondo za kumkabili wife (huyu ndo yule wa tumbo 2011 tuna watoto wawili Now)sasa wakati nimefungua nipige chabo naona maandishi mekundu kwamba nimebakiwa na page 5 kama mgeni kutembelea JF nikadhani ni mzaha, naamka asubuhi naingia ikanigomea nikaona ohooo yamekuwa hayo! Nikaona isiwe tabu, JF ndo mfariji wangu, kwa hiyo nikajianika kwa bwana Melo mambo mengine tutajua hapo hapo.

Dah! Eti na mimi ni member, nakuja eti na mimi kumkomenti GENTAMYCINE kama Genta mimi uso kwa uso na cocastic; ila sema nini, JamiiForums ukiitumia vizuri ni fursa.

Nisiwachoshe sana wasomaji, hivi ndivyo nilivyoijua JamiiForums.

Aluta Continua
 
Hahahaa mkuu kenzy usijipe moyo uenda wife anapigania inch 9 yake
 
Kwanini unajiita Inch 9 ?
Anyway 😂 Karibu sana hapa konani

 
GXSjdPnWUAAzb2j.jpg
 
Back
Top Bottom