....uwezekano mwingine alirudia shule[darasa la saba] na kulazimika kubadilisha jina.
Angekuwa amerudia darasa la saba, angekuwa na jina tofauti na la baba yake. Baba anaitwa William Mukasa, yeye alikuwa Oscar Mukasa na sasa amebadilisha na kuwa Oscar Rwegasira.
Kama angekuwa Oscar Rwegasira na kubadilisha kuwa Oscar Mukasa, ningekubaliana na hoja ya kurudia darasa la saba.
Kwa hiyo swali la kujiuliza kwanini amebadilisha jina mara baada ya kuteuliwa kuwa mgombea wa CCM? Ana umri wa miaka 39 sasa, kwanini hakubadilisha alipokuwa O-Level, A-Level ama Mlimani au wakati akifanya graduate program?
Lazima kuna kitu kinafunikwa, je ni tatizo la uraia? Ama ni tatizo la ukabila? Ama ndo njia ya kujisogeza kwa wapiga kura ili aonekane ni mwenzao (mwana Biharamulo)?
Nina hakika tatizo hilo walilishitukia tangu kwenye kikao cha CC na ndiyo maana mjadala ulikuwa mrefu kama FMES alivyotoa taarifa za uteuzi kwamba malumbano yalikuwa makali sana.
Ugomvi wa wana CCM (Mtandao vs Non-Mtandao) utasaidia sana kuwapa data wapinzani na nina hakika data za uraia zinaweza kuwa zimevuja kutoka kwenye kikao cha CC kilichojaa malumbano. Sijawahi kusikia CC wamelumbana kupitisha jina la mgombea na hasa ikizingatiwa kwamba Bw. Oscar Mukasa a.k.a Oscar Rwegasira alikuwa ameongoza kwenye kura za maoni, je ni hoja zipi zilizosababisha CC walumbane kumpitisha mtu aliyeongoza kura za maoni?