Biharamulo: Kampeni, kura na matokeo!

Biharamulo: Kampeni, kura na matokeo!

....uwezekano mwingine alirudia shule[darasa la saba] na kulazimika kubadilisha jina.

Angekuwa amerudia darasa la saba, angekuwa na jina tofauti na la baba yake. Baba anaitwa William Mukasa, yeye alikuwa Oscar Mukasa na sasa amebadilisha na kuwa Oscar Rwegasira.

Kama angekuwa Oscar Rwegasira na kubadilisha kuwa Oscar Mukasa, ningekubaliana na hoja ya kurudia darasa la saba.

Kwa hiyo swali la kujiuliza kwanini amebadilisha jina mara baada ya kuteuliwa kuwa mgombea wa CCM? Ana umri wa miaka 39 sasa, kwanini hakubadilisha alipokuwa O-Level, A-Level ama Mlimani au wakati akifanya graduate program?

Lazima kuna kitu kinafunikwa, je ni tatizo la uraia? Ama ni tatizo la ukabila? Ama ndo njia ya kujisogeza kwa wapiga kura ili aonekane ni mwenzao (mwana Biharamulo)?

Nina hakika tatizo hilo walilishitukia tangu kwenye kikao cha CC na ndiyo maana mjadala ulikuwa mrefu kama FMES alivyotoa taarifa za uteuzi kwamba malumbano yalikuwa makali sana.

Ugomvi wa wana CCM (Mtandao vs Non-Mtandao) utasaidia sana kuwapa data wapinzani na nina hakika data za uraia zinaweza kuwa zimevuja kutoka kwenye kikao cha CC kilichojaa malumbano. Sijawahi kusikia CC wamelumbana kupitisha jina la mgombea na hasa ikizingatiwa kwamba Bw. Oscar Mukasa a.k.a Oscar Rwegasira alikuwa ameongoza kwenye kura za maoni, je ni hoja zipi zilizosababisha CC walumbane kumpitisha mtu aliyeongoza kura za maoni?
 
Wanajamvi,
Katika mjadala huu nimebaini kuwa kuna watu hapa jamvini hukomalia (kuwa negative) na zile issues ambazo hawana maslahi nazo. Lakini kija issue ambayo iko wazi kabisa hata kwa mtoto mdogo wao watajifanya hawaioni. Suala la Mukasa ni la kisheria zaidi bila kujali amefanya nini nchini au amesoma wapi au wazazi wake walikuwa maafisa serikalini. Kuna mchangiaji mmoja anamtetea sana Mukasa, lakini siku za nyuma kidogo aliweka mtundiko hapa akisema tatizo la watanzania ni kutofuata sheria (kutoheshimu sheria) lakini leo huyo huyo hawezi kuona kuwa Mukasa inawezekana hakufuata sheria ya kuukana urai wa wazaziwe alipotimu miaka 18. Naombeni kama jambo liko wazi tukubali makosa hata kama linamhusu mtu au kikundi ambacho una maslahi nacho, itatusaidia sisi wachanga hapa JF kuwafuata nyinyi kama mifano mizuri kuliko mnavyofanya sasa.
 
imewezekana kwa rostam itashindikana kwa mukasa? kwa alivyoanikwa hapa anaweza kujitoa kabla hata ya uamuzi wa tume
 
Binafsi nilijua Chadema hawafiki mbali - kwani Jaji Lewis Makame akale wapi ? mzee wa watu na umri ndio huo tena. Kisheria Oscar Mukasa hawezi kuwa Oscar Rwegasira - labda akale kiapo mahakamani. Kuna ushahidi wa tangu awali kuwa Oscar Mukasa ndiye alijitokeza kuwania ubunge kwa tiketi ya CCM. Hili jina ndilo lililowasilishwa CC na ndio maana wadakuzi wakatutangazia kuwa aliyeteuliwa ni Oscar Mukasa

Hata hivyo baada ya vuta nikuvute ndani ya kikao cha CC kuhusiana na jina Mukasa, kikao kinachojulikana zaidi kwa kuhalalisha ufisadi, jina Rwegasira likawa "invented". Shughuli kubwa iliyofanyika baada ya hapo ni kulihalalisha hili jina na kikao kilimalizika tu baada ya kuhakikisha kuwa mamlaka zote husika zimehamasishwa. Ndio maana tunasikia habari za CCM chama makini, hakiwezi kufanya kosa kama hilo.
search_redirect.php

s891520514_6312.jpg
search_redirect.php

Oscar Mukasa - Rwegasira katoka wapi ?

CCM wameweza kumhalalisha Abdulrasul Chakaar
watashindwaje Oscar Rwegasira ?

- Sio kweli mkuu, kuna wana-JF waliothibitisha hapabaada tu ya kikao cha CC kwamba Oscar pia ana jina la Rwegasira, kwa sababu wanafahamiana naye kwa siku nyingi, sijui mengine kwenye hili la jina la Rwegasira kuna walioshuhuda hapa wkamba ni jina lake pia siku zote.

Respect.

FMEs!
 
Mag3 View Public Profile Send a private message to Mag3 Find all posts by Mag3 Add Mag3 to Your Contacts
#185 (permalink)
post_old.gif
5th June 2009, 09:58 PM
Masanilo
user_offline.gif

Masanilo is Alcoholic
JF Premium Member
Join Date: Tue Oct 2007
Location: Lahore
Posts: 2,668
Thanks: 709
Thanked 1,269 Times in 805 Posts
Rep Power: 67
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif

Credits: 1,004,636,755

icon1.gif
Re: CCM: Kamati Kuu Kukaa Chini Dar

Quote:
Mag3

Mukasa/Rwegasira - One and the same ?

Anaitwa Oscar Rwegasira Mukasa ni mtu mmoja! CHADEMA lazima waweke mgombea makini, vinginevyo jimbo walisahau! Hawa CCM wako makini, siipendi lakini ndo hivyo! Maana naona hata hapa JF kampeni ni kali zimeisha aanza naona watu wapo kiitikadi zaidi...

Mas
__________________
"People who drink to drown their sorrow should be told that sorrow knows how to swim." Ann Landers

- Mkuu Mag3, soma hapa.

FMEs!

JAMANI nadhani swala la uraia watu tumeshaliongelea hapa mpaka sheria na misahafu ikatundikwa humu. Kikubwa hapa naomba tujue kwamba..kila mtu anayo haki ya kubadilisha jina lake na kuitwa anavyotaka. Hata kama angeamua kuitwa Chungwa au embe...its him! Unless proved otherwise.

Nategemea watu humu JF tulijadili swala hili objectively. Kwanza, lazima tujue kabisa watu wengi wa Tanzania especially wa mikoa iliyo pembezoni mwa nchi kama Kagera, Kigoma, Mara nk..wengi wa wananchi wana connection na nchi jirani either kwa lugha au undugu. NA HILI ni purely geographical accident halikwepeki. Mtu wa Kigoma au Ngara definitely yuko closer na mtu wa Burundi kuliko mtu wa Rukwa kwa sababu ambazo ziko wazi kabisa. Wanaongea lugha moja! So is mtu wa Mara na mtu wa Kenya. But kasumba ambayo tunaiendekeza especially wabongo wengi..ni kuwaona raia wa hizi sehemu kama warwanda au warundi..simply because they speak similar language..same ukija Msoma..Mkurya ataambiwa..wewe kwanza ni mkenya..and on and on.. Hili lazima tulikubali kama legacy ya mipaka iliyowekwa blindly na mkoloni na kuhalalishwa na nchi zetu baada ya uhuru. Na hawa watu wameingiliana maana ndo wanasaidiana katika shida na raha..Its purely geographical accident.

Pili, lazima tujue kwamba Tanzania yetu sheria nyingi ziko kwenye mashelf wananchi waliowengi hawazijui na viongozi ambao wanapaswa kuzitekeleza wanafumba macho..zinaibuliwa pale kunapokuwa na maslahi ya watu fulani. Kwa hiyo usishangae kuona kuna warwanda, wakenya, waganda..name them..wameishi tanzania wakaoa watanzania..watoto wao wamezaliwa Tanzania..wamekulia tanzania kifupi they have known no other homeland than Tanzania. Na wamefanya yote haya bila kuulizwa na mtu. Sasa inapofika watoto kama hawa waliohangaika kama watanzania, ingawa wazazi wao either hawakuwa raia au hawakuhalalisha uraia wao.. wengine wanataka ku-participate kwenye shughuli pevu kama hizi za kisiasa..ndo sheria zinaibuliwa. Sasa huyu mtu aende wapi? mtu kazaliwa kijijini hata hiyo birth certificate hana! Yes, ni rahisi kusema kwamba watu wahalalishe uraia wao..lakini do you think..hii fursa ni wangapi wanaijua? Na swali langu kubwa..why should we punish a child kwa sababu ya makosa ya wazazi wake? Huyu hata ungemrudisha Uganda kwanza atajulikana kama Mtanzania..na at the end of the day..atakuwa Stateless. Maana hata huko hatakubalika!

Kama alivyouliza FMES..iweje kama baba siyo raia afikie level kubwa ya utumishi katika jamhuri yetu? Jibu wote tunalijua..swala la uraia ni kadi ya maslahi especially siasa. na si Tanzania tuu..its all over Africa.

Mi nadhani issue kama hizi za uraia..ni vema ku-raise legitimate questions, lakini tusiwahukumu watoto ambao wamepigana kama sisi..simply because their parents did this or that. Ni kuwanyima fursa...simply because baba au mama hakufanya kitu fulani..ni kama kumuita mtoto wa nje ya ndoa..illegitimate..its damn unfair..maana mtoto hakuhusika na maelewano ya wazazi wake..sasa kwa nini leo anyimwe haki sawa..simply because alizaliwa kwa baba aliyekimbia mimba? Think about it. NA KUNA SHERIA KAMA HIZI ARCHAIC NYINGI..BADO ZIMO KWENYE VITABU VYETU!

Ndo maana governance inatushinda, maana jiulize..ni lini hawa wanaomuwekea pingamizi walijua kwamba jamaa siyo raia? mbona hawakusema hilo mapema? Ofcourse Chadema wana haki ya kuuliza maswali kama haya..lakini..sisi kama wasomi humu JF..we should go beyond these cheap talk..tupeane ideas namna ya kuli-address hili tatizo maana kuna silent majorities wengi sana kwenye hii dilemma. Yaani baba ni wa kuja lakini mtu kazaliwa Tanzania na ameishi TZ miaka yote..leo amemaliza Chuo kikuu..amepata scholarship ya kwenda PHD nje..ananyimwa passport kwamba siyo raia..it doesnt add up..mtu kama huyo..anakuwa frustrated sana...yuko radhi kutoa rushwa yoyote apate hiyo passport.

My suggestion: Tufanye kama USA with some modifications kiasi..kila mtu ahukumiwe kama yeye! Kama umezaliwa ndani ya mipaka yetu basi wewe ni raia (with few exceptions kama wakimbizi walio chini ya uangalizi wa sheria za kimataifa..etc).... Hii itawasaidia watoto wengi..especially wanaozaliwa vijijini. Otherwise hii ni political witch hunt..ambayo inamuumiza kijana wa watu kwa kosa ambalo hakulifanya. Angalia hata CV yake..kijana ni mpiganaji..leo anaambiwa eti siyo raia..duh!

Masanja,

- Mkuu Masanja, kama kawaida you always come through wakati unapokuwa muafaka, tupo pamoja sana hapa.

Respect.

FMEs!
 
- Sio kweli mkuu, kuna wana-JF waliothibitisha hapabaada tu ya kikao cha CC kwamba Oscar pia ana jina la Rwegasira, kwa sababu wanafahamiana naye kwa siku nyingi, sijui mengine kwenye hili la jina la Rwegasira kuna walioshuhuda hapa wkamba ni jina lake pia siku zote.
Respect.
FMEs!

Mkuu labda hapa hatujaelewana - sijasema Oscar Mukasa siye Oscar Rwegasira. Mimi nasema jina lililowasilishwa CC ni Oscar Mukasa lakini lililopitishwa na CC ni Oscar Rwegasira - kwa nini ?

Jina linalojulikana na aliliolitumia toka utoto wake na kwenye vyeti vyake ni Oscar Mukasa lakini baada ya kikao cha CC, jina limebadilishwa na kuwa Oscar Rwegasira - kwa nini ? Mbona jitihada kubwa zimefanyika kulizika jina la Mukasa - kulikoni ?

Kwa nini kama ilibidi yasitumike majina yote matatu Oscar Rwegasira Mukasa kama ilivyo kawaida ya wagombea. Hili jina Mukasa lina siri gani nzito? Je tunawaficha ndugu zake huko Uganda wasitaharuki ?
Mficha ficha maradhi, kilio humuumbua.
Yaonekana "surname" haina maana tena.
 
Ni kweli naona ni vizuri mamba tukimuita mamba. Tusimuite Kenge. Lakini tukumbuke kuwa inapofika swala la CCM, maslahi yake yanakuwa mbele zaidi kuliko maslahi ya Taifa.

- Ahsante mkuu, unajua walipokuchora kule Ze-utamu wewe na dada yako nilidhani wamekuonea, kumbe na wao walishaona mbali kuwa mamba lazima aitwe kama alivyo yaani mamba, Bwa! ha! ha!

- By the way, JF hua hatuburuziwi kama bendera, huwa tunauliza facts ni haki yangu kuuliza facts za uraia wa Muakasa Bin Rwegasira, halafu umesahau maneno yale kwamba JF huwa hatuwekezi kwenye majina hata akisema nani ni lazima tuulize, sasa kama wewe ulinishauri kwamba JF hatuwekezi kwenye majina ni lazima kuuliza, sasa leo nimeuliza nimekua kenge? Na kwamba najali masilahi yangu kwanza? Bwa! ha! ha! nyani bwana ni vigumu sana kujiona.

Uraia ni vitambulisho sio maneno, wala kenge wala mamba, sasa leo nikisema wewe Bongolander sio raia then ina maana wewe sio raia? No ninatakiwa kuonyesha ushahidi wa maneno na tuhuma zangu over you, sasa Chadema chama kikubwa na mbadala cha siasa Tanzania, wameweza kutupa majina ya mafisadi bila tatizo, leo ishu nzito kama hii ya uchaguzi kimewashinda nini kuweka ushahidi to the public na kuwamaliza CCM kabisa katika huu uchaguzi?

Mkuu samahani huwa sifikiriwi na wengine, au kushikiwa akili na wengine, sasa ninasema hivi kama Chadema wana hard facts za uraia wa huyu Mukasa na wameamua kuzikalia, basi wanahitaji kufukuza kazi washauri wote wa siasa walionao, kwa sababu the minute walipoweka pingamizi la mgombea kule NEC, pale pale wangetoa usahidi walionao kuwabana NEC wasicheze na ukweli, na huo ndio ungekuwa mwisho wa CCM huko Biharamulo, lakini badala yake maneno mengi na sasa kuanza kututukana wenye mawazo tofauti na yenu, ndio maana Chadema huwa hatuwachukulii serious, kwa mawazo kama haya mtatusaidia nini hili taifa?

Kama Chadema mnao ushahidi wa uraia wa Mukasa kutokuwa mbongo, na mmeshindwa kuuweka to the public mpaka leo, basi fukuzeni wote huko muanze upya ama sivyo yatakuwa yale yale kila uchaguzi, malalmiko bila substance, halafu mnataka kutafuta mwachawi JF as if sisi hapa ndio tunaoamua no! wakuu hapa tunachambua anything hatuogpi, wala kuogopeshwa na mtu au jina, lete habari inachambuliwa ninasema hivi leteni facts za uraia wa huyu mkuu tuzione hapa for once kama huyu ni raia au sio?

Respect.

FMEs!
 
Mkuu labda hapa hatujaelewana - sijasema Oscar Mukasa siye Oscar Rwegasira. Mimi nasema jina lililowasilishwa CC ni Oscar Mukasa lakini lililopitishwa na CC ni Oscar Rwegasira - kwa nini ?

Jina linalojulikana na aliliolitumia toka utoto wake na kwenye vyeti vyake ni Oscar Mukasa lakini baada ya kikao cha CC, jina limebadilishwa na kuwa Oscar Rwegasira - kwa nini ? Mbona jitihada kubwa zimefanyika kulizika jina la Mukasa - kulikoni ?

Kwa nini kama ilibidi yasitumike majina yote matatu Oscar Rwegasira Mukasa kama ilivyo kawaida ya wagombea. Hili jina Mukasa lina siri gani nzito? Je tunawaficha ndugu zake huko Uganda wasitaharuki ?
Mficha ficha maradhi, kilio humuumbua.
Yaonekana "surname" haina maana tena.

- Mkuu tunaelewana sana, sasa naomba kukuuliza hivi eti unasema kwamba jina la mgombea lilipopelekwa CC, hakukuwa na Rwegasira katika majina yake yaliyowasilishwa huko, is that what unachosema kwamba Rwegasira limeongezwa na CC? Kwamba si jina lake wala halikuepelekwa huko CC, eti hiki ndicho unachosema?

FMEs!
 
- Ahsante mkuu, unajua walipokuchora kule Ze-utamu wewe na dada yako nilidhani wamekuonea, kumbe na wao walishaona mbali kuwa mamba lazima aitwe kama alivyo yaani mamba, Bwa! ha! ha!

Umeshaanza kuleta za kuleta ili kutishia watu wanyamaze wasiseme, ukirudishiwa kibao unaanza kulia na kuita safina.

Acha vioja u mtu mzima sasa.
 
Umeshaanza kuleta za kuleta ili kutishia watu wanyamaze wasiseme, ukirudishiwa kibao unaanza kulia na kuita safina.

Acha vioja u mtu mzima sasa.

Ndivyo alivyo huyo...nadhani waalimu wake walipata shida sana, jamaa ni kiazi haswa!
 
Ndivyo alivyo huyo...nadhani waalimu wake walipata shida sana, jamaa ni kiazi haswa!

Halafu anajiita mwanasiasa, aliyezaliwa na kukulia kwenye siasa. Hebu arudi bongo tumfundishe siasa za kileo kuwa anaposhindwa hoja ananyamaza sio kuanza kwenda personal na kuleta vitisho.
 
Binafsi nilijua Chadema hawafiki mbali - kwani Jaji Lewis Makame akale wapi ? mzee wa watu na umri ndio huo tena. Kisheria Oscar Mukasa hawezi kuwa Oscar Rwegasira - labda akale kiapo mahakamani. Kuna ushahidi wa tangu awali kuwa Oscar Mukasa ndiye alijitokeza kuwania ubunge kwa tiketi ya CCM. Hili jina ndilo lililowasilishwa CC na ndio maana wadakuzi wakatutangazia kuwa aliyeteuliwa ni Oscar Mukasa

Hata hivyo baada ya vuta nikuvute ndani ya kikao cha CC kuhusiana na jina Mukasa, kikao kinachojulikana zaidi kwa kuhalalisha ufisadi, jina Rwegasira likawa "invented". Shughuli kubwa iliyofanyika baada ya hapo ni kulihalalisha hili jina na kikao kilimalizika tu baada ya kuhakikisha kuwa mamlaka zote husika zimehamasishwa. Ndio maana tunasikia habari za CCM chama makini, hakiwezi kufanya kosa kama hilo.
search_redirect.php

s891520514_6312.jpg
search_redirect.php

Oscar Mukasa - Rwegasira katoka wapi ?​

CCM wameweza kumhalalisha Abdulrasul Chakaar
watashindwaje Oscar Rwegasira ?

Mag3,

Mimi ni msukuma tu, ningekuwa mmasai ningejinyonga kama Mkwawa maana afadhali niishi kuliko kufa.

Maneno yako ni mazito mno.
 
Na wewe unaitwa Solo nani? Taja la sivyo utatajwa...

Sitaji, taja......

...umeunga bandwagon la kina sheikh Yahya feki, ukiiga tembo ...... utapasuka msamba.

Umefulia si chochote si lolote, huna maana. Hebu pisha huko.
 
Wanajamvi,
Katika mjadala huu nimebaini kuwa kuna watu hapa jamvini hukomalia (kuwa negative) na zile issues ambazo hawana maslahi nazo. Lakini kija issue ambayo iko wazi kabisa hata kwa mtoto mdogo wao watajifanya hawaioni. Suala la Mukasa ni la kisheria zaidi bila kujali amefanya nini nchini au amesoma wapi au wazazi wake walikuwa maafisa serikalini. Kuna mchangiaji mmoja anamtetea sana Mukasa, lakini siku za nyuma kidogo aliweka mtundiko hapa akisema tatizo la watanzania ni kutofuata sheria (kutoheshimu sheria) lakini leo huyo huyo hawezi kuona kuwa Mukasa inawezekana hakufuata sheria ya kuukana urai wa wazaziwe alipotimu miaka 18. Naombeni kama jambo liko wazi tukubali makosa hata kama linamhusu mtu au kikundi ambacho una maslahi nacho, itatusaidia sisi wachanga hapa JF kuwafuata nyinyi kama mifano mizuri kuliko mnavyofanya sasa.

- Mkuu ninakusikia sana haya maneno unanirushia mimi, binafsi simtetei Mukasa, kwanza nimesema toka siku nyingi sana kuwa simjui na wala sijawahi kukutana naye, infact hata siku ninapewa dataz za kupitishwa kwake I had a hard time sana kuandika vizuri chini jina lake,

- Katika hii ishu ya Mukasa, ninajadili kila ninachokisoma kumhusu, nimesikia dataz za CC, na nikazileta hapa bila tatizo ningekua na tatizo nisingezileta hapa, ningenyamaza kimya naomba nirudie tena kwamba so far sijaona hard facts za kuonyesha kwamba Mukasa sio raia wa Tanzania, kama unazo naomba uziweke hapa, nitakuunga mkono kwa 100%, lakini bila hivyo ni wajibu wangu kuuliza.

- Again naomba nikukumbushe tena, ni mimi niliyesema kwamba Mwalimu aliliharibu sana hili taifa kwa sababu hakupenda sheria, nia na madhumuni yangu kuwepo hapa ni siku moja kuona taifa langu Tanzania linakua linaheshimu utawala wa sheria, ila sitegemei kwamba the rule of law ninayoililia inaruhusu mtu mmoja kudai mwingine sio raia bila ushahidi halafu hukumu inatolewa na public and then kweli hule aliyetuhumiwa anakuwa sio raia, kwangu that is insanity na ni uendawazimu na sitaki kuamini ndicho unachokililia hapa, ninashukur sana kwamba wewe ni mchanga hapa JF as your usual, lakini hatuko hapa kupitisha ishus bila maswali serious, na huwa hatulazimishani, tunajadili,

Naomba kurudia tena msimamo wangu on this ishu, ninaomba kuona proof kwamba Mukasa sio raia wa Tanzania, nitakuiunga mkono 100% kama huna kama mimi basi tusubiri Oscar na CCM watakapojibu, kama kwa kuwa na msimamo huu ni makosa basi samahani kwa kukuwkaza wewe kichanga cha JF, lakini ndio msimamo wangu.

The rule of law ni lazima kuwepo na dual process, yaani chadema kumtuhumu mgombea na mgombea kupewa nafasi ya kujibu, kama kwa kuwa na mawazo haya ni kuweka masilahi yangu mbele na CCM so be it!

Respect.

FMEs!
 
Sitaji, taja......

...umeunga bandwagon la kina sheikh Yahya feki, ukiiga tembo ...... utapasuka msamba.

Umefulia si chochote si lolote, huna maana. Hebu pisha huko.

Wewe ndo huna maana na meno yako yaliyooza. Sasa you dared me. I'm a certified wingnut. Stay tuned for the nukes garden tool
 
Angekuwa amerudia darasa la saba, angekuwa na jina tofauti na la baba yake. Baba anaitwa William Mukasa, yeye alikuwa Oscar Mukasa na sasa amebadilisha na kuwa Oscar Rwegasira.

Kama angekuwa Oscar Rwegasira na kubadilisha kuwa Oscar Mukasa, ningekubaliana na hoja ya kurudia darasa la saba.

Kwa hiyo swali la kujiuliza kwanini amebadilisha jina mara baada ya kuteuliwa kuwa mgombea wa CCM? Ana umri wa miaka 39 sasa, kwanini hakubadilisha alipokuwa O-Level, A-Level ama Mlimani au wakati akifanya graduate program?

Lazima kuna kitu kinafunikwa, je ni tatizo la uraia? Ama ni tatizo la ukabila? Ama ndo njia ya kujisogeza kwa wapiga kura ili aonekane ni mwenzao (mwana Biharamulo)?

Nina hakika tatizo hilo walilishitukia tangu kwenye kikao cha CC na ndiyo maana mjadala ulikuwa mrefu kama FMES alivyotoa taarifa za uteuzi kwamba malumbano yalikuwa makali sana.

Ugomvi wa wana CCM (Mtandao vs Non-Mtandao) utasaidia sana kuwapa data wapinzani na nina hakika data za uraia zinaweza kuwa zimevuja kutoka kwenye kikao cha CC kilichojaa malumbano. Sijawahi kusikia CC wamelumbana kupitisha jina la mgombea na hasa ikizingatiwa kwamba Bw. Oscar Mukasa a.k.a Oscar Rwegasira alikuwa ameongoza kwenye kura za maoni, je ni hoja zipi zilizosababisha CC walumbane kumpitisha mtu aliyeongoza kura za maoni?

FMES anazo data za kwanini walikesha hata hawakulala kwao. Kama kweli FMES una mapenzi na nchi hii sema yote. otherwise unaniyeyusha kinoma.
 
Back
Top Bottom