Biharamulo: Kampeni, kura na matokeo!

Dr.Slaa,

..tunaomba ufafanuzi wako kama kweli OSCAR MUKASA alikuwa mwanachama wa CHADEMA.

Masanilo,

..kila siku tunapigiana kelele jamii forums kwamba watu wa ID zaidi ya moja.

..sasa kituko kama hicho naona ndiyo kinatokea kwa Oscar.

..msije mkashangaa akila kiapo cha Ubunge kama Oscar Rweyemamu.
 
Wakuu, mi nadhani hapa swala ni uraia. Na kigezo wengi wanachokitumia ni kwamba Oscar kabadilisha jina. Zaidi ya hapo hakuna ushahidi mwingine. Na wala kama upo hatujaambiwa-atleast hapa Jamvini. Anachokisema FMES humu ni kwamba kama kuna mwenye evidence basi azimwage humu, hata kama CCM ni mafia lakini wananchi ndo wataamua.

Wakuu hakuna asiyeijua CCM ni mafia wa siasa na katika siasa back deals ni kawaida kwa hiyo maswala ya akina Kamara kumuita kijana na kumwambia atoke Chadema au JK kuongea naye..hizo ni back deals ambazo Masanilo na Masanja au Lunyungu we can do nothing about.

Cha muhimu Ingebidi CHADEMA wajipange kabla ya kuileta issue hii.... wangemwaga data mapema mno..ili kuwanyima CCM kufanya manuevre. Lakini sasa inavoonekana ni kwamba tunalalamikia majina tuu Rwegasira vs Mukasa. Hili ni non issue. Cha muhimu wanaohoji huo uraia wangekuja na details kuonyesha ni kwa nini Mukasa sio Rwegasira. Period.

Harafu wakuu...tuwe makini na siasa zetu za kibongo..hivi kuna anayeamini kwamba CCM ingeamua kumpitisha Mukasa na sio Rwegasira ingeshindwa? Ninachoona hapa Chadema wanapoteza mda na kama issue hii ni legit basi political strategist wao ni vema warudi nyuma waanze upya.

Mimi huyo Mukasa simjui na hapa jamvini ndo nimemsikia kwa mara ya kwanza..ila naomba jamaa asihukumiwe simply because jamaa anajina linalofanana na waganda sijui wanyarwanda ambao hatukubaliani nao (maneno ya Lunyungu haya#post 204). Anaweza kuitwa Mukasa lakini akawa na msaada kwa nchi hii kuliko Masanja raia wa Kwimba.
 
Karibu tena Dr. W Slaa, Vp unaweza kutupa ufafanuzi au ushahidi wa kwa nini huyu jamaa amewekewa pingamizi kuhusu uraia wake?
 

Mkuu Masanja mbona data zimewekwa?

Kwamba Mukasa Osacar aliyebatizwa juzi Rwegasira, hakuzaliwa nchini, alizaliwa mwaka 70 huko Uganda na akaja na wazazi wake mwaka 71.

Na hakuna inapo onyesha aliomba uraia au kukana uraia wa wazazi wake ili awe mtanzania!
Wanao tetea CCM wanadai tu babayake alifanya kazi nchini hadi akawa ofisa wa juu muda mrefu lakini hiyo haibatilishi kwamba Oscar hakuzaliwa nchini, na hajawi kula kiapo!
Ila tunajua chini wa mafya wa CCM viapo vilisha chorongwa na ndo kigugumizi hiki tusubili kesho kuletewa hivyo viapo!


But well dont undermine walio lalamika, labda wanasubili vizibiti feki vitoke ili wamkome nyani giledi!
 
Last edited:

Why are we elevating this guy that much?????? Ina maana huko Biharamulo hakuna watu mpaka huyu kijana atafutwe na pia kuitwa na mkulu akagombee????? Na well, ina maana hata hayo matokeo ya kura za maoni za CCM kuna uwezekano yalipikwa ili kulinda pendekezo la mkulu? Hiyo kama ni kweli basi wanabiharamulo na especially CCM -Biharamulo poleni sana!
 


CCM huwa hawataki data ila kuonyesha kwamba wao ni CCM wanaweza kubisha huku wanapita mlango wa gizani ndiyo zao hawa wandugu utaomba data utatoa data hawachukui hatua.Kama unabisha sema data ngapi hadi leo za RA ziko nje na bado wameuchuna ?
 


mzee application of logic sequences in Tanzanian politics will always prove to be an exercise in futility!
 
FMES mbona hii umeivali njuga hii kitu kuna siri unaijua ambayo sasa unaogopa itatoka nje ? Si kawaida yako mkuu kukaza buti namna hebu butafute sirini kwanza tuseme maana niko Bukoba nikupe yaliyopo hapa.

Sidhani kama anavalia njuga, naamini anachofanya ni kuturudisha kwenye mstari wa kufikiri kwa undani na kwa kina. Vinginevyo tunaweza kujikuta tunaburuzana.
 

"uelewavyo" Rostam alizaliwa Tabora wapi na lini na wazazi wake walizaliwa Tanganyika mwaka gani na walifariki lini?
 
FMES mbona hii umeivali njuga hii kitu kuna siri unaijua ambayo sasa unaogopa itatoka nje ? Si kawaida yako mkuu kukaza buti namna hebu butafute sirini kwanza tuseme maana niko Bukoba nikupe yaliyopo hapa.

- Mkuu wangu heshima mbele sana, unajua kuna siku nilikutana uso kwa uso na mkurugenzi mmoja maarufu sana kwa kutajwa hapa JF, akaniambia anaipenda sana JF kwa sababu wale vijana tofauti na forums na media zote za Tanzania, kwa sababu wao hawawezi kukusulubu bila kukupa haki akasema ukiona wote wanakubaliana kuwa hufai, ina maana moja tu kwamba hufai that was big statement.

- Sasa Mkulu wangu sina lolote sijui chochote, isipokuwa kama kawaida ninasimamia haki, tunalaumiwa sana na forums zingine kwamba sisi ni tool ya Chadema, sasa ni ishu kama hizi ndio zinaweza kutusemea of what exactly we are, we are not all Chademas, this is demokrasia at work.

- Haya ni mapambano ya fikra, JF tunazo standards zetu ziko wazi, sasa leo nashangaa sana hata waheshimiwa sana humu wakitaka tuziweke sheria zetu pembeni ili either ku-get back to the CCM au kumkomoa Oscar sijui hasa what is the deal, hakuna anayejali wananchi Biharamulo kwenye hili wameachwa kwenye mataa, labda hili likiiisha ndio masikini wa Mungu watakumbukwa, Mkuu Lunyungu ni kusimamia principle tu sina lolote, ukiletwa ushahidi convincing hapa sitakuwa na tatizo kukubali kwamba Oscar ajitoe na CCM wachukuliwe hatua kali sana, lakini otherwise inasikitisha sana iwapo huyu Oscar ni raia wetu.

Otherwise, ninasema hivi Oscar na CCM wapewe nafasi ya kutoa maelezo kama sheria inavyosema.

NB: Ninakutwangia sasa hivi.

FMEs!
 
FMES said:
Otherwise, ninasema hivi Oscar na CCM wapewe nafasi ya kutoa maelezo kama sheria inavyosema.

FMES,

..huyu jamaa umedai humjui. vipi tena unamtambulisha kwa jina lake na kwanza "Oscar" kana kwamba mmeshibana, ni mpwa wako, au ni mwanao wa kumzaa?

..muite tu OSCAR RWEGASIRA jina lake la kubatizwa na Kamati Kuu ya CCM.
 
- Kwenye hili mkuu you are very right, kwamba ni waste of time ku-logic siasa za bongo.

Respect.

FMEs!

Sasa mkuu ni vigezo gani ambavyo atavileta vya kuthibitisha uraia?? mimi mwenyewe cheti cha kuzaliwa nimekipata nilipotaka kujiunga na chuo kikuu na tena eti kithibitisho ni kupeleka living certificate ya form 4.

Hapa nataka kusema ni vigumu kuthibitisha kwamba si mtanzania ama sio Lakini hata kama sio mimi ,nafikiri 28 years alizoishi TZ tayari ni qualification isiyopingika kuwa jamaa ni Mtanzania.
 
FMES,

..huyu jamaa umedai humjui. vipi tena unamtambulisha kwa jina lake na kwanza "Oscar" kana kwamba mmeshibana, ni mpwa wako, au ni mwanao wa kumzaa?

..muite tu OSCAR RWEGASIRA jina lake la kubatizwa na Kamati Kuu ya CCM.


- Kama nilivyosema kule nyuma furaha yako ni kugonganisha vichwa watu hapa JF, it makes your day mkuu tunajaribu kuchambua a very serious ishu ya taifa can you for once be serious please?

- Yaani unasema mimi ninamuita Oscar tofauti na wewe unavyoniita FMEs? Yaani wewe mpwa wangu, mwanangu au umeshibana na mimi is that so?

Respect.

FMEs!
 
FMES,

..huyu jamaa umedai humjui. vipi tena unamtambulisha kwa jina lake na kwanza "Oscar" kana kwamba mmeshibana, ni mpwa wako, au ni mwanao wa kumzaa?

..muite tu OSCAR RWEGASIRA jina lake la kubatizwa na Kamati Kuu ya CCM.

Lakini kama amebadilisha jina inamaana vyeti vyake vyote havitasharabiana na jina jipya ina maana mtu huyu atakuwa hana elimu labda kama ali badirishia mahakamani.Na nafikiri ni move nzuri na inayopendeza kuanza kuhoji elimu yake na vyeti vyake,hapo ubishi utakwisha .
 
unasema mimi ninamuita Oscar tofauti na wewe unavyoniita FMEs? Yaani wewe mpwa wangu, mwanangu au umeshibana na mimi is that so?

Kamanda unavijembe kweli kweli!!! Panga kwa Panga siyo...
 

- Mkuu sijui sheria zetu za uraia zinasema nini, ila common sense ninataka kuamini itakuwa kwa yeye kujibu kwanza kwa NEC kwa ajili ya initial pingamizi la Chadema, kama wanaomtuhumu hawaridhiki basi itabidi kwenda kwenye sheria either Uhamiaji au mahakama, lakini in the process lazima uhamiaji wawe involved, hii ni beneficiary kwa taifa zima,

- Halafu ni vyema pia tukazipitia kesi za nyuma za viongozi na uraia wao, kama Idd Simba, na Ntagazwa tukajua the charges na verdict, zinaweza kutusaidia yaani in the meantime what is next na to expect!

Respect.

FMEs!
 
FMES,

..sasa hili jina MUKASA lina matatizo gani.

..huyu kijana ametumia jina hilo toka shule ya msingi,sekondari, chuo kikuu, mpaka PhD.

..inawezekana hata kadi ya CCM alikata kwa kutumia jina Oscar Mukasa.

..almost kila alicho-achieve and what i believe made him a viable candidate kimetokana na jina Oscar Mukasa.

..sasa ghafla bina vuu anakuja na jina lingine.

..suala la huyu kijana kubadilishwa jina linahitaji maelezo toka kwa Chama chake na yeye mwenyewe.
 
 
Kwa upande wangu sijui lolote kuhusu Oscar zaidi ya kinachosemwa. Kabla ya kusikia juu ya pingamizi la Chadema jina la Mukasa tu lilinidokeza kwa namna fulani kuwa huyo ndugu ana uhusiano na Uganda. Siikuwa na matatizo ya uraia wake kwani Mtu wa Uganda anaweza kuhamia Tanzania na akawa raia wa Tanzania.

Kama vile watu waliotoka Nyasa na wako Tanzania na ambao majina yao tunayajua ni ya Kichewa kina (Banda, n.k) na wapo ambao wametoka Uarabuni au asili yao ni uarabuni na ukakuta majina yao mengi tu Zenji, Dar, Tanga n.k So, kuwa na jina la "Mukasa" siyo sababu ya kusema si raia wala sababu ya kushuku kuwa si raia.

Tatizo:
a. Kwamba kulikuwa na mjadala wa jina la "Mukasa" kunamfanya mtu aulize "kwanini" ukizingatia hayo niliyoyasema hapo juu. CCM au Oscar mwenyewe hakuwa na sababu yoyote ya kukana jina lake isipokuwa kama hakutaka watu wahusishe na "kitu fulani" yaani Uganda.

b. W/alipoamua kutumia jina la Rwegasira ambalo kwa Watanzania wengine linawakubusha ya kina "Paul Rwegasira" na wahaya waliowazoea Oscar amefanywa awe na jina la "kitanzania", it begs the question "why"? Ukifirikia sana hakuna jina la Kitanzania per se, kwani "Patel, Dewji, Nyoni/Nyuni, Simba, Tembo, n.k" ni majina ambayo unaweza kuyakuta nchi nyingine vile vile lakini yanatumiwa na watanzania. Kwanini hili la Oscar libadilishwe? Isipokuwa pale penye ishara ya matatizo?

Ninaamini waliovurunda hili siyo Chadema kwa kuchallenge uraia wa Oscar bali CCM kwa kuufanya uwe issue. Kama Chadema wana info zile zile ambazo CCM ziliwafanya waone kutumia "Mukasa" ni kukaribisha udadisi usio wa lazima kwanini wasihoji?

Hivyo utaona kuwa kama Oscar yuko (na inaonekeana hivyo) comfortable na jina lake kama Mtanzania na hakuna chochote cha kuficha asione haya aseme "Kutumia jina langu la Rwegasira naona kumezua maneno mengi, na nimeamua kutumia jina langu la kawaida la Mukasa, kwani mimi ni Mtanzania na sina hofu na asili yangu". Na kuanzia hapo hayo ya Rwegasira wayarudishe huko huko kwenye vikao vyao na Oscar aendelee kuwa Oscar Mukasa kama anavyo/alivyo fahamika kwa wengi.

Inasikitisha kuwa CCM kwa kuamua kumbadili Oscar Mukasa kuwa Oscar Rwegasira wamekaribisha wenyewe utafiti katika maisha ya kijana huyu na hivyo kututoa kwenye kuangalia ni nani anafaa kuwa mbunge wa Biharamulo.

Hata hivyo, kama kuna sababu ya msingi ya kuhoji uraia wake (kama ilivyodokezwa na CCM katika kubadilisha majina) ni haki ya kila Mtanzania kuona sheria inafuatwa. Kama tumeweza kuhoji uraia wa Rostam tuweze kutumia hilo hilo katika kuhoji uraia wa mtu mwingine yoyote pale inapotokea sababu ya msingi (kama mtu kutaka kuwa muwakilishi wa watu).

Tatizo kubwa ni kuwa bila kumaliza huu mjadala, itakuwa ni yale yale ya RA ambapo tangu alipoibuka 1994 akiwa kijana wa kama miaka 25 maswali yameendelea kuulizwa juu ya uraia wake na hayajakoma. Sitaki Oscar ajikute anahojiwa tena juu ya uraia 2010 au huko mbeleni endapo maswali ya msingi hayatojibiwa.

Tunaposema sheria ni kipofu maana yake ni hiyo. Haiangalii mtu ana utajiri kiasi gani, amesoma kiasi gani, amefanya vitu gani n.k swali ni JE AMEFUATA SHERIA? Wenzetu katika hili wanajitahidi sana ndio mwaana hapa in the "D" wamemfunga Meya wao jela, na sehemu nyingine wamewatia pingu wabunge wao (maseneta na wawakiilishi) bila kuwaonea haya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…