Mimi nashangaa kuwa mpaka karne hii bado wanaume tunang'angania hali ya msichana kuwa bikira bila kuangalia nyakati tunazokwenda nazo. Kuna zama bikira ilikuwa kitu cha thamani kiutamaduni, wakati ule ambapo bado idadi ya watu ilikuwa ndogo na hivyo hata michanganyiko ya tamaduni tafauti ilikuwa hafifu. Lakini kwa zama tulizonazo, ambapo kwanza imethibitishwa kuwa msichana anaweza kupoteza bikira bila ya kuingiliwa au asizaliwe nayo kabisa, kumhukumu msichana kama huyu kuwa si bikira ni kumwonea. Vivyo hivyo kumzawadia/kumthamini mwenye bikira ya kununua ni uzumbukuku. Mwisho wa habari, msichana anaweza kutunza bikira kwa miaka, lakini kuondolewa ni suala la sekunde tu. Baada ya hiyo furaha ya sekunde chache, maisha yanaendelea.
Ninathamini tamaduni za jamii zetu, lakini nahisi tumefika pahala tuangalie sifa nyengine kwa wasichana na sio ubikira tu. Na zaidi, na zaidi, la muhimu sana, TUSIWACHE KUPIMA KABLA YA NDOA na kwa wale wanaorukaruka, ninawashauri WASISAHAU KUFANYA NGONO SALAMA.