Bikira wa kisukuma alitoa jumbe za moto sana kuhusu uchumi

D Metakelfin

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2017
Posts
3,399
Reaction score
3,666
Ndo mana namkumbuka Bikira wa KISUKUMA Kwa hizi Jumbe zake.
RIP Bro [HASHTAG]#RIPSeth[/HASHTAG]

[HASHTAG]#Repost[/HASHTAG] @bikira_wa_kisukuma .

Laki tano, Mshahara wa Ma-Teller wa Benki hapa mjini Laki Tano, Bei ya TECNO PHANTOM mpya kabisa kwa kujishaua Snapchat na Istagram
Laki Tano, Bajeti ya Mafuta ya SUBARU mwezi Mzima.
Laki Tano , Bajeti ya HEINEKEN 100 KWA wanywaji wa Pombe.HELA FLANI MBUZI TU ambayo wengi wanaona HAINA ISHU.
.

Lakini , Laki Tano hii ina uwezo wa kukodi shamba Ekari 13 pale Kiteto au Mpwapwa na ikakutengenezea Million 15 baada ya Miezi MITATU kwa kulima Matikiti maji. Laki Tano hii hii ina uwezo wa kununua SIMTANK la lita 5000 ( ndoo 250 za lita 20) ambal inaweza kutumika kusolve shida ya maji mtaani kwako kwa kuuza ndoo 1 Sh 500 na ukaingiza 125,000 kwa kila SIMTANK unalouza.
.

Laki tano hii hii inaweza kulima Ekari 2 za Maharage pale Simanjiro na baada ya Miezi Minne ukavuna si chini ya Million 3 ambazo zitaexpand kilimo chako MARA 6 zaidi ya Mwanzo na Kuexpand Kipato chako mara 6 zaidi ya Mkupuo wa kwanza!
Laki Tano hii ina uwezo wa kulima Matikiti Maji Ekari 2 na zikakupa si chini ya Milion 2 na nusu baada ya SIKU 90!.
.

SHIDA NI: Kila mtu anataka akae mjini AONEKANE SAMAKI SAMAKI, aonekane Muvi Mlimani City, Apige Snapchat akiwa 777
MDADA yupo radhi aishi mjini kwa kuuza mwili wake kuliko kwenda Ruaha Mbuyuni Kuinvest kulima Vitunguu... Ataonyesha saa ngapi CROP TOP yake Mpya kutoka YAHYA BOUTIQUE? Sistaduu alime vitunguu?? Hapana, bora atafute Danga la Laki 2 akalale nalo!!
Big Up kwa wadada wote wajanja WALIOINVEST KWENYE KILIMO,kila Jumamosi wakati wewe unaona sifa kwenda HIGH SPIRIT LOUNGE Wadada wenzako wako RUVU wamekodi mashamba wanalima mpunga, unashangaa Huyu mdada anafanya nini kumbe mwenzio analima.

KUDOS kwa wanaume wenzangu ambao wamegundua siri kwamba kuuza Sura hakulipi ma wameinvest Shamba, kila weekend wanapotea kwenda kusimamia nyanya na pilipili Bagamoyo.
Utaendelea kuwashangaa wenzio wanatajirika na kudhani kila mtu anauza UNGA hapa mjini, Kilimo ndio unga mpya... Unadhani @mkandamizaj amenuunua ile BMW X6 kwa Episode za ORIJINO COMEDY? Thubutu, nenda MBARALI umkute amejaa Matope.....Huu ujumbe aliuandika miaka kadhaa iliyopita..

[HASHTAG]#RIPBro[/HASHTAG] [HASHTAG]#PumzikaKwaAmani[/HASHTAG]
[HASHTAG]#YourArticlesWillRemain[/HASHTAG]

sent from posta
 
Vitu vingi alivyokuwa anavisema vilikuwa havitekelezeki hapo in short mipango sio matumizi

Sent from my IPhone-7 using JamiiForums mobile app
 
Hapo kwenye simtank maji unapewa bure ? unasambaza bure ? Ujumbe mzuri ila tusitumie nadharia sana

Sent from my iPhone6 using JamiiForums mobile app
 
marehemu alikua analima mashamba makubwa ya viazi...mc wa sherehe...mhamasishaji na muelimishaji pia alitarajia kutoa kitabu chake cha shule bila ada..mtangazaji
inshort.. mtafutaji kwelikweli..
mcheshi hswaa..mara ya kwanza nlikuta threas inuongelea huku kumuhusu yeye..nkaanza kupata image atakuwa mtu ajabuajabu..lakini nlipomtafuta na luona page yake insta..wallah sikujutia.nkawa namsoma kila siku

Pumzika kwa amani seth!
 
Namkumbuka Kaka Yangu SETH 'Bikira wa Kisukuma' kwa haya aliyowahi kuyaandika.

[HASHTAG]#Repost[/HASHTAG] @bikira_wa_kisukuma (@get_repost)
・・・
#28/April/2016
SHULE BILA ADA:
Sa11 Kila Siku unakurupuka kuwahi barabarani kutoka huko BONYOKWA unakoishi,ili uwahi Posta Mpya Ulikoajiriwa...
Wewe ni Msomi mwenye Digrii,na Ulipata GPA 4.6 ukiwa unajua GPA ni dili lakini ulizunguka 2YEARS bila kazi mpaka ulipodaka Kibarua hiki cha Benki ukiwa kama LOAN OFFICER,na wakakupa Mshahara wao wa 750,000 Kwa Mwezi...Baada ya Mwaka Mmoja ukajihisi UNA HADHI huna haja ya kurukia Daladala kama wengine,ukajibandika KAMKOPO KA PASSO ambako unakatwa LAKI4 Kila Mwezi na unabakiza 350,000 inayoenda Mfukoni kila Muamala Ukisoma...
.

Pale Chini ya Ghorofa la Ofisi unakofanya kazi yuko Kijana,Mchafu Mchafu,ANAOSHA MAGARI,na kila "MABOSI" mkifika wote mnamuachia Funguo za Magari yenu ya Mikopo Awaoshee...Mtaji wake ni KOPO LA FUNGUO,SABUNI,na MAJI anayochota kwenye Kimtaro karibu tu na mnakopaki gari zenu..
KWA SIKU anaosha MAGARI 30,ya Mabosi Nyinyi kwa Shilingi 3000 kwa Kila Gari...Anakula Wali Maharage Kibandani kwa Sh 800 tu wakati WEWE na "HADHI YAKO" unaenda kula YMCA Canteen,IFM Restaurant au KFC,ili Kulinda Hadhi ambayo Actually HUNA!.
.

Mshahara ukitoka,wewe una 350,000 Mfukoni,ila Kijana huyu Mchafu Mchafu anayekula kwa Mahesabu,ambaye sometimes kwa kuona ANA HALI NGUMU huwa unamuachia hata CHENJI imsaidie,Anatengeneza Sh 3000x Magari 30 x Siku 30 =2,700,000(Milioni Mbili na Laki Saba Kwa Mwezi,NON TAXABLE!
Tai Kubwa,Viatu Vimeenda Upande,Mkopo wa Gari,HELA HAITOSHI,ila TITLE KUBWAAAA Ofisini unazunguka kwenye Kiti,Kila Siku una STRESS na unashangaa huyu kijana ANASMILE KILA SAA na Kukusalimu "Shkamoo Bosi" na unajiuliza Huyu Maskini Mbona Ana Raha Kila Siku na Mimi Majanga??.
.

NANI MASKINI KATI YENU???
NANI BOSI WA KWELI???
Wake Up Brother/Sister,Find a Plan B for Your Life,Huwezi Kuwa Mjinga Milele na Ukaamua Kutulia tu...Unalipwa Laki 4 DSM Hii,HUJALA,HUJALIPA KODI,HUJANUNUA UMEME,HUJAHONGA,HUJAZUNGUSHA RAUNDI ZA BIA,na HUNA KIPATO KINGINE ZAIDI YA AJIRA lakini Unahisi UKO SAWA TU,Nenda kapimwe Utaahira!
Dear Loan Officer,You need Another Loan to Buy BRAINS!

[HASHTAG]#RIPBro[/HASHTAG] [HASHTAG]#TheShuleBook[/HASHTAG]

sent from posta
 
Mara nyingi mipango ya kwenye makaratasi huwa huwa haishindwi. That is rehearsal and not a performance!! Jaribu uone.

Sent from my TECNO M3 using JamiiForums mobile app
 
Yeye mwenyewe muandishi kafa akiwa ameajiriwa. Sijui ndio nn. Maandiko sio reality
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…