maganjwa
JF-Expert Member
- Sep 11, 2012
- 2,800
- 2,339
Habari wakuu.
Mimi nimetafakari sana kuhusu jinsi mambo yanavyokwenda hapa kwetu. Yaani unaweza kupata hasira hawa jamaa hatua waliyofikia ni mbaya sana.
Kwanza wamejua hawapendwi na uchaguzi bila kutumia nguvu ya dola hawashindi.
Pili wanawaza mambo ya kuwakomoa watu kuwalit uhuru awamu hii waliaanza na kuzuia bunge live, ikapitishwa sheria kali ya mitandao, kusikiliza simu za watu kuwatesa wanaowakosoa, watu kupotea bila maelezo na sasa kupandisha bei ya vifurushi na gharama utumiaji wa simu. Haya yote ni kwa faida ya nani au ukiangalia ni kwa maslahi ya nani? unashindwa kuelewa kwani haya yote.
Tatu ukija kwenye siasa wameharibu kabisa hakuna siasa safi badala yake wanawaza kusalia madarakani kwa gharama yoyote ile na kutengeneza vijana na kuwafundisha ugaidi na kuwaaminisha kuwa wapinzani eti siyo wazalendo. Uzalendo ndugu zangu siyo kuisifia serikali na viongozi wake hilo ni lazima ijulikane. Sasa vijana wao wamevalishwa makofia yenye nembo ya chama kama maaskari fulani na wanajiona nao maaskari kila kiongozi wa CCM utaona kuna kijana yuko nyuma yake. Hii ni ajabu sana na wameachwa kwa muda sasa.
Nne ukwapuaji wa fedha za umma kwa hawa jamaa ni jadi yao. Wanalindana hawawezi wajibishana kwa kuwa huo ndo jadi yao wamefikia hatua mbaya kwa sasa wanaamini hela inaweza kufanya kila kitu mtu wa ccm huwa hajiandai kwa hoja anajiandaa kwa hela na wameharibu nchi kuwaaminisha watu wakati wa uchaguzi watu wanasema huu ni wakati wetu kula. Utamaduni mbaya sana
Kuendelea chama hiki kutawala ni kuendelea kudidimiza taifa tangu uhuru mpaka leo tuna hali mbaya ni aibu sana umaskini unawaandama watu. Hakuna mpango wa poverty reduction
Ebu tujadiliane ila haya ni maoni yangu shida kubwa sana kwangu mimi ni hiki chama siku ikiondoka madarakani tunaweza pata direction mpya