Bila dini kusingekuwa na amani na haki na ustawi mzuri wa jamii!

Bila dini kusingekuwa na amani na haki na ustawi mzuri wa jamii!

natambua kuwepo na magomvi mbalimbali kwa sababu ya dini tofauti na hata wafuasi wa dini moja kupambana. lakini kusingekuwapo na dini kabisa, haka ka amani na ka haki kadogo na ustawi na maendeleo ya jamii visingekuwepo kabisa. kwani dini zimeleta yafuatayo:
1. zinafundisha upendo, umoja, amani na haki
2. zinajenga taasisi kama shule, hospitali na viwanja vya michezo. na hapa wengi tumefaidika sana.
3. zimesaidia kutatua migogoro mbalimbali
4. zinafundisha maadili mema na kukemea maovu.
Naamini bila dini tungeuana sana na tungeishi ktk mazingira hatari kuliko ilivyo sasa. asante Mungu kwa dini. swali? Dini ipi ya kweli? kila mtu atatetea ya kwake. cha kufanya ishi kadiri ya dhamiri yako na usipuuze nini dini ya mwenzako inasema, bali tafakari na yaliyo mema yachukue. ila jiamini na tenda unachoamini ni haki na chema. yapo mambo ambayo kwa akili na sheria ya asili(natural law)aliyotupa Mungu tunaweza kuyajua juu ya uhalali wake. watu wa dini tofauti tuvumiliane. atakayeshindwa kumvumilia mwenzie na kumjeruhi ndiye atakayemchukiza Muumba. Asanteni

SINA DINI WALA IMANI KATIKA IMAGINARY BEING AND AM HAPPY!

Karibu katika ulimwengu huru!!

..........Freee ideas.....
 
SINA DINI WALA IMANI KATIKA IMAGINARY BEING AND AM HAPPY!

Karibu katika ulimwengu huru!!

..........Freee ideas.....
dini ni uhusiano kati ya mtu na Mungu. je wewe huamini uwepo wa Mungu?
 
Kinacholeta amani na
Asilimia kubwa ya watu wanaogopa sheria sio imani au Mungu, watu wanahofu kufungwa kunyongwa kupigwa risasi kuchomwa moto n.k ndio maana hata wezi humuomba Mungu wanapokwenda kuiba.
Kinacholeta amani na utulivu ni uwepo wa dola na Serikali. Sio dini.
 
Kinacholeta amani na

Kinacholeta amani na utulivu ni uwepo wa dola na Serikali. Sio dini.
dola na serikali vina mchango ila dini ni zaidi. pia nawakumbusha uzi unaongelea na mambo ya ustawi wa jamii hasa maeneo ya hospitali, shule, michezo
 
angalia michango ya dini ktk nyanja hizi:
1. Hospitali za BUGANDO, KCMC, KIBOSHO, HINDU MANDAL, AGHAKAN, BILAL MUSLIM AGENCY HOSP. n.k
2. Vyuo: SAUT, MAKUMIRA, MWENGE, TUMAINI, JORDAN, MUSLIM UNIV. OF MORO n.k huku kote kwa uchache ni mkono mrefu na mpana wa dini. watu wakielimika na kuwa na afya nzuri ya mwili na akili wanakuwa na amani. jamani hatuoni hayo?
 
dini ni uhusiano kati ya mtu na Mungu. je wewe huamini uwepo wa Mungu?

MUNGU,SHETANI,ROHO,PEPO NA VITUBKAMA HIVYO NI NADHARIA TU SIO VITU HALISI .KIUFUPU HAKUNA MUNGU WALA SHETANI

Karibu katika ulimwengu huru

.... Free ideas...
 
MUNGU,SHETANI,ROHO,PEPO NA VITUBKAMA HIVYO NI NADHARIA TU SIO VITU HALISI .KIUFUPU HAKUNA MUNGU WALA SHETANI

Karibu katika ulimwengu huru

.... Free ideas...
swali kwako: binadamu tumeletwa na nini au nani? na miti na viumbe vyote nini kimevileta au nani kavileta?
 
Inaonekana we ni mgeni sana hapa Jf.Karibu sana ndugu haya mambo yote tumeshajadili!.

Kwa ufupi! Sana ,We are the product of nature!

Karibu sana katika ulimwengu huru
.....Free ideas....
 
Inaonekana we ni mgeni sana hapa Jf.Karibu sana ndugu haya mambo yote tumeshajadili!.

Kwa ufupi! Sana ,We are the product of nature!

Karibu sana katika ulimwengu huru
.....Free ideas....
mjadala haujafungwa! hiyo nature inayoproduce binadamu, miti n.k ndo ambayo wenzako tunaiita Mungu na hata majina mbalimbali yanatumika. kwa kifupi hakuna kiumbe au kitu chenye uwezo wa kujianzisha chenyewe vimeletwa na kitu kingine chenye nguvu kuliko vyote ambacho chenyewr hakianzishwi na chochote. hicho kitu ndo Mungu. wengine wanamwita.Mungu ALLAH. ndugu Mungu yupo! ndo huyo we unamwita Nature!
 
Back
Top Bottom