Bila dini sisi Waafrika tusingeishi?

Bila dini sisi Waafrika tusingeishi?

Saad30

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2020
Posts
2,737
Reaction score
5,464
Habari wakuu.

Nimeekaa na kuwaza na kuwazua hizi dini zimeletwa tumuogope MUNGU au tumpende MUNGU?

Miaka ya tangu na tangu kulikuwa hakuna dini ila tuliamini kwamba kuna mbaye anaongoza hii dunia na vilinyo ndani yake.Tulitumia miti shamba kupona maradhi.

Je ,Mababu zetu na mabibi zetu hawakuona ubaya wa kuwapokea hivi viumbe vya kizungu?

Ona mashekhe na mapadri wanaishi maisha mazuri ya kujidai na familia yao kwajili ya sadaka zetu.

Kwanini sisi wenyewe tukiomba bila hizo dini kwa MUNGU mmoja hatuwezi kufanikiwa?

Hawa jamaa wametumia kufuli gani la kutufunga akili hadi mkristo akisemwa Yesu anakasirika sana na vilevile mwislamu akisemwa Mtume Muhammad anakasirika....kuna siri gani wametuwekea kwenye mioyo yetu.

Mama anadiliki kuuza shamba akatoe sadaka...alafu badae anaenda kukodishwa tena hilo shamba kwajili ya kujipatia kipato cha kulisha familia.

Viongozi hao wa dini wanajenga mahoteli na kisha waaenda wazee wa kuzini walevi na kadhalika....mbaya zaidi hawataki wajulikane kwamba wao ndio wamiliki wa hizo hotel.

Asee tunapigwa sana pesa na hawa jamaa..

Kwani tukiomba kwajina la MUNGU mmoja kuna shida gani?

NB: Napenda kuelekezwa kama nimekosea.
 
Mungu hana dini wala kanisa.

Ni wajanja wachache kwa maslahi yao binafsi walianzisha dini, ku control binadamu.

Religion is a crowd control, Spirituality is the personal relationship with the Divine.

Huitaji kuwa na dini au kanisa kumjua Mungu...

Sasa waafrika walisha potoshwa wanadhani Mungu yupo kanisani na kwenye dini zao tu.

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Nchi zilizo na Wakristo, zimejaa Uzandiki na Ufisadi, na Ubadirifu wa hela.

Kumbuka, Nchi hizi haziko Afrika peke yake.

Walakin, utakuta hayo ndio yanayosingiziwa kuanzia Afrika.
Vile vile, Hayo hayatokei bila ya kuwa na mfumo wa aina fulani.
 
Nimeekaa na kuwaza na kuwazua hizi dini zimeletwa tumuogop
Ukiwa huna akili unafundishwa kumuogopa Mungu, ila ukiwa na akili zinachaji utajifunzaga kumpenda Mungu.

Ni kama hatua za ukuaji wa mtoto; akiwa mdogo atamuogopa baba na akikua atajifunza kumpenda.

Kupenda hakuanzi mpaka utashi ukomae, maana bila utashi haiwezekani kupenda.
 
Habari wakuu.

Nimeekaa na kuwaza na kuwazua hizi dini zimeletwa tumuogope MUNGU au tumpende MUNGU?

Hapo una maana Ya Islam Na Ukristo.
Miaka ya tangu na tangu kulikuwa hakuna dini ila tuliamini kwamba kuna mbaye anaongoza hii dunia na vilinyo ndani yake.Tulitumia miti shamba kupona maradhi.

....umeshuka, halafu ukaleta Unyanyasaji.....Kutumia miti shamba kuponyesha maradhi na Mungu wapi na Wapi
Je ,Mababu zetu na mabibi zetu hawakuona ubaya wa kuwapokea hivi viumbe vya kizungu?
Kwanini waone Vibaya? Hao mabibi na mababu zetu walikuwa wakifanya Biashara nao toka enzi na Enzi na Hao Mashetani.

...kejeli, na Matusi ' Ati Viumbe' what a bigoted statement!
Ona mashekhe na mapadri wanaishi maisha mazuri ya kujidai na familia yao kwajili ya sadaka zetu.
Sadaka za nani? Wazungu na Waarabu au Sadaka za Waafrika.... Kejeli nyingine hapo
Kwanini sisi wenyewe tukiomba bila hizo dini kwa MUNGU mmoja hatuwezi kufanikiwa?
WtF. Una maana ya kuomba kitu gani hapo? Kufanikisha lipi?
Hawa jamaa wametumia kufuli gani la kutufunga akili hadi mkristo akisemwa Yesu anakasirika sana na vilevile mwislamu akisemwa Mtume Muhammad anakasirika....kuna siri gani wametuwekea kwenye mioyo yetu.
Sijawahi Kusikia "Yesu atakasirika" au Muhammad anakasirika....umejiuliza ni kinyongo gani umewekewa wewe kwenye roho yako kuandika uwongo huo?
Mama anadiliki kuuza shamba akatoe sadaka...alafu badae anaenda kukodishwa tena hilo shamba kwajili ya kujipatia kipato cha kulisha familia.
Unadhalilisha, unaleta fedheha. Hiyo ni Lugha chafu ya Ukimbari....
Viongozi hao wa dini wanajenga mahoteli na kisha waaenda wazee wa kuzini walevi na kadhalika....mbaya zaidi hawataki wajulikane kwamba wao ndio wamiliki wa hizo hotel.
Unachochea, Unafananisha hulka....Wanaozini ni kina nani? Walevi kina nani? Unajua kati ya Kristo na Muhammad walikuwa na kitu gani in common?
Asee tunapigwa sana pesa na hawa jamaa..

Unachochea, na Kufedhehesha hapo.
Kwani tukiomba kwajina la MUNGU mmoja kuna shida gani?
Mungu gani huyo? Yesu ni Mungu? Muhammad ni Mungu?

Au ndio yule Mzungu Mungu?
NB: Napenda kuelekezwa kama nimekosea.
Umekuja kutukana , na Unajua hayo.
 
Kumbuka dini zilikuja kama vitanhulizi vya ukolononi, ikisaidiana na kundi la wapelelezi na kundi la wafanyabiashara,jivyo si kila lililo katikadini au so kila dini ina manufaa, dini ulikuwa mpango wa kuwaandaa watu kutawaliwa bila kubisha. Hata sasa nia kubwa ya watawala ni hiyo.

Sent from my Infinix X693 using JamiiForums mobile app
 
Hapo una maana Ya Islam Na Ukristo.

....umeshuka, halafu ukaleta Unyanyasaji.....Kutumia miti shamba kuponyesha maradhi na Mungu wapi na Wapi

Kwanini waone Vibaya? Hao mabibi na mababu zetu walikuwa wakifanya Biashara nao toka enzi na Enzi na Hao Mashetani.

...kejeli, na Matusi ' Ati Viumbe' what a bigoted statement!

Sadaka za nani? Wazungu na Waarabu au Sadaka za Waafrika.... Kejeli nyingine hapo

WtF. Una maana ya kuomba kitu gani hapo? Kufanikisha lipi?

Sijawahi Kusikia "Yesu atakasirika" au Muhammad anakasirika....umejiuliza ni kinyongo gani umewekewa wewe kwenye roho yako kuandika uwongo huo?

Unadhalilisha, unaleta fedheha. Hiyo ni Lugha chafu ya Ukimbari....

Unachochea, Unafananisha hulka....Wanaozini ni kina nani? Walevi kina nani? Unajua kati ya Kristo na Muhammad walikuwa na kitu gani in common?

Unachochea, na Kufedhehesha hapo.

Mungu gani huyo? Yesu ni Mungu? Muhammad ni Mungu?

Au ndio yule Mzungu Mungu?

Umekuja kutukana , na Unajua hayo.
Acha makasiriko ya kudanganywa na mganga
 
Mungu hana dini wala kanisa.

Ni wajanja wachache kwa maslahi yao binafsi walianzisha dini, ku control binadamu.

Religion is a crowd control, Spirituality is the personal relationship with the Divine.

Huitaji kuwa na dini au kanisa kumjua Mungu...

Sasa waafrika walisha potoshwa wanadhani Mungu yupo kanisani na kwenye dini zao tu.

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
Ni kweli dini na madhehebu ni miradi ya watu , cha msingi ni kudumisha mahusiano yako na Mungu , imagine Yesu alimuokoa mwizi msalabani ambaye hakuwa na dini Ila mafarisayo wenye dini wengi waliachwa ..... Viongozi wa dini washageuza dini kuwa biashara
 
Kilichonishangaza, sanamu ya Yesu ni nyeupe ila la shetani ni nyeusi kama mkaa! Ni ishara gani hiyo? Ni kwa nini hatukuhoji? Ina maana watu weusi ndio mashetani? Ni ukoloni wa aina yake. Hakika imani nzuri ni Ile ya mababu zetu.
 
Kiuhalisia

Mzungu asingeweza kuendelea kuishi, Ilikuwa aangamie....angeangamia kwa uovu wake mwenyewe. Mzungu, hususani Mwingereza, Dhalimu mkubwa katika wazungu, alikuja gundua anahitaji baraka zote za Mungu. Kwani Vita yao, wenyewe kwa wenyewe ndio iliyosambaratisha Ulaya. Ndio ilikuwa chanzo kikuu cha kuanza kutubu baada ya miaka nenda rudi ya Udhalimu kwao Ulaya, India, na Kwingine.

Hata kanisani walikuwa hawaendi, na baada ya kuanza kuona laana iliyowapata wakaanza kuchanganyishana, kuchangisha hela hadi makanisani kuendeleza Udhalimu wao. Walikuwa masikini wa kutupwa, walevi, waesherati, wanafiki, wazandiki na mafisadi kuliko nchi nyingine Ulaya....Walitishana wenyewe kwa wenyewe.....Je wajua kwanini iliwachukua mda kupatana na Wanyonya Damu wakatoliki na Uovu wa Kanisa la Uingereza? Yaani kumtambua Papa?
 
Kilichonishangaza, sanamu ya Yesu ni nyeupe ila la shetani ni nyeusi kama mkaa! Ni ishara gani hiyo? Ni kwa nini hatukuhoji? Ina maana watu weusi ndio mashetani? Ni ukoloni wa aina yake. Hakika imani nzuri ni Ile ya mababu zetu.
Wapi hapo ulipoona hizo sanamu? na Hiyo Imani ya Mababu zetu ndio Ipi?
Nakuhoji sasa
 
Back
Top Bottom