Leo Lissu yupo Tabora Mjini, wakati huohuo kuna mtufuano unaendelea kati ya wana CCM wenyewe kwa wenyewe.
Upande mmoja ni CCM uongozi ambao umejiratibu kuanzia ngazi ya tawi hadi Mkoa, upande wa Pili ni Mh.Mkuu wa. Wilaya na Mgombea wake wa Ubunge Bwa. Mwakasaka ambaye wenye CCM yao wanadai DC alicheza rafu sana kudhofisha wagombea wengine ili Mwakasaka apite.
DC aliwatisha baadhi ya washindani wa Mwakasaka na kuwaambia apite asipite jina lake lazima lirudi.
Sasa kilichotokea jana cha Uongozi wa CCM kufanya press conference na baadae Mkuu wa Wilaya kuvamia mkutano na kuanza kuwafokea ni ushahidi kwamba hali sio shwari na inahitajika jitihada za haraka kabla mambo hayajaharibika.
Kila anachofanya DC na Mwakasaka wake, timu ile iliyohujumiwa inapinga na kutamani kuona wanashindwa. Upinzani wananufaika sana na huu mgogoro, siri za chama zinapelekwa upinzani bila gharama yoyote.
Wana CCM wanafanya kampeni kummaliza mwakasaka,wao wanaamini.kumuumiza Mwakasaka ni kumuumiza DC ambae amekuwa kero sio kwa wana CCM pekee, bali hata kwa watumishi na wananchi wa Tabora mjini.
Ushauri wangu kwa Dr. Bashiru, muondoeni haraka huyu DC ili chama kiondoe migawanyiko, chama kimepasuka kwasababu ya DC kukosa busara, Mwakasaka kwenye majukwaa anasema Tabora imejaa majungu, wananchi wa Tabora ni wanafiki sana, halafu huyohuyo anategemea kuwaomba kura watu wanafiki na waliojaa majungu (Maajabu)
Lissu leo wala asitumie nguvu nyingi kuomba kura za wanyamwezi, aelezee tu viparata na jinsi DC anavyonyanyasa watumishi na wana CCM wenyewe atakuwa kamaliza.