Bila furaha hakuna ubunifu wala mafanikio

Bila furaha hakuna ubunifu wala mafanikio

MoureenAbel

Member
Joined
Sep 24, 2021
Posts
29
Reaction score
43
Siku moja kundi la watu 50 walikuwa wakihudhuria semina moja.

Ghafla mwezeshaji akaacha kufundisha na kutoa zoezi ambalo walitakiwa kulifanya kwenye makundi aliyoyagawa.

Baada ya hapo akampa kila mtu puto na kumwambia alipulize lijae hewa na kuliandika jina lake kisha wakayakusanya na kuyaweka kwenye chumba kimoja.

Walipoyaweka kwenye kile chumba akawapa zoezi la pili kuwa kwa pamoja watumie dakika tano ambapo kila mtu awe amefanikiwa kulitafuta puto lenye jina lake.

Waliingia mle ndani kila mtu akawa busy akijaribu kulitafuta puto lake lakini hakuna aliyefanikiwa na dakika tano zaikaisha huku kila mtu akiwa hana puto mkononi.

Mwezeshaji akasema tena haya sasa kila mtu aingie na alichukue puto lolote na kumpa mwenye jina lake.

Wakaingia na haikufika hata dakika ya nne kila mtu akawa ameshapata puto lake na kakaa kwenye kiti chake.

Mwenzeshaji akawaambia hongereni sana, na huu mfano unaendana sana na maisha yetu ya kila siku, ambapo watu wako busy kuitafuta furaha katika maisha yao bila kujua furaha hiyo ipo wapi au wataipata wapi.

Furaha zetu zipo katika furaha za watu wenigne, wape furaha yao nawe utapata furaha yako.

Na hili ndilo kusudio na hitaji kuu la kila binadamu

Wewe unatafuta nini katika maisha?

Comment FURAHA na kisha share kama nawe waamini bila ya furaha hakuna mafanikio na ubunifu kwani mwili unakuwa katika hali ya unyonge na kusababisha kutokuwa na ujasiri wa kujituma.

Furaha inatakiwa sehemu zote: Nyumbani, kazini, mtaani, shuleni na kila sehemu katika maisha yetu

_MG_1223.jpg
 
Umwamba mwingi sana mkuu.. ubarikiwe
 
Duhhhhh.....
Huu mzigo kweli konki, uzi umeshiba huu...💪
 
𝐔𝐤𝐰𝐞𝐥𝐢 𝐤𝐮𝐭𝐨𝐤𝐚 𝐦𝐨𝐲𝐨𝐧𝐢 𝐦𝐞 𝐟𝐮𝐫𝐚𝐡𝐚 𝐲𝐚𝐧𝐠𝐮 𝐧𝐢 𝐬𝐢𝐤𝐮 𝐚𝐦𝐛𝐚𝐲𝐨 𝐧𝐢𝐭𝐚𝐩𝐚𝐭𝐚 𝐦𝐜𝐡𝐮𝐦𝐛𝐚 𝐰𝐚 𝐤𝐮𝐨𝐚 𝐧𝐢𝐦𝐮𝐨𝐞 𝐧𝐚 𝐭𝐮𝐩𝐚𝐭𝐞 𝐰𝐚𝐭𝐨𝐭𝐨, 𝐚𝐢𝐬𝐞𝐞 𝐈 𝐰𝐢𝐬𝐡 𝐚𝐭𝐚𝐤𝐚𝐲𝐞 𝐧𝐢𝐨𝐧𝐚 𝐬𝐢𝐤𝐮 𝐡𝐢𝐳𝐨, 𝐇𝐮𝐮 𝐧𝐢 𝐮𝐤𝐰𝐞𝐥𝐢 𝐤𝐮𝐭𝐨𝐤𝐚 𝐦𝐨𝐲𝐨𝐧𝐢 𝐧𝐚 𝐌𝐮𝐧𝐠𝐮 𝐚𝐧𝐚𝐣𝐮𝐰𝐚.
𝐀𝐜𝐡𝐚 𝐧𝐢𝐢𝐬𝐡𝐢𝐞 𝐡𝐚𝐩𝐚 𝐭𝐮🤔🤔🤔🤔
 
Ukweli mchungu ni kwamba kamwe na milele hutoweza kumfurahisha kila mtu.
Au itapelekea kuwa people pleaser na utakufa kwa disappointments sababu utakuwa unatumika na watu kukufanyia makusudi.
Huo mfano ni mdogo sana kucover uhalisia mkubwa wa maisha.

Furaha utaipata kutoka kwako tu, ndani kabisa.
 
Huu uzi wako nautumia kuanzia leo na hautojua utafanya niguse watu wangapi
 
Back
Top Bottom