Bila katiba mpya nzuri, wawekezaji watatukimbia!

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Bila katiba nzuri wafanyabiashara ambao mnakaa na kuona katiba haikuhusu unajidanganya kwa sababu hii hapa ya msingi.

1. Kwanza maandamano ya juzi sio kwamba serikali ilipenda bali umma umepata nguvu zaidi na viongozi wa upinzani wako serious sana.

2. Wamesema “watakinukisha” maana yake ni kwamba bila katiba mpya nchi haitaweza kuwa shwari. Hii haina maana ya fujo lakini maana yake ni kwamba malalamiko haitaisha, mikutano haitaisha, na maandamano hayataisha.

Kwa mazingira haya hakuna mwekezaji atataka kuja na kuwekeza kwa muda mrefu. Kwasababu wakiangalia nchi nyingine kubwa zote kama hazina demokrasia basi zina matatizo makubwa hasa kwenye ushwari. Ilianza Egypt, ikaja Sudan, ikaja Ethiophia, Kenya wamejiokoa na katiba nzuri ndiyo maana wapo powa, chini yetu kuna zambia na malawi ambazo zina demokrasia.

Hili linahusu kila mtu bila uwekezaji hakuna kodi bila kodi hakuna huduma muhimu na bila huduma hakuna usalama nchini. Hivyo kama unataka maendeleo, utulivu na unapenda nchi tumia muda huu kuunga mkono katiba mpya wakati ni mtaro kabla swala hili halijawa bahari.
 
Una hoja mkuu usikilizwe ingawa uandishi wako ni mbovu mno
 
Huwekezaji hauna maana kama wananchi hatuoni matunda ya uwekezaji. Deni la taifa linakuwa kila kukicha, maana yake tunakopa sana. Nchi hii yenye rasilimali nyingi asilia, na hazitusaidii wananchi uwekezaji ni ujinga.

Tungeacha kwanza swala la uwekezaji tuweke shera zetu ziwe ni zenye meno hasa.

Tufanye audit ya nini tunacho na kiasi gani kisha tuanze upya. Kwa mfumo uliopo, wanakimbia kila siku kukopa, pesa wanalipana wao.

Jiulize Mbunge na mawaziri pesa wanazolipwa kila mwezi, wakati wa vikao na baada ya kumaliza ubunge wao zinatoka wapi.

Unasikia kila siku wanatamba TRA imevunja record ya makusanyo, lakini Bajetu yetu tuna tegemea wahisani kwa asilimia 60 au 70. Deni la nchi linakuwa, licha ya kukua, bado huduma hatupati. Hospitali hazina dawa, na vitendanishi vingine.

Bado wanaofaidi ni watawala na matajiri walioupata utajiri kwa kutuibia.

Sioni haja wala sababu ya wawekezaji, wanawekeza wapi?Sisi tunafaidikaje na uwekezaji huo?

Utawasikia mara Royal tour, mara madini ,mara utalii, lakini Rais kila siku yuko nje kaenda kuomba.
 
Hujui kama hujui. Hebu jaribu kujielimisha kwa wanaojua hayo uliyoyaandika upewe ufafanuzi. Tatizo ni uelewa mdogo tu.
 
Back
Top Bottom