Bila kifo watu wasingeenda kanisani/msikitini

Bila kifo watu wasingeenda kanisani/msikitini

Ni kweli.

Siku nilipochoka kauli za kutishiana maisha ndio ikawa mwisho kuonekana nyumba za ibada.

Pata picha unaambiwa.

“Usipo swali/sali, we ni motoni tu” 🙁

Mara uambiwe,

“Siku ya mwisho ukiingia kaburini Kuna linyoka likubwa/ Nge atakugonga kichwani mara saba”

Wooooi, Ya niniii, ya niniiii mieee, nimeachaaa.

Namuomba Mungu wangu nyumbani, full stop.
 
Ndio hivyo,

Kwa sasa tunatia huruma kanisani na msikitini kwa kuwa hatujui baada ya kifo nini kinafuata.
Vitisho ni mbinu pekee ya Mungu.

Hana mbinu mbadala.

Mungu ameishiwa mbinu.
 
Ndio hivyo,

Kwa sasa tunatia huruma kanisani na msikitini kwa kuwa hatujui baada ya kifo nini kinafuata.

Mbona Chinese wanajua kifo kipo na hawaendi huko...?
 
Kifo pekee sio sababu maana hicho kipo tu,unataka au hutaki utakufa.
Shida ni kwamba huko kanisani ibada hazina logic,sasa ukiwa mtu wa kutafuta logic lazima utakata mguu kwenda huko!
 
Nadhani ishu ya kwenda kanisani au msikitini ni kutafuta heshima ya mazishi , kwamba kaswaliwa na sheikh ,au kasaliwa na padre, kaingizwa kanisani,au msikitini
Na ile ya huyu hakuwa wetu ,hatukua tukimuona ibadani

NB : kumbe wewe ni mchanga mungu mzuri kuliko wao kwa mungu wako ,, ila hukupenda milolongo yao
 
Back
Top Bottom