Bila kujirudi, Kassim Majaliwa atapigwa chini!

Bila kujirudi, Kassim Majaliwa atapigwa chini!

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Tanzania sasa inapitia wakati muhimu sana. Sasa hivi kuna watu wachache ndiyo wameshikilia fungua za amani na katiba ya nchi yetu. Watu hao ni Rais Samia, Kinana, Mbowe, Rais Mwinyi, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Lissu na Zitto. Hawa ndiyo watu muhimu kwenye Katiba yetu ijayo

Waziri Mkuu Majaliwa ana matatizo mawili makubwa

1. Kitendo cha kuengua mpinzani wake wa uchaguzi ili apite bila kupigwa inaonesha alikuwa anapenda ule mfumo na hii imemfanya kutokuaminika kabisa na wapinzani

2. Kitendo cha kukubali hadharani kwamba alikuwa anawatumia wakina Sabaya kule kwa Mbowe kumemwaribia sana.

Kwa mwenendo wa sasa Rais Samia pamoja na Mwinyi wanahitaji viongozi wa upinzani ili waweze kupeleka taifa mbele.

Waziri mkuu bila kutafuta njia ya kutubu na kusema wazi kabadilika itabidi atolewe kwa manufaa ya umma.

Hivyo anaweza kutafutia issue kama Spika Ndugai au tu Rais kufanya mabadiliko ya kawaida au anaweza kutubu na kujirudi kitu ambacho hajafanya mpapa sasa.

Mbowe kwa sasa ana nguvu kuliko Majaliwa. Na akiweka kichwa ngumu na kujifanya ni mzalendo yatamkuta ya Ndugai.

Namshauri awahi haraka sana kuweka msimamo wake wazi bila hivyo atapigwa chini kwani hatakuwa anasaidia nchi au chama
 
Yawezekana una hoja lakini umeandika zaidi kwa ushabiki wa kisiasa, hasa ulipowataja wasiokuwa kwenye uongozi Serikalini. Ungetaja, kwa ushahidi, kauli na matendo/mienendo yake inavyoathiri utendaji wa Serikali
 
Waziri Mkuu Majaliwa ana matatizo mawili makubwa

1. Kitendo cha kuengua mpinzani wake wa uchaguzi ili apite bila kupigwa inaonesha alikuwa anapenda ule mfumo na hii imemfanya kutokuaminika kabisa na wapinzani
Mkuu Kamundu , sio Waziri Mkuu aliyeengua bali wabunge waheshimiwa sana, wapinzani hujiengua ili wapite bila kupingwa, na hii ni kwa mawaziri wakuu wote na senior ministers kama Mwandosya.
2. Kitendo cha kukubali hadharani kwamba alikuwa anawatumia wakina Sabaya kule kwa Mbowe kumemwaribia sana.
Sii kweli, Sabaya alikuwa anatumiwa na the status quo yote.
Kwa mwenendo wa sasa Rais Samia pamoja na Mwinyi wanahitaji viongozi wa upinzani ili waweze kupeleka taifa mbele.
Sii kweli, ila imetokea tuu wote ni waungwana, JPM crushed the opposition and wiped it off na bado Tanzania ikapaa!.
Waziri mkuu bila kutafuta njia ya kutubu na kusema wazi kabadilika itabidi atolewe kwa manufaa ya umma.
Not necessarily, Tanzania viongozi wetu wapo at the pleasure of the president na sio kuwajibika kwa umma. Baada ya PM Majaliwa kusema alichokisema kumhusu JPM, and what happened thereafter, tungekuwa na utamaduni wa kuwajibika, he shouldn't be there by now!. Hivyo usimpangie Samia!.
Hivyo anaweza kutafutia issue kama Spika Ndugai au tu Rais kufanya mabadiliko ya kawaida au anaweza kutubu na kujirudi kitu ambacho hajafanya mpapa sasa.
Kwa vile hatuna utamaduni wa viongozi kutubu, hana sababu ya kutubu kwa yeyote, hata Spika JYN, kule kutubu ndiko kumeponza, angekauka tuu kwasababu rais hana mamlaka kumuondoa Spika, Jaji Mkuu au CAG!.
Mbowe kwa sasa ana nguvu kuliko Majaliwa. Na akiweka kichwa ngumu na kujifanya ni mzalendo yatamkuta ya Ndugai.
Hapa unachanganya nguvu ya powers, popularity, umaarufu na umashuhuri, Mbowe ana nguvu gani?. He is somebody kama Mwenyekiti wa Chadema lakini hana nguvu yoyote nje ya Chadema!. As an opposition leader ni kweli Mbowe commands much respect lakini you can't compare na PM!.
Namshauri awahi haraka sana kuweka msimamo wake wazi bila hivyo atapigwa chini kwani hatakuwa anasaidia nchi au chama
Atapigwa chini na nani kwa kosa gani?. Kama Mama amemkubali, ni amemkubali, subirini tuu 2025 amalize kipindi chake kwa amani. Tusitake kumpangia Mama kazi!.
P
 
Back
Top Bottom