kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Timu ziko nyingi kwanini iwe wasemaji wa Azam, Simba na Yanga tu wahamasishe timu ya taifa? Kama ni kwaajili ya kuwa na mashabiki wengi lakini kuna ushahidi gani kuwa Azam ina mashabiki wengi kuliko KMC na Coastal Union?
Pili, kuna wasemaji ambao huwa wanajigamba hadharani kuwa timu zao zimetoa wachezaji wengi taifa stars kuliko timu nyingine pale ambapo uteuzi wa timu ya taifa umechagua wachezaqji wengi kwenye timu yake kuliko timu nyingine, hii ndiyo mbaya zaidi kuliko hata hiyo sababu ya kwanza.
Kauli kama hizi zinasababisha dhambi mbili kuu kutendwa, mashabiki wa timu nyingine kujiona kama sio sehemu ya timu ya taifa, hivyo kususia kwenda kwenye mechi; na pili, inaweza kusababisha uteuzi wa timu uzingatie kubalance wachezaji wa timu badala ya kuteua kwa kufuata ubora.
Soma Pia: Yanga, Simba na Azam kununua goli milioni 5 ili kuipa hamasa Taifa Stars
Majigambo kama haya ya kitimu kwenye jambo la taifa ni utoto kabisa, halina faida kwa Yanga na Simba wala kwa timu ya taifa wala kwa mashabiki.