Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 7,672
- 9,039
Baada ya kifo cha Magufuli na Samia Suluhu Hassan kuanza kuachana na yule aliyemtengeneza, kumekuwa na juhudi za makusudi kwake na chama cha Mapinduzi kushikilia dola. Hata hivyo, wawili hawa wanajua kuwa bila ya kura za Kanda ya Ziwa, hakuna anayeweza kushika madaraka nchini.
Tokana na utendaji na ushawishi aliokuwa nao Magufuli, yeyote anayejitahidi kumweka kapuni ataishia mwenyewe. Kuepuka balaa hili, Samia alipinda katiba na kumteau Dotto Biteko kuwa naibu waziri mkuu cheo ambacho ni upotezaji wa fedha za umma mbali na kutokuwamo kwenye katiba.
Janja ya pili ni kumpa Stephen Wasira umakamu mwenyekiti wa CCM mbali na kuteua mawaziri kama Innocent Bashungwa na Stagomera Tax wanaotoka mikoa ya Mwanza na Kagera wakati Biteko anatoka Geita. Kwa vile mkoa wa Mara mmoja wa mikoa ya Kanda ya Ziwa haukuwa na waziri. Hivyo, wameamua kumpa umakamu mwenyekiti Wasira ili kuirubuni mikoa husika isiwapige kibuti.
Je hii janja itafanikiwa na kuiwezesha CCM kuendelea kushika dola mbali na uchakachuaji wa uchaguzi? Je hii janja itaepusha mgawanyiko ndani ya chama baada ya magwiji kama Makamba na Kinana kuonekana kujiweka mbali nayo?
Je janja hii itazima hasira za wale waliokuwa wakimuunga mkono Magufli walioutupwa nje ya ulaji?
Je bila Kanda ya Ziwa, ccm inaweza kuendelea kushikilia dola?
Je bila Kanda ya Ziwa, Samia anaweza kuwa rais tena baada ya kuupata kwa mkono wa Mungu?
Karibuni tujadili na kudadavua pamoja.