Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Tokea Mwenyekiti wa Chadema, shujaa Freeman Mbowe, atoke jela, siku chache zilzopita, alikokuwa amekaa zaidi ya miezi 8 kwa Kesi ya michongo ya ugaidi, amekuwa alisisitiza Sana neno HAKI kuwa likidumishwa nchini, Taifa letu litapona.
Hata kwenye maandiko matakatifu ya Biblia, kitabu cha Mithali 14:34 imenenwa "Haki huinua Taifa" mwisho wa kunukuu.
Hivi inakuwaje Katika nchi yetu, tuwaachie Polisi watende mambo wanavyotaka wao, halafu wasichukuliwe hatua yoyote??
Tumejionea Katika Kesi ya "michongo" ya ugaidi iliyofunguliwa mahakamani namna Polisi wetu walivyothibitika bila shaka yoyote, namna wanavyoweza kumbambikia mtu Kesi kubwa, kama hii ya ugaidi, pasipo kuwajibishwa.
Tumejionea namna mhimili wetu wa Mahakama, ambao ndiyo tunaoutegemea utende HAKI nchini, namna ulivyokuwa "umemezwa" na mhimili mwingine wa Serikali na kutoa maamuzi yaliyoacha maswali mengi nchini na nje ya nchi.
Hivi inakuwaje viongozi wetu wakuu wa dini waendelee kutuhimiza wananchi tuendelee kudumisha AMANI nchini, huku hawakemei watawala wetu wakishirikiana na Polisi wakiendelea kutotenda HAKI kwa wananchi wao?
Tulijionea namna uchaguzi mkuu ulivyoendeshwa nchini, bila kufuata misingi ya HAKI, huku wasimamizi wa kura, wakiwatimua mawakala wa vyama vya upinzani nchini, huku zoezi hilo likisimamiwa kikamilifu na Polisi wetu!
Kuanzia hivi sasa iwe ni wajibu wa kila mzalendo nchini, apaze sauti kubwa kadri awezavyo kila siku, kuhimiza itendwe HAKI nchini Ili tudumishe AMANI nchini.
Kwa kuwa AMANI ni tunda la HAKI