Bila kuwa na ndoto zilizo hai ni ngumu kufikia malengo yetu.

Bila kuwa na ndoto zilizo hai ni ngumu kufikia malengo yetu.

S.N.Jilala

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2012
Posts
540
Reaction score
507
BILA KUWA NA NDOTO ZILIZO HAI NI NGUMU KUFIKIA MALENGO YETU.


Je, wewe una NDOTO gani?. NDOTO zako/yako ni hai?.


Mwalimu Masanja ni kati ya walimu wanaopenda kufundisha kwa mifano na vitendo. Na njia anayoipenda kuitumia akiwa anafundisha darasani ni NJIA SHIRIKISHI.


Siku moja akiwa anafundisha wanafunzi wake wa kidato cha nne aliwasisitiza sana kusoma kwa bidii ili waje kuendelea na elimu ya juu yaani Chuo Kikuu na kuweza kufanikisha NDOTO zao walizo nazo kwa sasa. Na hapa Mwalimu Masanja yuko darasani anafundisha kwa njia anayoipenda sana yaani njia SHIRIKISHI.


Mwalimu Masanja: Eheeee, John ebu liambie darasa wewe una NDOTO zipi katika maisha yako baada ya kumaliza Elimu ya juu yaani Chuo Kikuu?


John: Kwanza nitasomea masomo ya uhasibu, nikimaliza tu nitafanya juu chini ili nipate kazi Benki Kuu ya Tanzania au Benki yoyote hapa nchini. Baada ya mwaka mmoja nikipata kazi nitanunua gari nzuri sana aina ya Harrier au Lexus. Na mwaka unaofuata nitanunua kiwanja maeneo ya Masaki au ikiwezekana nitakaa miaka miwili ili ninunua nyumba kabisa maeneo ya Masaki au Mbezi Beach. Pia, baada ya hapo, mwaka wa tatu au wa nne kazini, nitafungua maduka mawili la kwanza ni la Nguo ambalo litakuwa Kariakoo na lingine la vipodozi nitaliweka Sinza. Kupitia maduka hayo nitakuwa nina pesa sana Mwalimu. Na mwisho kabisa nitaoa mwanamke mzuri na anayemucha Mungu. Hizo ndizo ndoto zangu kwa ufupi alisema John na kushangiliwa sana na wanafunzi wenzie.


Mwalimu Masanja: Duuuuuuuh!!!! John, NDOTO zako kubwa sana, ukisoma kwa bidii yote haya aliyoyasema John yanawezekana kabisa. Lakini John ndoto zako zikigoma usiibe kwani ukikamatwa na kutiwa hatiani utafungwa maisha sawa.


John: Sawa Mwalimu sitaiba.


Mwalimu Masanja: Na wewe Amina NDOTO zako ni zipi?


Amina: Akaangalia juu ya darasa huku akitafakari amjibu Mwalimu. Baadae akauliza swali; Mwalimu si NDOTO nzuri ni ile inayokupelekea kuishi maisha Mazuri?


Mwalimu Masanja: Ndiyo Amina.


Amina: Mimi nahitaji maisha mazuri sana. Na baada ya kuelezea NDOTO zake John zimenivutia sana, tena sana. Na kusema kweli Mwalimu NDOTO zangu zimebadilika ghafla.Kwa hiyo ndoto yangu itakuwa ni fupi sana. John akishafanikisha NDOTO zake zote hapo juu aje anioe Mimi nitakuwa mke MWEMA na tutaishi maisha mazuri sana maana tutakuwa na kila kitu.


Darasa: Wanafunzi wote walivunjika mbavu kwa vicheko baada ya Amina kuelezea NDOTO zake kwa ufupi.


Ukifuatilia kwa makini Mwalimu Masanja na wanafunzi wake UTAONA kuna kitu cha kujifunza katika maisha yetu ya sasa. Je,tunajifunza nini hapo juu kuhusu NDOTO zetu?. Nawatakieni JUMAPILI njema na Tutafakari NDOTO zetu na kuzifanyia kazi.
 
Asante sana kwa ujumbe murua. Ila next time mkunbushe Mwalimu Masanja kuwa the best way ya kuifanya ndoto yako iwe halisi ni lazima uweke mipango inayotekelezeka. Juhudi binafsi ni njia kuu ya kukufikisha huko na kutokukubali kukatishwa tamaaa ni gundi ya kufanikisha ndoto yako. Kamwe usitishwe na Woga lakini kila unapoanguka, simama tena na sema hivi "hata hivyo nilijaribu"
 
kawahadithie darasa la tatu huko
Hata watu waliokuwa wamelazwa Milembe wanaruhusiwa kuccomment maana nao wana haki pia, maana madaktari waliwapima na kuwaruhusu....tatizo ugonjwa huu unachukua muda mrefu ndipo mgonjwa apone kabisa ni sawa na ukivuta BANGI.
 
Back
Top Bottom