Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 59,045
- 94,974
Hili la kudai kuwa Tanzania HAKUNA utawala wa sheria naona linazidi kusemwa kila siku. Sasa hebu tuweke hata kwa "hisia" Tu list ya matukio unaona yanathibitisha kukosekana kwa utawala wa sheria Huko Tanzania. Naanza na mfano huu:
1. Kunyimwa dhamana kwa makosa yanayodhaminika.....rejea kesi ya kiongozi wa CHADEMA kule Tanga ambapo mahakama, POLISI na MAGEREZA wako kimya kwa SABABU za kipumbavu.
2. Tukio au matamshi ya kichochezi yanayosemwa na VIONGOZI wa CCM bila kuchukuliwa hatua na POLISI, mfano statements za Tulia Ackson, Yule Dogo wa UVCCM Bukoba, yule DC alikua kiongozi wa UVCCM aliyewahi kusema "this time hatutatumia risasi tutatumia sindano za sumu".
3. Kupotea kwa Watu hasa wenye mrengo wa upinzani bila Polisi na mahakama kufanya Jambo Lolote la maana. Rejea hukumu ya kipumbavu mno ya mahakama kwa CHADEMA na Polisi kuhusu utekwaji wa kijana Deusdedit Soka na wenzake.
4. Matukio tofauti ya Wabunge tena Ndani ya bunge ya kuendelea kuisifia Serikali na kushindwa kuhoji wala kusimamia Serikali na hivyo kujikuta nao kujifanya ni sehemu ya Serikali.
Kwangu Mimi, matukio haya ya haraka haraka yanathibitishia kuwa Tanzania HAKUNA utawala wa sheria.