MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,252
- 8,003
Kwa matukio haya yanayoendelea kuripotiwa kwenye vyombo mbali mbali vya habari na mitandao mbali mbali ya kijamii ndani ya taifa letu ni kweli hatuko salama kabisa, mshikamano na umoja wa kitaifa haaupo tena. Imefikia hata sasa kila Mwananchi ukimsiliza anaongea kwa hofu na uoga mkubwa. Matumaini ya watu kuishi ndani ya taifa lao hayupo tuna.
Majeshi yetu ya ulinzi na usalama yatakua na kazi kubwa sana kupambana na matukio mbali mbali ya kutisha bila kikomo kama hatutapata kiungo muhimu wa kuwaunganisha watanzania kuishi kwa hofu ya mungu na upendo, tunatakiwa kusikia maneno yenye kutia moyo kulingana na hali halisi ilivyo. Tunatakiwa kuunganishwa kwa kuambiwa ukweli wa mambo pale yanapotokea matukio ya wazi yenye kututenganisha watanzania.
Yameanza matukio ya kutoweka kwa watu na ni zaidi ya miaka miwili sasa hawajulikani walipo, wanatekwa watu na kupotezwa kusikojulikana, mauaji ya kutisha kule wilayani Rufiji-Kibiti mkoani Pwani, Kuvamiwa kwa vituo vya redio na runinga, kuvamiwa kwa ofisi za mawakili na bado zinaendelea kuvamiwa, kupigwa Risasi kwa wanasiasa mfano wa Tundu Lissu juzi tu. Ni vipi kwa matukio haya tunaweza kusema kua taifa liko salama, tutasemaje kua mshikamano wetu upo?
Tusifikiri kuishi kwa mshikamano, amani na utulivu ni kazi ya vyombo vya ulinzi na usalama tuu, laahasha! Yanatakiwa kuzungumzwa maneno mazito yenye kuiondosha hofu iliyotanda kwenye nyoyo za watu. This is not a physical phenomenon, it needs a spiritual approach. Haya mambo ni wazi kua sheitwani anatembea na nyoyo za watu, hofu ya ukubwa wa Mungu haipo tena.
Madhara ya matukio kama haya hua ni makubwa sana, yanaweza kulibomoa taifa kwa muda mfupi sana. Kuanza kuishi kama maadui hakutaweza kulifikisha taifa letu mahali zaidi ya kurudi nyuma. Itatuchukua miongo mingi sana kuja kuwaweka pamoja watu walioishi kama maadui endapo jitihada na tahadhari za makusudi hazitachukuliwa hivi sasa.
Watakaolipasua taifa letu ni wachache kwa kujawa na uovu lakini watakaoumia ni wengi, taifa lenye idadi zaidi ya watu million 50 ni taifa kubwa sana hasa kwa kuzingatia maeneo na mpaka yetu. Hii hofu ya Mungu inayokosekana kwa kasi miongoni mwetu sisi italipeleka kupabaya sana.
Kama ni dini au siasa, kama ni utajiri au ushirikina, ni mambo ambayo wanaohusika waambiwe kwa namna ambayo wataelewa. Ni vipi Mungu ataweka watu wake pamoja endapo hawa watu hawajapenyeshewa hofu ya ukubwa wake. Huwezi kumuondosha mwenzako kwenye mgongo wa ardhi huku ukijua huna life span hata ya miaka 30 kwenye hii dunia? Ni nani mwenye mkataba wa Maisha yake na Mwenyezi Mungu?
Viongozi wa kisiasa na kiimani mnalo jukumu kubwa la kuliunganisha taifa hili, chochote kibaya kitakachotokea kwenye mgongo wa ardhi ambayo mmepewa mamlaka ya kukemea mtaulizwa. Hakikika hamtauepuka moto wa jehanam ikiwa mnakosa aina ya maneno ya kulinganisha taifa badala ya nisubiri shurti.