Watanzania tuna mazingira mazuri sana ya kupiga hatua kwenda mbele zaidi ya hapa tulipo.
Lakini tatizo letu ni nidhamu katika maisha yetu, kila kitu kinafanyika kiholela holela hakuna njia thabiti za kuhakikisha sheria na taratibu zote zinafuatwa.
Barabarani bodaboda hawana nidhamu, na hakuna sheria yoyote inayowasimamia vyema kuhusu uendeshaji wao na vigezo vya wao kuwepo barabarani.
Wamachinga wamevamia kila eneo kwa kigezo cha kutafuta mkate wao. Tazama stendi ya Magufuli, angalia stendi mpya ya Mwenge ilivyo na itakavyokuwa baada ya kufunguliwa.
Wamachinga watajaa kila sehemu na wakiondolewa wanasema wakale wapi. Kwani muda huu wanakula wapi?
Wafanyakazi serikalini wamekaa kwa nia ya kupiga dili sio kusaidia wananchi. Hawana nidhamu ya kazi wanawaza njia na mbinu za kupiga pesa.
Viongozi wamekosa nidhamu wanayumbisha sheria na taratibu ili kuwafurahisha wapiga kura wao kwa kuruhusu mambo yasiyo na tija kwa taifa kama ujenzi holela, wamachinga na bodaboda mijini.
Ni muda sasa wa kuhakikisha sheria zinafuatwa, kusiwe na mazungumzo na wasiofuata taratibu. Tusiwaze kura za kuwafurahisha wanaoharibu utaratibu likifanyika kwa mwaka mmoja tuu kila mtu atakaa sawa relini.