Bila rushwa ya pesa na vyeo, upinzani ungekuwa imara

Bila rushwa ya pesa na vyeo, upinzani ungekuwa imara

tripof

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2024
Posts
829
Reaction score
1,120
Nimekuwa nikitafakari sababu zinazopelekea upinzani kuwa dhaifu hapa nchini ukilinganisha na Kenya. Kwa haraka haraka, upinzani umekuwa ukidorora kwa vile CCM imekwisha gundua udhaifu wa wapinzani kuwa ni njaa ya Pesa na vyeo.

Hali inayopelekea kununulika haraka na kukimbilia Chama Tawala. Chama Tawala kina raslimali zote pesa, vyeo, dola na kila aina ya mifumo ya kugandamiza upinzani. Na mbaya zaidi, wananchi nao hupokea pesa na vitu mbalimbali kuwashawishi kukipigia chama tawala wakati wa uchaguzi, hii ni pamoja na kuwaghilibu wagombea kuvisaliti vyama vyao.

Kimsingi siasa na demokrasia ya uchaguzi imekuwa ni bidhaa kwenye soko la ushindani. Hakuna Uzalendo tena.Upinzani usahau kuchukua nchi kwa muktadha huu. Nawatakia mapambano mema uchaguzi ujao.
 
Sahihi, pia ruzuku na viti maalumu ni sumu mbaya kwa upinzani
 
Back
Top Bottom