Bila shaka nchi ya Tanzania ina kinga kali sana

Israel ni Nchi ya AHADI,

TANZANIA ni Nchi ya AGANO.

Imeandikwa Mungu atajiteulia TAIFA lake ktk siku za mwisho, Taifa hili litatumika kuwaficha WATAKATIFU wake dhidi ya Hila na utawala wa Mpinga kristo.

INJILI ya UFALME sawasawa na mathayo 24 itakayohubiriwa ULIMWENGUNI kote itahubiriwa Kutokea Tanzania.

SABABU ya umuhimu wake Kwa Dunia nzima, waliomo Tanzania lazima wachague upande, linakuja chujio la kuwatenga wema Kwa waovu Ili Ipatikane nafasi ya kuwatunza WATAKATIFU Kutoka mataifa mbalimbali duniani.

Tanzania ni kisiwa Cha AMANI, tangu zamani tumezisaidia Nchi nyingi kupata uhuru, limekuwa kimbilio la wapigania uhuru wengi kipangia mipango Yao ya Ukombozi, south Africa, msumbiji, Zimbabwe nk nk, hata Putin wa Russia,alipata uzoefubhapa akiwa kijana, Amani iliyopo Si Bahati mbaya.

Mshukuru Mungu Kuzaliwa TANZANIA, bt chukia sana Dhambi na UOVU, chukia USHOGA,na kumwaga Damu, maovu ndo hufanya Nchi ipate majanga Kutoka JUU sababu ya Damu kumwagika isiyo HATIA nk nk.

Mungu ibariki TANZANIA.

Amen
 
Kwahiyo unasema Samia alikuwa makamu wa raisi kwa kura halali za wananchi; March 19 aliapishwa kwa kura hizo hizo halali za wananchi sio?

Jiwe aliiba kura?
 
Nakuunga mkono yote uliyoyasema, LAKINI hapo kwenye USHOGA panahitaji TAFAKURI PANA KIDOGO.

Ukisema "tuchukie ushoga" unamaanisha nini? TUWAFUNGE JELA MASHOGA?
 
Nakuunga mkono yote uliyoyasema, LAKINI hapo kwenye USHOGA panahitaji TAFAKURI PANA KIDOGO.

Ukisema "tuchukie ushoga" unamaanisha nini? TUWAFUNGE JELA MASHOGA?
Wait and see what will happen.

Malawi wameona, Brazil wameona, Turkey wameona nk nk nk.

Utaona HAKIKA.
 
Asilimia kubwa kinachotuokoa sisi tunakubali 10% kabla mambo hayajawa mengi[emoji518]
 
Na hiyo dp nafananisha hiyo sura na haya maneno[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] hiyo sauti ninayo ipata balaa[emoji86][emoji86][emoji86]
 
Ewe mama yetu Tanzania tunakushukuru sana sisi watoto wako,


Huo ni ushirikina dhahiri, badala ya kumshukuru Mungu muumba wa nchi na Tanzania ikiwemo wewe unaishukuru nchi kitu kilichoumbwa na Mungu!!.

Ni Mungu ndiye anayestahiki kushukuriwa na sio kitu kingine chochote.
 
Nyerere hakuruka stage alipokuwa akiunda Taifa. Alianza na kuunda national unity. Hata wewe unapotaka kuondoa majanga kama chuki, husuda, umaskini, magonjwa, kulogana, kuendana kwa waganga katika familia(your extended family), tafuta kwanza kitu kinachoitwa unity. Ni national unity, national cohesion ndivyo vinavyoisaidia Tanzania.
Matumizi ya neno uzalendo katika vyombo vya ulinzi na usalama, katika ufanyaji kazi ndani ya serikali imeisaidia kuipunguzia Tanzania Sabotage. Jirani zetu, ukiacha majanga ya asili yasiyozuilika, kuna pia sabotage.
Janga halizuiliki lakini madhara yake yanapunguzika. Sasa kukiwa na sabotage ndani ya serikali na dola, basi madhara yatakuwa makubwa.
Pili ni maamuzi magumu yasiyohujumiwa. Mfano state inaweza ikaamua kufanyike karantini kwa watu waliopata ugonjwa. Basi hufanyika kwa ufanisi bila hujuma.
Tatu ni ujasusi wa ndani ulio imara. Unajua majanga mengine ni ya kuletewa ili tu tusumbuke, tupate tabu kama Taifa. Sasa intelligensia ikiwa kali basi husaidia katika kuepuka majanga ya yaletwayo na binadamu kama magonjwa.
Nne: Ni muundo wa utawala wa nchi kutoka juu hadi chini kabisa. Leo hii Rais akiagiza jambo mfano usafi wa mazingira, litatekelezwa hadi ngazi ya shina, balozi wa nyumba 10 kutoka Misenyi hadi Newala, Kalambo hadi Mkinga, Longido hadi Tunduma, Kigamboni hadi Manyovu, Tarakea hadi Mbamba Bay.
 
Magufuli alimtanguliza Mungu
 
Mbona majanga yalishatupata makubwa tu?
Mfano:
Kuzama Mv bukoba mwaka 1996
Mvua za mafuriko ya Elnino mwaka 1998
Ajali ya Tren nk.
Pia kuna janga la "Jiwe" mwaka 2020 - mwaka 2022
 
Majanga mengi yanapita kushoto huenda ni upepo unapovuma
Ingawa na sisi yanatokea ila kidogo sana
Wana geography watasema
Maana tukisema sisi hatuna madhambi kama watoto wadogo sio kweli
Hakika, au kutotoa taarifa sahihi kuzuia taharuki kwa watu hasa yakiwa sio ya asili
 
watanzania sisi japo hatujui sisi sio wa kubezwa hata kidogo, bila shaka tuna sehemu yetu kwenye ufalme wa Mungu.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Hapa nikasema subiri kwanza Micheke kidogo duuuh 🀣
 
Hizi hapa silaha za Mungu

1. Earthquakes
2. RAINFALLS
3. Thunderstorms
4. Fire Storms
5. Lightings

Ukiona Ardhi imepatwa na mambo haya....., basi ni wazi Mungu anakua anataka wakazi wa Ardhi ile wajitafakari na kujitafuta sana.
Kwa hio KIGOMA na RUVUMA na majanga ya radi hata mvua isiponyesha imekaaje hapo wajitafakari mara 4 na kujitafuta mara 70 na 7 ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…