Mkwawa
JF-Expert Member
- Jun 8, 2011
- 1,334
- 1,466
Katika tukio la ugaidi la mwaka 1998 ambapo kulitokea kitendo cha kulipuliwa kwa ubalozi wa Marekani Tanzania, magaidi walitumia watu wengi sana bila kujijua, Dereva aliyepeleka bomu alijua kabeba maji, aliyetengeneza lile tank yaani karakana ya Thomas Lyimo alijua anatengeneza tank la maji. Waliopokea wageni walifikiri wanapokea wageni wema. Kumbe kuna kazi maalumu.
Arusha tumepatwa na simanzi, mshtuko na maafa makubwa. Polisi, usalama wataifa, Jeshi la wananchi naomba tufanye kazi kwa ujuzi, weledi, miiko sio kutoa majibu kwa shinikizo la wanasiasa na kutesa watanzania wasio na hatia na kuwafungulia kesi zisizo wahusu. Jifunzeni kwa wenzenu jinsi wanavyoendesha upepelezi, hii ni taaluma haihitaji akili za akina Mulongo au mwana siasa awe yote, huhitaji akili za Pinda, Nchimbi ili kubaini wahalifu, hawa tayari wanayao kichwani. KURA.
Msifanye uchunguzi kwa shinikizo, ili kutoa majibu ya kubalance story, iiteni beleshi beleshi, mtathaminika sana ndani na nje ya jamii.
Ndugu wanausalama haiingii akilini kwanini manataja jina moja au mawili kati ya watuhumiwa kumi mlionao, kama mnaona kazi ya upepelezi bado mnaharaka ya kwenda wapi?? Raisi kasema eti mmekamata kwa kushuku tu, Mawaziri wanasema mmekamata kumi ila majina ni mawili ambayo yako hadharani. Hao nane wanakinga gani??
Kumbukeni mnavyozidi kucheza siasa ndio mnakimbiza ushahidi. Hili linatufanya tuamini mnaendeleza uchunguzi kama wa Marehemu Mwangosi, ambapo pamoja na kwamba kila jicho alishuhudia lakini danadana mpaka leo. Ulimboka alitekwa na watu wanaojulikana mkatulitea jina la kikenya ambalo uwezekano hakuna mtu mliyemkamata ni mkubwa sana. Kibanda katolewa jicho, meno, Mkaanza na kumtupia lawama Lakwatare ikawashinda mpaka sasa mnarukaruka kama samaki. Padri kauwawa mmekosa jibu , kapigwa risasi mmeshindwa kwa sababu ya siasa kuingizwa kazini.
Sheikh kachomwa kisu mkamalizia kwa kusema eti ni wezi wa mahindi, sheikh kamwagiwa Tindikali mpaka leo hatujui kwanini. Haya yote yanazidisha hasir akwa wananchi na kukosa kabisa imani na vyombo vyetu vya usalama.
Leo mnakamata waendesha bodaboda, halafu bila maelezo ya kujitosheleza mnataka kutuaminisha ndio waliopanga na kukamilisha ulipuaji wa kanisa la Olasik, kwa sababu gani, dereva wa bodaboda aliwapata wapi bomu? Ana hasira ya nini na balozi wa Vatican kwanza inawezekana hata alikuwa hajui kama kuna balozi anakuja, na hii si kwasababu ya majina yao hata angekuwa na jina gani, siamini dereva wa bodaboda anaweza kupata bomu sokoni na kulirusha kanisani kwa manufaa gani?? Hakuna Mtanzania masikini raia wa kawaida awe mkristu, muislamu au dini yeyote mwenye chuki ya kuuwa wenzeka. Wengi wenye chuki hizi ni wale wenye uwezo, madaraka, wasomi, na wenye uchu wa madaraka yawe ya dini, siasa, biashara nk.
Bomu la Arusha ni zaidi na dereva wa bodaboda, naomba wapepelezi wetu rudini kwenye drawing board, msione haya kuomba msaada. Acheni kabisa kudeal na wanasiasa wao wanatafuta KURA na huruma kwa matukio ya kuuwawa sisi. Ndivyo wanavyofanya, watafanya tayari wanafanya.
Updates

Kabla ya Mei 5, mwaka huu, jina la Victor Ambrose (20), halikuwa likijulikana miongoni mwa jamii kubwa ya wakazi wa Jiji la Arusha. Hali kadhalika, kwa Watanzania wengi.
Lakini baada ya tarehe hiyo, jina lake lilianza kujulikana nchi nzima na pengine kimataifa kwa kuhusishwa na tukio la kigaidi la mlipuko wa bomu katika Kanisa Katoliki la Parokia ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Olasiti jijini Arusha.
Parokia hii mpya awali ilikuwa ni kigango cha Parokia ya Burca, ambako ndiko pia yapo makazi ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Arusha, Josephat Lebulu, na uzinduzi uliotarajiwa kufanyika Jumapili iliyopita, ilikuwa ni kukipandisha hadhi kigango hicho kuwa parokia kamili.
Hali ilianza kwa shamrashamra, waumini wengi walionekana kuwa na nyuso za furaha, ghafla shamrashamra zao zilizimwa muda mfupi baadaye kabla ya uzinduzi wenyewe na hali ya simanzi ikatawala.
Tukio la mlipuko wa bomu kanisani hapo lilitokea siku ya kuzindua jengo la kanisa hilo, uzinduzi ambao ulikuwa umepangwa kufanywa na Balozi wa Vatican nchini, ambaye ni mwakilishi wa Baba Mtakatifu, Askofu Mkuu Fransisco Padilla, akishirikiana na mwenyeji wake, Askofu Mkuu Lebulu.
Hata hivyo, uzinduzi huo ulikatishwa kwa tukio la mlipuko wa bomu hilo ambao hadi sasa umesababisha vifo vya watu wanne na zaidi ya 66 kujeruhiwa.
Ilikuwa ni asubuhi muda ambao mvua zilikuwa zikinyesha, baadhi ya waumini wakipika chakula kwa ajili ya mlo wa mchana, huku ibada ikiwa ndiyo kwanza imeanza kwa Balozi Padilla, kupiga ishara ya msalaba na kubariki maji.
Umati mkubwa wa waumini kutoka parokia mbalimbali mkoani hapa, unaokadiriwa kufikia zaidi ya watu 2,000 hivi, ulikuwa umejitokeza kuhudhiria uzinduzi wa parokia hiyo.
Baada ya kubariki maji hayo, Askofu Mkuu Padilla, alitaka kunyunyiza maeneo mbalimbali na huku akiwa ameshika kifaa cha kunyunyizia, ghafla mtu mmoja ambaye bado hajakamatwa akiwa nyuma ya watu na nje ya uzio, alirusha kitu kinachoelezwa kuwa bomu kwenye mkusanyiko huo. Haijafahamika mlengwa alikuwa nani, lakini mtazamo wa wengi hauweki shaka kwamba mlengwa Askofu Mkuu Padilla.
VICTOR AMBROCE NI NANI?
Huyu ni dereva wa pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda, kazi ambayo aliianza tangu aliposhindwa kuendelea na masomo yake ya sekondari mwaka 2011 akiwa amefikia kidato cha pili.
Alimaliza elimu ya msingi katika Shule ya Terrat, mwaka 2009, na akaendelea na masomo ya sekondari katika Shule ya Oljoro, zote za mkoani Arusha.
Victor, anaelezwa na bibi yake, Lucia Victor, kuwa katika familia yao walizaliwa watoto wawili, yeye akiwa ni mtoto wa pili kwa wazazi wake ambao wote wawili walishatangulia mbele ya haki. Kaka yake anaitwa Philip.
Bibi Lucia, anasema tangu kufariki dunia kwa wazazi wake, amekuwa akiwalea watoto hao mpaka hapo walipofikia, na kwamba wanaishi eneo la Kwa Mromboo kama linavyotamkwa na wakazi wa Jiji la Arusha.
"Wazazi wa Victor wote walifariki dunia, na mimi ndiye nimekuwa mlezi wao tangu wakiwa watoto wadogo," anasema Bibi Lucia.
Bibi Lucia anasema familia yao pamoja na mjukuu wake, ni Wakristu wa madhehebu ya Katoliki. Anasema wanasali kwenye kigango cha Kwa Mromboo, cha Parokia ya Sombetini. Anamwelezea mjukuu wake kwamba hajawahi kumuona akinywa pombe, kuvuta sigara au kutafuna mirungi.
SIMULIZI KUTOKA KIJIWE CHA BODABODA:
"Tunamfahamu Victor, na hapa ndiyo kijiweni kwake," anaeleza dereva mmoja wa bodaboda. Hata hivyo, dereva huyo alikuwa na wasiwasi mkubwa hata kule kusema tu kwamba hapo ndipo palikuwa ni kijiwe chake, lakini mara kwa mara alikuwa akitaka kujua ni nani anayeongea naye.
Na baada ya kuelewana naye alianza kunielekeza eneo analoishi ingawa alisema hajui nyumba yake ni ipi isipokuwa eneo.
Dereva huyo alikuwa msaada kwangu kwani baadaye alinipa namba ya Mwenyekiti wake wa Jumuiya ndongo ndogo za Kikristo za Kanisa Katoliki na bila kusita nikampigia na kumweleza shida yangu.
Mwenyekiti huyo alikuwa mbali na eneo hilo kwa shughuli za ujenzi na akasema asingeweza kuwahi kwa muda huo, lakini alinielekeza na kufuata ramani hiyo niliweza kuifuata hadi nyumbani kwa Victor, kama vile unaelekea Oljoro.
Baadhi ya wenzake katika kijiwe hicho wanasema kuwa Jumapili Victor alikodiwa na mtu asiyemfahamu ampeleke kanisani na alikubali. Lakini baaada ya kufika, mkodishaji aliteremke na kukimbia bila kumlipa na kwamba wakati anamfuatilia amlipe fedha zake, ghafla ulitokea mlipuko.
Wanasimulia kuwa baada ya mlipuko huo hakumuona aliyemkodi zaidi ya kujikuta akiwa amevamiwa na watu waliokuwa karibu na eneo la kanisa hilo wakimgang'ania kuwa ndiye aliyefika eneo hilo na mlipuaji.
HALI ILIVYO NYUMBANI KWAKE
Majirani wachache na wote akina mama ndiyo waliokuwapo hapo. Ilikuwa nyakati za jioni na walikuwa wenye nyuso za wasiwasi.
Hali hiyo ilinifanya nianze kwa kuwapa pole na kuwafariji kwa yote yaliyotokea nao wakanikaribisha ndani na kuanza mazungumzo huku sauti ya nyimbo za kwaya ikisikika kwenye redio yao, baadhi yao walikuwa wakipika kuandaa chakula cha jioni.
Baadhi ya majirani walisema walipokea kwa mshangao tukio la kukamatwa kwa Victor kwa maelezo kwamba hakuwa wamesikia kama ana matatizo yoyote.
PAROKIANI ST. JOSEPH
Paroko wa Parokia ya Burca, Padri Peddy Castelino, ambaye kigango cha St. Joseph kipo kwenye parokia yake, anasema licha ya kutokea kwa tukio hilo, bado shughuli za misa zinaendelea kama kawaida asubuhi.
Wakatoliki wana kawaida kuadhimisha Misa Takatifu kila siku, maadhimisho ambayo Padri Peddy anasema wanayafanya kwa waumini wa kanisa hilo la St. Joseph.
Mazingira katika eneo hilo la kanisa yapo vile vile, huku walinzi wachache wa kanisa wakilinda viti na vifaa vingine vilivyotumika kwa siku ya uzinduzi. Meza, viti na vitu vingine vimeachwa hapo hapo na pia viatu vya watu vilivyovulika wakati wa purukushani navyo ni vimeachwa hivyo hivyo.
Hakuna ulinzi wa askari waliovaa sare au wale waliovaa kiraia huku wakiwa wameshika bunduki, lakini kwa mbali na eneo hilo kulikuwa na gari la polisi aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili PT 0591, hali inayoashiria kuwa ulinzi upo katika eneo hilo.
Akielezea mahusiano na majirani zao, Padri Peddy, anasema hawana ugomvi wowote na majirani zao tangu waliponunua uwanja huo hadi kukamilika kwa ujenzi.
"Hatuna ugomvi wo wote na majirani zetu, tunaishi nao vizuri tu," alisema