Bila uchunguzi wa kisayansi tutafunga kuku: 1998 dereva wa lori alikufa

Mkwawa

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2011
Posts
1,334
Reaction score
1,466
Katika tukio la ugaidi la mwaka 1998 ambapo kulitokea kitendo cha kulipuliwa kwa ubalozi wa Marekani Tanzania, magaidi walitumia watu wengi sana bila kujijua, Dereva aliyepeleka bomu alijua kabeba maji, aliyetengeneza lile tank yaani karakana ya Thomas Lyimo alijua anatengeneza tank la maji. Waliopokea wageni walifikiri wanapokea wageni wema. Kumbe kuna kazi maalumu.

Arusha tumepatwa na simanzi, mshtuko na maafa makubwa. Polisi, usalama wataifa, Jeshi la wananchi naomba tufanye kazi kwa ujuzi, weledi, miiko sio kutoa majibu kwa shinikizo la wanasiasa na kutesa watanzania wasio na hatia na kuwafungulia kesi zisizo wahusu. Jifunzeni kwa wenzenu jinsi wanavyoendesha upepelezi, hii ni taaluma haihitaji akili za akina Mulongo au mwana siasa awe yote, huhitaji akili za Pinda, Nchimbi ili kubaini wahalifu, hawa tayari wanayao kichwani. KURA.

Msifanye uchunguzi kwa shinikizo, ili kutoa majibu ya kubalance story, iiteni beleshi beleshi, mtathaminika sana ndani na nje ya jamii.

Ndugu wanausalama haiingii akilini kwanini manataja jina moja au mawili kati ya watuhumiwa kumi mlionao, kama mnaona kazi ya upepelezi bado mnaharaka ya kwenda wapi?? Raisi kasema eti mmekamata kwa kushuku tu, Mawaziri wanasema mmekamata kumi ila majina ni mawili ambayo yako hadharani. Hao nane wanakinga gani??

Kumbukeni mnavyozidi kucheza siasa ndio mnakimbiza ushahidi. Hili linatufanya tuamini mnaendeleza uchunguzi kama wa Marehemu Mwangosi, ambapo pamoja na kwamba kila jicho alishuhudia lakini danadana mpaka leo. Ulimboka alitekwa na watu wanaojulikana mkatulitea jina la kikenya ambalo uwezekano hakuna mtu mliyemkamata ni mkubwa sana. Kibanda katolewa jicho, meno, Mkaanza na kumtupia lawama Lakwatare ikawashinda mpaka sasa mnarukaruka kama samaki. Padri kauwawa mmekosa jibu , kapigwa risasi mmeshindwa kwa sababu ya siasa kuingizwa kazini.

Sheikh kachomwa kisu mkamalizia kwa kusema eti ni wezi wa mahindi, sheikh kamwagiwa Tindikali mpaka leo hatujui kwanini. Haya yote yanazidisha hasir akwa wananchi na kukosa kabisa imani na vyombo vyetu vya usalama.

Leo mnakamata waendesha bodaboda, halafu bila maelezo ya kujitosheleza mnataka kutuaminisha ndio waliopanga na kukamilisha ulipuaji wa kanisa la Olasik, kwa sababu gani, dereva wa bodaboda aliwapata wapi bomu? Ana hasira ya nini na balozi wa Vatican kwanza inawezekana hata alikuwa hajui kama kuna balozi anakuja, na hii si kwasababu ya majina yao hata angekuwa na jina gani, siamini dereva wa bodaboda anaweza kupata bomu sokoni na kulirusha kanisani kwa manufaa gani?? Hakuna Mtanzania masikini raia wa kawaida awe mkristu, muislamu au dini yeyote mwenye chuki ya kuuwa wenzeka. Wengi wenye chuki hizi ni wale wenye uwezo, madaraka, wasomi, na wenye uchu wa madaraka yawe ya dini, siasa, biashara nk.

Bomu la Arusha ni zaidi na dereva wa bodaboda, naomba wapepelezi wetu rudini kwenye drawing board, msione haya kuomba msaada. Acheni kabisa kudeal na wanasiasa wao wanatafuta KURA na huruma kwa matukio ya kuuwawa sisi. Ndivyo wanavyofanya, watafanya tayari wanafanya.

Updates
 
CCM bwana, wanaingiza siasa hata sehemu zinazohitaji utaalam na wataalam walio bobea.
Hivi Pinda alienda kufanya nini Arusha?
 
Haya majibu ya polisi wa bongo hayana tofauti yule form four aliyemchora mess!
 
CCM bwana, wanaingiza siasa hata sehemu zinazohitaji utaalam na wataalam walio bobea.
Hivi Pinda alienda kufanya nini Arusha?

alienda kuwaambia modokta. Kuwa kila kipande cha chuma wanachokitoa ktk mwili wa majerui wakipeleke kwa magesa mulongo kwa ajiri ya upelelezi
 
Mkwawa umesema... Ni wakati wa tiss, na vyombo vingine kuonyesha 'kazi' iliyotukuka. Ikibidi watoke hadharani na kujulisha wananchi kuwa uchunguzi unaendelea na kama utachukua muda, wawe wakweli maana usalama wa nchi umechezewa tayari...
 
Mkwawa umenena. Nilishajiuliza humu haraka ya kutaja lile jina moja ilikuwa ya nini? Siku zote polisi wetu hawana haraka kabisa ya kutaja majina ya watuhumiwa, wakati mwingine mpaka wanapowafikisha mahakamani, sababu ikiwa wakitaja watavuruga upelelezi. Kwa hili hsraka ilikuwa ya nini, kama siyo kuscore matakwa ya kunfi fulani? Wapelelezi wenye weledi katika tukio kama hili cha kwanza kufanya baada ya kuwasaidia mahanga/waathirika ni kuhifadhi sehemu ya tukio na kuhakikisha vitu vyote vilivyopo hapo havichafuliwi. Hapa kwetu hiki hakifanyiki, wakifika wstu hapa na hasa viongozi, wakiwemo viongozi wa polisi wote ni wajuzi. Watagusa kila kitu na kujidai kutoa maelexo ambayo mengine hata hayana maana. Nilishangaa jana kumsikia Waxiri Mkuu akiagiza madakitari kuhakikisha chembechembe za vyuma vinavyotolewa kwenye miili ya waathirika viifadhiwe vizuri kwa uchunguzi! Hii haihitaji Waziri Mkuu kuagiza adharani, wapelelezi wanapaswa kufanya kazi na madaktari siyo tu kupata vyuma hivyo hata aina ya majeraha.Jana wakati Bunge linapitisha bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani nilishangaa sana wabunge kupinga hoja ya kuliunda upya. Nani wakiwemo hao wabunge hawajui muunfo wa polisi ulivyokuwa compromised na kuwafanya wasifanye kazi yao kwa weledi na ufanidi? Nani hajui jinsi polisi wanavyobambnikizia watu kesi za ajabu? Taarifa ya habari ya ITV saa mbili leo inaonyesha kiundfi cha polisdi kinambambikizia mtu kesi ya mfanyabiashara kukutwa na kichwa cha mtu (walichokiweka wao) huko Morogoro - na hii pengine ni kutaka kuwaonyesha hao wabunge hali halisi!Tusiingize siasa kwenye vyombo vyetu vya usalama polisi, TISS na JW.
 
CCM bwana, wanaingiza siasa hata sehemu zinazohitaji utaalam na wataalam walio bobea.
Hivi Pinda alienda kufanya nini Arusha?

Haa haa haa. Mkuu nimecheka sana! Nilisoma kwenye gazeti eti Pinda amawaagiza madaktari wasiitupe ile misumari wanayotoa kwenye miili ya majeruhi kwani itatumika baadae kwenye uchunguzi! Sisemi kuwa alitoa wazo baya ila nataka kuonyesha jinsi wapelelezi wa Tanzania wanavyoendeshwa na wanasiasa! Kwani wao walikuwa hawajui mpaka Pinda awaongoze namna ya kufanya upelelezi? Hata kama alikuwa usalama wa taifa lakini hii inaonyesha jinsi hapa kwetu mambo yanavyokorogwa na wanasiasa!
 
nchi si salama tena kila mwananchi ajitafutie mbinu yake ya kupambana na uhalifu kama tunavyopambana na umasikini.
Serikali imeshindwa kutuondolea umaskini,maradhi na ujinga na sasa imeshindwa hata kutulinda.zimebaki show za walinzi wa kiongozi mkuu wa nchi,madoido ya intercoms,suti nyeusi,mawani za jua na sukuma sukuma za hapa na pale huku madereva wa boda boda wakiachiwa kurusha mabomu kanisani.
Watanzania wanatamani mtoto azaliwe bila kucha kumuepusha na misukosuko ya makoleo ya kungo'lea kucha.
 
CCM bwana, wanaingiza siasa hata sehemu zinazohitaji utaalam na wataalam walio bobea.
Hivi Pinda alienda kufanya nini Arusha?

Si hoja yeye kufika pale mapema, ila hoja ni alichoongea kina mashiko?, kimepelekea adui kuogopa?, unakumbuka kauli ya bush pale ground zero dunia nzima ilijua america wamechukia na wanakuja sasa..
 
Nadhani wanataka kuonesha siuo suala la udini bali ni ugaidi. Okay. Mbona hayo mengine hayatajwi? Kwani huyo aliyekamatwa hajasema alikopata bomu? Vinginevyo wanyamaze hadi wakamate watu wote. Halafu hayo majina ni kama fake kwa kuwwa kataika hali ya kawaida jina moja lilitakiwa liwe la ukoo lakini hayo majina yote ni ya kistaarabu. Walau lingekuwapo moja la kishenzi.


Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Sijui viongozi wetu wanadhani wanaongoza watoto jamani!! Sijui tunaonekana hatuna ufaahamu? Sijui kwasababu tunaonekana hatuwezi ku react?

Wakiambiwa akili ndogo inaongoza akili kubwa wanadai wametusiwa. Kwa hili sijui wanawaza nini mpaka saivi kututajia jina moja uku wengine wakifaamika kama wasaudia!!! Na hivi wamerahisishiwa kwa kuambiwa haliusiani na udini tutasikia mengi yakushangaza zaidi ya hili.

Mmmh Tanzania yangu!!! ???.....
 

Shangaa tu nawewe unisaidie cse nilibaki mdomo wazi kwa muda niliposikia . Sijui hawa viongozi wakiwaonaga waandishi wa habari wanachanganyikiwa?
 
Hilo ndilo tatizo. Haraka haikuhitajika. Kwanza unataka kuonyesha kuwa siyo udini ili iweje? Kwani kulikuwa na vurugu za kulaximisha watu wajue kuwa aliyetupa bomu ana jina la Kikiristu? Sasa tuseme tu inakuja kuonekana kuwa huyu mtu alilipwa na mwenye jina la kiislamu kufanya hivi je hii itaonyesha kuwa ni udini? Weledi ulikosekana hapa. Tunatarajia bado kwamba polidi watatupa majibu ya kuondoa kiu yetu kwa sababu wamesha tuangusha huko nyuma katika matukio ambayo yana hisia kwa wananchi.
 
Kwa msimamo wa viongozi wetu wa sasa, mtu mwovu anaangaliwa kwanza dini yake halafu itikadi yake ya kisiasa. Vyombo vyetu vya usalama lazima viepuke mtizamo huo kwa gharama yoyote. Mwovu ni mwovu akiwa Muislamu au akiwa Mkristo. Akiwa shehe au akiwa Askofu! Nadhani sababu ya kutaja harakaharaka jina la Dereva wa bodaboda na kuwaacha wengine ni kwa kuwa ni Mkristo. Tayari hadi hapo mmeshanasa. Aliyeshiriki ugaidi huo ni gaidi tu bila kujali dini yake. Msijaribu hata kubalance kama ambavyo viongozi wetu wanavyofanya. Msifikie mahali pa kusema magaidi wale nusu ni waislamu na nusu ni wakristo. Ni wauwaji tu bila kujali dini zao. Tumeona dalili za kushughulikia matatizo ki hivyo. Makanisa yamechomwa lakini badala ya kuwakamata wahalifu inasemwa, lakini hata misikiti imechomwa pia. Wote hao ni wahalifu. Msiangalie wamevaa nini! Anasakwa Shehe Ilunga lakini na Askofu Mpemba pia. Inafungiwa radio Iman ilakini na redio Kwa neema FM pia. Kanisa linalipuliwa anatajwa mtu mkristo na wengine hawatajwi. Na huenda huyu alikuwa dereva tu. Kama mtakuwa mnamtafuta mhalifu na kunshughulikia bila kuangalia dini yake mtarudisha heshima yenu ambayo inaning'inia karibu kutumbukia shimoni. Mara ngapi wakati wa vurugu mmewagandamiza chadema kwa sababu ya itikadi ya kisiasa tu? Haya!!!!!
 

Mkuu umenena......siasa imevuka mipaka Tanzania....kila kitu ni siasa...hadi hali ya hewa....ni vema vitu vinavyohitaji utaalam visemwe na wataalam.....sijafurahishwa na mh waziri mkuu kutoa maelekezo ya kitaalam kwa madaktari kuhusu ukusanyaji wa vielelezo vya uchunguzi wa tukio hili.....kungekuwa na ushirikiano wa moja kwa moja kati ya wapelelezi, madaktari na mashahidi wa tukio bila kupititia kwa wanasiasa.....
 
Mara zote huwa najaribu kulinganisha mambo nayoyaona kwenye movie za holywood au hata tamthiliya ya isidingo tu then nalinganisha na zile show na tambo za mshereheshaji pale uwanja wa taifa najumlisha tena tambo za hao mabwana bar za uswailini"Unajua mi ni nani?"Huku akitoa kitambulisho au bastola basi nachoka naishiwa nguvu kabisa. Kwa maelekezo yale ya pm achilia mbali kuwa alikuwa usalama napata shaka hata kama aliwah soma vitabu vya Elvis Musiba vya Willy Gamba.
 
Nimeangalia taarifa ya habari ya saa mbili ITV daktari akieleza ilivyokuwa vigumu kutoa chembechembe za. Yuma. Ilivyoko kwa majeruhi kwa vile. Viliishia kwenye nyama. Nikajiuliza uhusiano wa ili na agizo la jana la Waxiri Mkuu. Bahati mbaya kila mwanasiasa na viongozi sasa wanataka kuonekana jinsi walivyo na huruma na wanavyofanya kaxi kwa bidii!
 
Hakuna Mtanzania masikini raia wa kawaida awe mkristu, muislamu au dini yeyote mwenye chuki ya kuuwa wenzeka. Wengi wenye chuki hizi ni wale wenye uwezo, madaraka, wasomi, na wenye uchu wa madaraka yawe ya dini, siasa, biashara nk.

Damn True...!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…