Shakoor Jongo na Musa Mateja
Diva wa kiwanda cha filamu Tanzania, Irene Uwoya Ndikumana ameendelea kusababisha viulizo vingi mitaani kutokana na ukaribu wake na baadhi ya wanaume wakati yupo mbali na mume wake, Hamad Ndikumana ‘Kataut'.
Tayari Uwoya ambaye ni Miss Tanzania namba 5 2006-07, alishahusishwa kutoka kimapenzi nje ya ndoa na staa wa African Stars International ‘Twanga Pepeta', Kalala Hamza Jr. ikahojiwa ukaribu wake na msanii, Juma Chikoka ‘Chopa' na Jumamosi iliyopita alinaswa ‘live' akiwa na wengine
The 5star Paper, Risasi Mchanganyiko lina kitu kamili, baada ya kumnasa Uwoya katika mapozi tata na wanaume wawili kwa nyakati tofauti kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Upanga, Dar ambapo kulikuwa na onesho la mwanamuziki kutoka DRC, Ferre Gola.
Kwa mujibu wa ushuhuda wetu ukumbini hapo, muda mwingi Uwoya alikuwa ‘amepozi' na jamaa mmoja (anaonekana picha kubwa mbele) na kwa namna walivyoonesha ukaribu wa kina, ilianza kuibua maswali ya hapa na pale.
Kutokana na uliza uliza ya baadhi ya watu ukumbini hapo, paparazi wetu alimkaribia Uwoya na kumuuliza uhusiano wake na jamaa huyo, na jawabu lake likawa: "Huyu ni bodyguard wangu, kwani kuna tatizo?"
Wakati Uwoya anatoa jibu hilo, alimsogelea zaidi jamaa huyo kuonesha kwamba hahofii kitu.
Baadaye, Uwoya alionekana na pedeshee mmoja (jina hatujalinasa), akiwa anampa kampani ‘mnene' huyo wakati anamtuza Gola jukwaani.
Baada ya kumaliza kutuza, Uwoya aliongozana na pedeshee huyo kwenye siti za VIP.
Mapaparazi wetu, walimnasa Uwoya kwa mara nyingine ‘shoo' ilipomalizika, wakati huo akiwa ‘beneti' na pedeshee aliyekwenda naye jukwaani kumtuza Gola.
Katika fuatilia yetu, paparazi wetu alipata picha ya Uwoya akiwa amebambiwa kiunoni na pedeshee huyo (tazama picha kushoto ukurasa wa kwanza).
Picha hiyo, pia inawaonesha wasanii Steven Kanumba ‘The Great' (mwenye koti jeusi na shati rangi ya fedha) na Vincent Kigosi ‘Ray' (nyuma ya Kanumba) wakishangaa kitu, wakati Uwoya yeye alitulia kwenye mkono wa pedeshee huyo.
Paparazi wetu, alimuuliza Uwoya pedeshee huyo ni nani wake lakini aligoma kusema chochote.
Siku inayofuata (Jumapili iliyopita), gazeti hili liliwasiliana na Irene kwa simu na kumuuliza kuhusu uhusiano wake na jamaa aliokuwa nao ukumbini na mazungumzo yalikuwa hivi;
UWOYA: Ahaa unamzungumzia yule niliyekuwa nimekaa naye?
RISASI: Yeah, huyo wa kwanza, ni nani wako?
UWOYA: Ni kampani yangu kama ilivyo kwa Ray au Kanumba.
RISASI: Achana na Ray na Kanumba, fafanua uhusiano wako na yule pedeshee.
UWOYA: Nimesema ni kampani yangu na siwezi kuzungumza zaidi ya hapo.
Mbali na mahojiano hayo, watu waliomshuhudia Uwoya Diamond Jubilee walikuwa na maswali mengi kama Ndikumana ambaye ni mwanasoka wa kimataifa wa Rwanda, anajua kila kinachoendelea kwa mke wake anapokuwa nchini.
Waliliambia gazeti hili kuwa wana hofu kwamba Ndikumana ‘Kataut' anayecheza soka la kulipwa nchini Cyprus, hajui kuhusu Uwoya nchini.
"Mwandishi umesema Uwoya amekwambia yule ni bodyguard wake, huoni kama kuna utani hapo? Pozi gani lile la mtu na bodyguard wake? Namna hii kweli au wanataka kuleta ile stori ya mke wa Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma (Nampumelelo Ntuli) aliyepewa mimba na mlinzi wake?" alihoji mdau wa filamu, Peter Haidark.
Shuhuda mwingine, Ras Bill wa Kigamboni, alisema: "Kuna haja hawa mastaa wetu wakapewa semina elekezi kuhusu life style inayowafaa. Haileti picha nzuri tunamfahamu ni mke wa mtu halafu anahusishwa kwa mambo haya na yale."
Huyo aliyetajwa ni bodyguard wa Uwoya anakuwa wa pili kupewa nafasi hiyo, kwani hata Chopa, naye amewahi kutajwa ni mlinzi wake baada ya kuonekana wapo pamoja muda mwingi.
KWELI NI MKE WA MTU NIMEAMINI MKUU
HIZO NI LATEST ZA GAZETI LA LEO ...
UWOYA: Mbona nilikujibu? Yule ni bodyguard wangu.
RISASI: Mlivaa nguo sare, mlimaanisha nini?
UWOYA: NI bodyguard wangu, sikuona tatizo kuvaa nguo za kufanana.
RISASI: Na yule pedeshee aliyevaa koti jeupe na jinsi ni nani wako?
UWOYA: Yule kampani yangu tu.
RISASI: Kampani yako kivipi?