Bwana Mohamed Said "upuuzi" hapa halikuwa tusi ni kinyume cha hoja yenye mantiki ile isiyo na maana ndio upuuzi sio tusi kamwe!! We ndugu yangu nilichosema mimi sio kuwa hatupendi au hatuwaenzi wapigania uhuru wetu la hasha!! Tena ifike mahali wapewe hadhi ya manabii wetu lakini katika context ya Utaifa na sio udini au ukabila Kaka!! Waikela kama yeye ni shujaa wa kumtoa mkoloni kwangu na naamini kwa Watanzania wengi ni mtu muhimu sana bila kujali dini yake au kabila lake. Hapo pia, haitegemei kutembelewa kwake na "mwanasiasa kijana aliye mashuhuri - Zitto Kabwe". Historia yetu imeandikwa na wageni sisi ndio sasa tunaamka kama anavyotaka kuamka rafiki yangu Paskali. Kama hao mashujaa hawakuthaminiwa au hawakutanjwa kwenye historia basi isiwe kuwa tuone ni kwa ajili ya dini zao bali tu kwa ajili ya kile walichokuwa wanakipigania ambacho mgeni alieandika historia hakukipenda. Wewe kama kijana wa sasa rekebisha ukisisitiza Utaifa na sio udini.
Kokola,
Wala sitakulaumu kwa kuona neno ''upuuzu,'' si tusi na mara nyingi
lugha mfano na hii yako nakutananayo hapa jamvini.
Kwetu siye hilo ni tusi.
Ingekuwa mimi ningeweza kuandikia sentesi hiyo hiyo bila ya kutumia
neno, ''upuuzi.''
Tofauti kati yangu mimi na wewe ni kuwa mimi kwanza ingawa hii nini
historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika kubwa ni kuwa historia hii
imewahusu wazee wangu.
Kwa ajili hii basi mimi nayajua mengi ambayo wewe huyajui.
Ukweli ni kuwa palikuwapo na bado ipo njama ya kuifuta historia hii
na laiti kama nisingeliandika historia hii mengi yasingejulikana.
Hili la Uislam katika historia ya TANU huwezi kuliepuka hata ukifanya
nini kwa kuwa ndiyo historia yenyewe ilivyokuwa na mifano iko wala
si ya kutafuta.
Waasisi wa African Association 1929 ndiyo hao walioasisi Al Jamiatul
Islamiyya Fi Tanganyika 1933.
Al Jamiatul Islamiyya ndiyo iliyotoa viongozi wa mwanzo wa TANU na
wanachama wake.
Mimi sijaona ubaya wowote katika kuandika historia hii.
Idd Faiz Mafungo kadi yake ya TANU ni No. 25 na yeye ndiye alikuwa
mweka hazina wa Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika na pia mweka
hazina wa TANU.
Idd Faiz ndiye aliyekuwa mkusanyaji wa fedha za kumpeleka
Nyerere UNO
mwaka wa 1955.
Umepata popote kumsikia akitajwa?